Video: Timu ya Yanga tayari imewasili uwanjani Mkapa, ila ndani hakuna mashabiki wametolewa

Video: Timu ya Yanga tayari imewasili uwanjani Mkapa, ila ndani hakuna mashabiki wametolewa

Jamani si mnakumbuka maneno ya haji manara aliwahi kusema kuwa pale katika timu yoteYA yanga kuanzia uongozi wanachama na mashabiki kuwa katika wote hao wenye akili ni watu wawili tu. hivyo kwa wao kuamua kuingiza timu uwanjani wakati mchezo huo ukiwa umeahirishwa hiyo yote ni kujithibitisha kuwa ni kweli kwa kile alichowahi kukisema haji kuwa ndani ya yanga wenye akili ni wawili tu.
 
Halafu na zile gharama walizotumia Yanga kuandaa timu kule Avic Town kwa wiki nzima atalipa nani? Na vipi kuhusu wale mashabiki waliotoka Mikoani kuja kuishangilia timu yao, watafidiwa na nani gharama zao?
Na vipi kuhusu wale wafanyabiashara waliondaa bidhaa zao mbalimbali kwa ajili ya kuuza kwenye hiyo mechi, watafidiwa na nani?
Je, ni sahihi kwa timu kususia mechi kwa sababu ya kuzuiliwa na meneja wa uwanja kufanya mazoezi masaa 24 kabla ya mchezo, halafu Bodi ya ligi na yenyewe inaungana kirahisi tu na hiyo timu kuahirisha huo mchezo?

Je, na timu nyingine zikifanya upuuzi kama huu zitalindwa na hiyo Bodi ya ligi kama walivyolindwa simba?
Ndio ukichaa wa ligi yetu huu ila na sisi mashabiki tukiendelea kuwaunga mkono na hui ujinga wataendelea kutufanya majinga siku zote.
 
Sisi timu tunaipeleka Taifa, kisa cha kuahirisha mechi ni ujinga wa watu wanaoamini nguvu za giza. Jana hakuna wachezaji walioenda kufanya mazoezi usiku. Kwenye basi mlijaza vibabu kibao, kondoo na mbuzi. Mlitaka mkapike supu mule ndani?

Acheni uchawi wenu, kinachowafanya leo msilete timu, ni hiko makafara yenu hayakufanyika hovyo kabisa. Na mna bahati nyie, leo mngeokota mipira wavuni, mpaka mngekimbia uwanjani. Zile 5 ingekuwa mara mbili simbilisi nyie, mmetukosesha uhondo.
Nimemsikia Manara anasema kikosi kilichopelekwa jana usiku ni B halafu na vizee vifupi tupu. Ujinga tupu yaani!
 
Wameruhusiwa vipi kupita na msafara wao kwenye geti wakati bodi na TFF wameshatoa taarifa kuwa mechi hakuna. Halafu unamsikia chura mmoja anasema hawahusiki na kuwazuia Simba kuingia uwanjani siku ya jana.
Hii nchi uhuru
 
Mbona hii mechi haikufutwa round ya kwanza au nyani ndio nyani haoni lake kund..........le.
View attachment 3263814
Au TFF hawakupata ripoti za kilicho fanyika kabla ya mechi?
Hapana.. hapa ni kwamba nyani ana wanasheria wabovu ambao hajui kutafsiri kanuni... au kwa maneno mengine nyani hakujua haki zake na wakaa kimya.
 
Hapana.. hapa ni kwamba nyani ana wanasheria wabovu ambao hajui kutafsiri kanuni... au kwa maneno mengine nyani hakujua haki zake na wakaa kimya.
Nope ujue hata CAF ukifanyiwa vitimbi vya kukataliwa kucheza si kwamba ukimbilie kususa. Nchi za kiarabu zinafigisu nyingi sana,hizi sijui kuzuia timu zisitumie viwanja siku moja kabla ya mechi ni kawaida, ila still timu hazisusi mechi inapigwa .Ila repoti ya mechi CAF wataipitia then maamuzi yatafanyika kupitia repoti.

Sasa huku TFF tulitegemea baada ya ile mechi ya KOLO FC kubondwa moja bila angetoa adhabu kwa walio mzuia Yanga,ila hawa kufanya hivyo,tulijua TFF wana culture kama za CAF kumbe tofauti.
 
Nimemsikia Manara anasema kikosi kilichopelekwa jana usiku ni B halafu na vizee vifupi tupu. Ujinga tupu yaani!
Ni aibu tupu Kaka, jana kuna mtu alikuwa pale. Kashuhudia kwa macho yake uhuni wanaoufanya hawa. Bodi nayo haijielewi, na bahati mbaya wengi ni simba hiyo bodi.

Mpira wa miguu kuja kukua zaidi ya hapa ni ndoto. Badala tuhangaike na watoto wa umri mdogo kucheza mpira. Tunakuja kujadili timu imegoma kuingia uwanjani, kisa usiku wake walitaka kuingiza vibabu vyao uwanjani.
 
Naona sofa score game inaendelea ipo dakika ya sita
IMG_20250308_192023.jpg
 
Sisi timu tunaipeleka Taifa, kisa cha kuahirisha mechi ni ujinga wa watu wanaoamini nguvu za giza. Jana hakuna wachezaji walioenda kufanya mazoezi usiku. Kwenye basi mlijaza vibabu kibao, kondoo na mbuzi. Mlitaka mkapike supu mule ndani?

Acheni uchawi wenu, kinachowafanya leo msilete timu, ni hiko makafara yenu hayakufanyika hovyo kabisa. Na mna bahati nyie, leo mngeokota mipira wavuni, mpaka mngekimbia uwanjani. Zile 5 ingekuwa mara mbili simbilisi nyie, mmetukosesha uhondo.
Hata kama Yanga wamefanya kosa kuzuia mpinzani kufanya mazoezi bado hii sio sababu inayoweza kufanya mechi kuhairishwa badala yake Kuna adhabu kama fain zimewekwa.

Ingekuwa nchi inayofata sheria Yani hakuna influence ya serikali kwenye masmuzi ya bodi Wala timu, Simba wasingejaribu kususia mechi Wala TFF kuhahirisha. Sema wanajiamini kwakuwa serikali itaingilia kuwatetea na sheia zao za kutumia busara badala ya kufata kanuni.

Yanga wakikaza kufata kanuni lazima TFF na simba watawajibishwa lakini Sasa kinachokera hakuna mwenye ubavu wa kufanya hivyo ikiwa serikali itaingilia, rejea ishu ya feitoto ambapo kauli ya rais ikafanya yanga walegeze kamba na ule msimu wa 2021.
 
Najaribu tu kuwaza, yaani simba wamefanyiwa harassment, mwisho wa siku wanacheza mechi hivo hivo na mwisho wa siku wanaishia kufungwa kutokana na kukosa utimamu wa kimwili na mambo mengine yanayotokana na hiyo harassment.... Mwisho wa siku bodi ya ligi wanaishia kuwapa adhabu yanga ya shilingi laki tano kwa kosa la kum harass mgeni wake na kutomruhusu ku train.... yanga anatoa laki tano huku amekusanya zake points tatu.... hapo jiulize hasara ni ya nani halafu jibu baki nalo mwenyewe...
 
Benchi la ufundi Oyeeeee. Ila mnatia aibu sana, nyie hamjiamini ndiyo tatizo. Mkiisikia Yanga, mlivyoona video wachezaji wa Yanga wanavyojifua kimazoezi. Mkasema piga uwa hatuchezi nao Jumamosi. Mtani mmeanza kutukimbia tena 😂😂😂😂😂
mngekuwa mnajiamini mngemuacha mnyama atibue nyasi na kafara zenu😆😆
 
Back
Top Bottom