Niwakumbushe waliojenga MIRERANI walajiriwa mwaka mmoja + baada ya kuahidiwa hao hata miezi sita hawakumaliza
Baada ya wale vijana kuahidiwa wakidhani imeisha wanaondoka na kuachana ana adha.
1. Walirudi vikosini na huko ilikua kama neema kila CO alianzisha mradi wa ujenzi na hapo jeshi likatoa ramani za zahanati na amala za mfano mafundi wakiwa ni walewale na hawakugoma
2. Walienda kujenga ukuta chamwino sehemu kubwa ikiwa ni wale wale wengi wakidhani kutokwenda kunawwza kubatilisha ahadi
3. Walijenga ukonga hizi nyumba za magereza tena kuweka kumbukumbu sawa waliojenga ukonga wengi walitolewa katika ukuta wa chamwino na hawakugoma.
3. Wanaenda kozi ya ajira Msata wanakutana na ujenzi mwingine kabla hawajaanza kozi wanaliunga na hawakugoma.
NARUDIA, Sikuwahi kusikia wanegoma
Baada ya kuchukuliwa MSATA likaja picha la vipimo vya afya na kundi kubwa likatolewa Kwa homa ya ini na Tb na hapakua na mgomo
Hawa ni kina nani...
Kwanza hawana ushirikiano walijiona wao bora wakasahau wapo karibu 3000 ambao ni intake moja ila wamesambazwa katika miradi na wote wanatakiwa kuajiriwa kwa ahadi ile (kumbuka bwawa la nyerere wapo, chato wapo, shule mfano ya bunge wapo)
Kozi mbovu na hili wakufunzi wajitathimini hapakua na askari ila mafundi ujenzi waliopitishwa Jkt kama kichaka
Watu wanagoma vikosini na tifu linapigwa na CO analimaliza ni kawaida tunamalizana kijeshi ila sio kushinikiza kwenda ikulu hiyo ni hatua ya juu sanaaa... Chamwino mpaka ufike resort umevuka sehemu nyingi sana na kote walizuiwa hawakusikia...
Tulioshuhudia tulijua nini kinafuta na mapaka kunakucha hawakuamini nao walibaki wanaulizana ni kama ulipita upepo ukavuma upande wao.
Mwisho kusamehe ni kubariki uasi ndani ya jeshi na HAIRUHUSIWI
Nilikuwepo, niliona na baadhi yao nilionya tangu wanaanzisha vuguvugu tena usiku ule kwa kuwaambia wakafolen tuongee na bado waligoma.
MUNGU nae hua na mipango yake yametokea na sio wa kwanza kurudi nyumbani walirudi op jk 2000+, walirudi op Magufuli 2000+ ujenzi ni sehemu ya jeshi kama ilivyo kuchota maji na kukata kuni.
Sio mimi nimesema ila mimi nimeyabadili kuwa maandishi
Wasalaaam