Video: Rudia kusikiliza maneno yaliyomtia matatani Lissu; Serikali ilichukua hatua mwafaka

Video: Rudia kusikiliza maneno yaliyomtia matatani Lissu; Serikali ilichukua hatua mwafaka

View attachment 3322296

Yeye mwenyewe Tundu anasema anataka nafasi fulani, hataipata kwa sheria hii ya uchaguzi. Inabidi aanzishe uasi na walio tayari. Anaendelea kusema akianzisha uasi atakinukusha, uchaguzi hautafanyika. Atakamatwa, atashtakiwa kwa uhaini....
Harafu unakutana na TEC wanasema atolewe , upuuzi matupu
 
Mimi sioni kosa lake! Viongozi wengi wa ccm wametoa kauli nyingi za kiuchochezi tena zaidi ya hayo maneno lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwao! Sisi wananchi huu ni uonevu tu kwa vyama vya upinzani! Nendeni kenya mkajifunze maana ya demokrasia ya vyama vyingi!! Mwacheni tundu lissu
Mahakama itasema, Serikali ilichofanya ni kumtuhumu tu kisha kumshitaki
 
Kwenye video kaanza na maneno …” wanasema hivi…”
Hao wanao sema ni akina nani? Si maneno yake…
Mpaka hapo tayari kachomoka…
Katika maamuzi ya maana yaliyofanyika na Serikali ya Rais Samia kulinda amani na utulivu wa nchi yetu, ni kumfungulia mashtaka Tundu ambaye alikuwa anapanga kuanzisha uhalifu ili KUKINUKISHA.

Wahenga walisema UKICHEKA NA NYANI UTAVUNA MABUA. Na mdharau mwiba huota tende.
 
Sio mpumbavu tu. Hana akili kabisa.
Tatizo mkuu Lord denning mumemfanya Tundu ni kama nabii au malaika wenu. Hamtaki akosolewe, laiti mungekuwa mnasahihisha anapokosea, kamwe asingetoa ile kauli.

Ananyea debe Ukonga, nyie mko huku MNAKINUKISHA kama ma key board warriors
 
Maneno ya Lissu hayana shida yeyote. Shida ni upumbavu ulionao na kukosa akili tu.
Kama hayana shida mbona kakamatwa na wewe hujakamatwa?

Basi mwambie Makamu Mwenyekiti John Heche ayarudie kwenye mikutano yake
 
Na kwenye video hiyohiyo baada ya kusema "wanasema hivi" alithibitisha kwa kusema "ni kweli tutahamasisha uhasi" hadi hapo hachomoki ame confess kupanga mbinu za uhasi
Uasi maane yake ni nini ?
Kumbuka hupiga kura ni uasi.
Kushawishi watu waipigie ACT ni uasi
Kufanya campaign ni uasi

Je uasi ndio uhaini?
Acheni kumsumbua mtu wa watu huko gerezani.
 
Sasa hilo jibu ndiyo Tundu atatuambia akiwa kizimbani
Kumbe Shida ni kuambiwa tu ili mtafute plan B yake? Maana mpaka sasa - tafsiri ya maneno “ kukinukisha” bado no Ngumu.
Kuzuia uchaguzi bado haijulikani atafanyaje…
Kaeni mezani muyamalize.
Hivi Kikwete aliwezaje ku deal na huyo Lissu na sasa nyie mumeshindwa?
 
Unaongelea Dunia ipi hiyo? Tatizo wewe na wenzako wengi hamna exposure na wala hamfuatilii global issues mnajiropokea tu. Marekani kuna msanii mkubwa alisema anataka kulipua ikulu na walimuangalia tu. Hata hao walio mshitaki Lissu wanajua hakuna kesi hapo ila wanatumia mianya ya kisheria kumuweka kizuizini.
Sasa mkuu Lissu si aende Marekani ndiyo akaseme maneno hayo ya kulipua Ikulu.

Hiyo Marekani mnaitumia visivyo. Mnaamini kuna haki sana lakini huko ndiyo kuna abuse of human rights za kutisha.

Hebu niambie kwa nini R Kelly, Bill Cosby, P Diddy wamepata musukosuko lakini watuhumiwa wa Jefrey Epstein kwenye child sexual scandal kama Prince Andrew, Bill Clinton etc wala FBI hawajawatafuta? Instead wamemuua Jeffrey Epstein na shahidi muhimu Virginia Giuffrey wao wanasingizia kuwa wame commit suicide.
 
Harafu unakutana na TEC wanasema atolewe , upuuzi matupu
Katibu Mkuu wa TEC ni cousin brother wa Lissu. Hata baadhi ya mikutano ya CHADEMA kama mitatu ya viongozi wakuu imewahi kufanyika kwenye ofisi za TEC.

Sema TEC inatumika vibaya na Fr Charles Kitima. Tumuombee apone majeraha. Ila inabidi ajitafakari
 
Uasi maane yake ni nini ?
Kumbuka hupiga kura ni uasi.
Kushawishi watu waipigie ACT ni uasi
Kufanya campaign ni uasi

Je uasi ndio uhaini?
Acheni kumsumbua mtu wa watu huko gerezani.
(1) Kanuni ya Jinai (Penal Code): Vifungu namba 38 (kuchochea fujo- sedition), 40 (kuchochea machafuko-inciting unrest), au 41 (kuashiria kusudi la kuvunja utulivu wa umma-conspiracies to breach public peace) vinaweza kutumika kuwashitaki wanaotangaza mambo hayo.
 
(1) Kanuni ya Jinai (Penal Code): Vifungu namba 38 (kuchochea fujo- sedition), 40 (kuchochea machafuko-inciting unrest), au 41 (kuashiria kusudi la kuvunja utulivu wa umma-conspiracies to breach public peace) vinaweza kutumika kuwashitaki wanaotangaza mambo hayo.
Huyu mleta Mada kaomba connection za M23. Je ni ya kutafuta kazi au fujo?
Ni vigumu kujua nia yake kwa hiyo, Hivyo vifungu vitakaa Sana makabatini.
 
Ndio atachomola lakini uzur wake sio kesho wala keshokutwa mpk kama mwaka mmoja akitoka akafanye checkup ubeljeje
Hutaamini kitakachotokea subiri uone km atakaa huo mwaka 😚
 
Back
Top Bottom