VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

VIDEO: Tarehe 08 Desemba 2020 Hayati Rais Magufuli akitoa amri kwa CDF kuwaajiri vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino

Mfano wangeajiriwa wangejijengea akilini mwao kumbe tukidai kitu kwa nguvu tutasikilizwa, kipindi hicho kumbuka wamevaa kombati. Askari walioajiriwa baada ya kuandamana ni hatari kwa usalama wa nchi saf CDF Mabeyo.
Jeshi ni utii

Jeshi ni heshima...
 
Huyo Magufuli aliwasiliana na jeshi au katoa amri tu?

Alitoa fungu la pesa la kuajiri watu su katoa amri tu?
 
Jeshi ni utii

Jeshi ni heshima

Jeshi hakuna kuhoji kabla ujafanya ulichoelekezwa

Jeshi halina siasa chama wala dini

Ni utovu wa nidhamu mkubwa sana wanajeshi kuandamana

Maandamano ni ya wanasiasa NGO's za kiraia makundi mengine but sio majeshi.

Alichokifanya Mabeyo namuunga mkono 100% lazima jeshi Liwe tiifu kwani ndio sifa namba moja ya kuwa mwanajeshi.
Haya waambie CCM sababu ndo wanatuharibia jeshi letu tukuka na Taasisi nyingine nyeti kwa kujaza humo makada wao wakitumua mifumo dhaifu ya kikatiba na kitaasisi.
 
Kama maelezo ya kuwa vijana waliofukuzwa JKT eti kwa kudai ajira zao walizo ahidiwa na Amiri jeshi walikuwa wanastahili posho pia lakini hawakuwa wanapewa maana zimeliwa na wachache basi wametendewa uonevu mkubwa.

Madhara ya uonevu huo ni kuwajengea roho za ukatili ambao wanaweza kuja kuutekeleza kwetu mtaani.

Kwanini wahusika waliokula pesa hizo wasiwajibishwe na ahadi ya Rais isitekelezwe? Au rais aliyepita alikuwa mropokaji tuu ili aweze kupigiwa makofi hata kwa vitu anavyojua havitekelezeki?

Hili bomu litafutiwe ufumbuzi haraka

Screenshot_20210421-043023_Twitter.jpg
 
Kama maelezo ya kuwa vijana waliofukuzwa JKT eti kwa kudai ajira zao walizo ahidiwa na Amiri jeshi walikuwa wanastahili posho pia lakini hawakuwa wanapewa maana zimeliwa na wachache basi wametendewa uonevu mkubwa....
Ina maana siku zote mpaka leo huamini mpaka useme kama ni kweli?
 
Bunge lishaonekana ni dhaifu na hoja hazina afya.

Usifanye jeshi letu nalo liwe kama bunge

Mtakapo ingiza siasa jeshini ndo matatizo yanapoanzia.

Watz wanakuwa wasemaji wa kila kitu. Vitu vingine iwe mnapewa tuu taarifa bila kujadili.

Kwa hali yoyote ile CDF akikubali kusikiliza ngoma za mitandaoni na bungeni na akawarudisha ni dhahiri inatakiwa ajipige risasi ya kichwa.
 
Jeshi ni utii

Jeshi ni heshima

Jeshi hakuna kuhoji kabla ujafanya ulichoelekezwa

Jeshi halina siasa chama wala dini

Ni utovu wa nidhamu mkubwa sana wanajeshi kuandamana

Maandamano ni ya wanasiasa NGO's za kiraia makundi mengine but sio majeshi.

Alichokifanya Mabeyo namuunga mkono 100% lazima jeshi Liwe tiifu kwani ndio sifa namba moja ya kuwa mwanajeshi.
Wale Vijana Walifanywa Watumwa wa Mweko kwa Kimvuli cha Jeshi
 
Niwakumbushe waliojenga MIRERANI walajiriwa mwaka mmoja + baada ya kuahidiwa hao hata miezi sita hawakumaliza

Baada ya wale vijana kuahidiwa wakidhani imeisha wanaondoka na kuachana ana adha.

1. Walirudi vikosini na huko ilikua kama neema kila CO alianzisha mradi wa ujenzi na hapo jeshi likatoa ramani za zahanati na amala za mfano mafundi wakiwa ni walewale na hawakugoma

2. Walienda kujenga ukuta chamwino sehemu kubwa ikiwa ni wale wale wengi wakidhani kutokwenda kunawwza kubatilisha ahadi

3. Walijenga ukonga hizi nyumba za magereza tena kuweka kumbukumbu sawa waliojenga ukonga wengi walitolewa katika ukuta wa chamwino na hawakugoma.

3. Wanaenda kozi ya ajira Msata wanakutana na ujenzi mwingine kabla hawajaanza kozi wanaliunga na hawakugoma.

NARUDIA, Sikuwahi kusikia wanegoma

Baada ya kuchukuliwa MSATA likaja picha la vipimo vya afya na kundi kubwa likatolewa Kwa homa ya ini na Tb na hapakua na mgomo

Hawa ni kina nani...

Kwanza hawana ushirikiano walijiona wao bora wakasahau wapo karibu 3000 ambao ni intake moja ila wamesambazwa katika miradi na wote wanatakiwa kuajiriwa kwa ahadi ile (kumbuka bwawa la nyerere wapo, chato wapo, shule mfano ya bunge wapo)

Kozi mbovu na hili wakufunzi wajitathimini hapakua na askari ila mafundi ujenzi waliopitishwa Jkt kama kichaka

Watu wanagoma vikosini na tifu linapigwa na CO analimaliza ni kawaida tunamalizana kijeshi ila sio kushinikiza kwenda ikulu hiyo ni hatua ya juu sanaaa... Chamwino mpaka ufike resort umevuka sehemu nyingi sana na kote walizuiwa hawakusikia...

Tulioshuhudia tulijua nini kinafuta na mapaka kunakucha hawakuamini nao walibaki wanaulizana ni kama ulipita upepo ukavuma upande wao.

Mwisho kusamehe ni kubariki uasi ndani ya jeshi na HAIRUHUSIWI

Nilikuwepo, niliona na baadhi yao nilionya tangu wanaanzisha vuguvugu tena usiku ule kwa kuwaambia wakafolen tuongee na bado waligoma.

MUNGU nae hua na mipango yake yametokea na sio wa kwanza kurudi nyumbani walirudi op jk 2000+, walirudi op Magufuli 2000+ ujenzi ni sehemu ya jeshi kama ilivyo kuchota maji na kukata kuni.

Sio mimi nimesema ila mimi nimeyabadili kuwa maandishi

Wasalaaam
 
Jeshi ni utii

Jeshi ni heshima....
Rais alisema wakimaliza kujenga jengo waajiriwe kwani wamekwishamaliza kujenga? au bado jengo linaendelea liko hatua ya finishing. Kwa nini kiherehere kuandamana kabla ya kazi kuisha, kuandamana ni kuingiza siasa jeshini si mahala pake ni uasi fullstop!

Hao vijana hawana utii wa kweli hata kama wangeajiriwa hawana sifa ya kuwa walinzi wa nchi, taifa lingejuta wameaibisha jeshi, Bravo CDF umeonyesha uzalendo na mfano mwema wa usimamizi wa dhana ya utiifu kwenye jeshi letu.
 
Ina maana siku zote mpaka leo huamini mpaka useme kama ni kweli?
Tusaidie huo ushahidi kuwa fedha zao zimeliwa na tutajie wahusika ili hatua zichukuliwe haraka. Tunasema kama ni kweli maana taarifa ya uchunguzi haijawekwa hadharani
 
Hivi hii nchi bado inaendeshwa na nani? Rais haoni haya au ndo cdf anapandisha mabega siku hizi...Enzi zile wangeambiwa hata wakadeki vyoo stend ya mbezi wangeenda! Mama samia aseme neno.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Tusaidie huo ushahidi kuwa fedha zao zimeliwa na tutajie wahusika ili hatua zichukuliwe haraka. Tunasema kama ni kweli maana taarifa ya uchunguzi haijawekwa hadharani
akikujib nitag. watu wanadhani jeshi linaendeshwa kisiasa.
 
Rais alisema wakimaliza kujenga jengo waajiriwe kwani wamekwishamaliza kujenga? au bado jengo linaendelea liko hatua ya finishing. Kwa nini kiherehere kuandamana kabla ya kazi kuisha, kuandamana ni kuingiza siasa jeshini si mahala pake ni uasi fullstop...
simple and clear. cha kuongezea haku room ya maandamano jeshini. no room for wasaliti
 
Mkaruka

kwahiyo amri ya cdf, anayeteuliwa na rais ni kubwa ya kuliko ya rais mteuaji?
Sivyo. Kijeshi amri ya afande mkubwa zaidi ndiyo inabidi kutiiwa. Kama Kanali akikuagiza kufanya kitu inabidi ukifanye. Wakati ukikifanya akaja Generali akakuambia vinginevyo, inabidi ugeuze na kutekeleza maelekezo ya sasa. Rais ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Hivyo, agizo lake ndilo linabidi kufuatwa.
 
Back
Top Bottom