VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

Unamlaumu bure maana yeye alisema waajiliwe wakimaliza. Sasa CDF amebadili upepo, nani wa kulaumiwa?

Wewe unaona ni sawa hao vijana kufanyishwa kazi ambayo ilipaswa serikali yenyewe itenge bajeti ya man power kwa kigezo cha wao eti wafanye then wataajiriwa? Ni sahihi kweli
 
Nadhani katika day to day activites/duties of wanajeshi. Linapokuja suala kuwa kuna mtanziko fulani, AJM na CDF .......anyway sijui
Hapo sasa CIC Vs CDF. Naona vijana wakaamua wajiongeze maana amri ya CIC iliwekwa kapuni kiaina.

Sema naye Magufuli alikuwa anakurupugaka mno. Yeye jambo likimfurahisha ni kutoa tu kauli kiholela.
 
We unaona ni sawa hao vijana kufanyishwa kazi ambayo ilipaswa serikali yenyewe itenge bajeti ya man power KWA kigezo Cha wao eti wafanye then wataajiriwa??ni sahihi kweli
contract, sheria ya mkataba, Law of contract act! . Umeingia mkataba.... sanctity of contract!..... walijifunga, wapate ajira. Hivyo ni haki yao kuajiliwa.
 
Hapo sasa CIC Vs CDF. Naona vijana wakaamua wajiongeze maana amri ya CIC iliwekwa kapuni kiaina.

Sema naye Magufuli alikuwa anakurupugaka mno. Yeye jambo likimfurahisha ni kutoa tu kauli kiholela.
Ndiyo tatizo la madikiteita.. Roadside Decrees! Akifurahi anakuteua akiwa ndani ya gari akila mahindi ya kuchoma
 
We unaona ni sawa hao vijana kufanyishwa kazi ambayo ilipaswa serikali yenyewe itenge bajeti ya man power KWA kigezo Cha wao eti wafanye then wataajiriwa??ni sahihi kweli
Jkt haitoi ajira mzee
Tupunguze lawama..
Sema wanasiasa ndiyo wa kulaumiwa
Kuingilia mambo ya jeshi

Ova
 
contract, sheria ya mkataba, Law of contract act! . Umeingia mkataba.... sanctity of contract!..... walijifunga, wapate ajira. Hivyo ni haki yao kuajiliwa.

Hujanielewa,I am neither challenging the law of contract,nor saying that they should not be employed,

My point is,before hata hawajaingia kwenye hayo makubaliano ilikuwa sahihi kuwaweka kwenye mtego huo kuwa mfanye kazi kwanza ya kujenga ikulu kisha ndipo niwape ajira?ajira jeshini huwa zinatolewa KWA muktadha huo?,I just want to know
 
Hii ni ishara mojawapo kuwa shujaa wa Chato alivuruga kila idara, sekta na taasisi kwa kauli zilizotoka kwa kuropokwa bila research!!
Mungu fundi sana... yule shujaa mshamba angetufikisha pabaya zaidi
 
Unasema kweli au uko one sided? Amiri Jeshi Mkuu na CDF nani ana kauli ya mwisho kama kuna sintofahamu yoyo
Rais hutoa kauli baada ya kushauriana na cdf. Vinginevyo jeshi ni taasisi independent na haifungamani na siasa au matamko ya kisiasa.
Pia strategically jeshi kupitia CDF linawezs kukinzana na kauli ya Rais kwa manufaa ya kitaifa.
 
Najua kilichowaumiza ni wizi mkubwa kwenye miradi enzi ya mfalme!

Hao walitumika kama vibarua huku watu nyuma ya pazia wakitia pesa kibindoni..

Mwisho wamekuja kuwatosa! Pole sana kwao !

Lakini najiuliza jeshi pia nitalioneaje huruma mara walikua sehemu ya kubariki udhalimu ule wa October mwaka jana?

Je hawa waliorudi mtaani wataenda kufanya nini ilhali wana mafunzo ya silaha! Sio chanzo cha kuzaa uasi sasa kama kisasi?

Nafikiri jeshi letu sasa lijifunze kutofungamana na kiongozi au chama bali liwe la wananchi kweli kweli...

Wanaweza kujifunza jinsi yule mkuu wa majeshi USA alipogoma kumwaga wanajeshi barabarani kwa sababu tu Rais Donald Trump kaamuru iwe hivyo
 
Hujanielewa,I am neither challenging the law of contract,nor saying that they should not be employed,

My point is,before hata hawajaingia kwenye hayo makubaliano ilikuwa sahihi kuwaweka kwenye mtego huo kuwa mfanye kazi kwanza ya kujenga ikulu kisha ndipo niwape ajira?ajira jeshini huwa zinatolewa KWA muktadha huo?,I just want to know
Utaratibu wa saivi ni lazima upitie JKT kabla ya kupata ajira jeshi lolote Tz, na kupita JKT vilevile sio guarantee ya hiyo ajira, JKT ni sehemu ya kujitolea na kufunzwa.
 
contract, sheria ya mkataba, Law of contract act! . Umeingia mkataba.... sanctity of contract!..... walijifunga, wapate ajira. Hivyo ni haki yao kuajiliwa.

Ni kweli lakini njia ya kudai haki inavumilika katika taratibu na uendeshaji wa Jeshi? Jibu ni hapana. Ukicheka na hawa itafika siku na wale wa Sangasanga watasema ngoja tuige ule utaratibu wa JKT. Hivyo vifaru na ndege vita vya kuwazima muda utakuwa rafiki wa kuvi mobilize.
 
Ok kama unaongelea njia za kudai hazikuwa sahihi, hapo sawa! support 100%
 
Ndio kwa mujibu wa viapo vya askari.

Wanajeshi wanaapa kwa CDF.
Jibu lako haujaliweka vizuri ndio maana watu wanashindwa kukuelewa.

Askarijeshi yoyote ambaye sio 0fficer (hana nyota) au cheo chake kinakaa chini ya bega kiapo chake anakula mbele ya Mkuu wa Majeshi (CDF) au atatuma mwakilishi kama yeye ana majukumu mengine sio lazima awepo.

Askarijeshi yoyote ambaye ni Officer (cheo chake kinaanzia nyota kwenda juu) au cheo chake kinakaa juu begani kiapo chake anakula mbele ya Amiri Jeshi Mkuu ambaye ndiyo Rais wa JMT.

Kama una swali uliza, na kama una nyongeza ongeza.
 
Back
Top Bottom