Uchaguzi 2020 VIDEO: Wachambuzi wa siasa Kenya washangazwa na muundo wa uchaguzi wa Tanzania, wasema walitoka huko kitambo sana

Wakiambiwa wenye akili timamu watoke mbele nawe utatoka,mada inasema nini na wewe unajadili nini,jamaa wameongea ukweli mtupu sasa wewe mlumumba unavuruga mada
Huna akili!

Kenya haina cha kujivunia mpaka inakosoa ya tz!

Wangekuwa na akili wangeanza kukosoa ya ukabila nchini mwao kwanza
 
Watanzania wa wapi unawasemea? Pesa ipi wapinzani wataenda kuitafuna wakati tayari trilion- 1.5 imepigwa na CCM na zingine wanaendelea kukomba sufuria
CCM ni wezi wametafuna hiyo 1.5 tr, je CHADEMA bungeni wamekuwa wakitafuta nini? Tusizubaishane. Hawajatimiza wajibu wao wa kusemea mfumo mzuri wa nchi badala yake miaka 5 yote wanahangaika na kelele za umaarufu bungeni bila kusema mambo muhimu ya mfumo wa utawala. Umefika mwaka wa uchaguzi ndo wanasema watasusia uchaguzi, hadi wapate tume huru, mbona hawakususia bunge ili serikali ilete muswada wa kubadili katiba. Kwani tume ni kelele?
 
Uzalendo ni kuwabambikia kesi kesi kuwapiga risasi wapinzani?
Kamilisha sentensi yako kwa kuongeza maneno haya kwanza ili tuelewane vizuri."Wapinzani waliopo kwaajili ya kupinga kila kitu,kupotosha,na kutoangalia masilahi mapana ya watz"
 
Bungeccm spikaccm hakuna haki kwa wabunge wa upinzani Bungeni
 
Kenya hawabambiki kesi kesi kwani mahakama ipo huru ni vigumu kupenyeza kesi za kubambikiwa kama Tanzania ambapo CCM humiliki mahakamaccm
Huwezi kuelewa,unaendeshwa na akili za kishabiki,kiasi kwamba unahisi Kenya Ni sehemu salama Sana.Jaribu kukumbuka hata ya 2007 basi.
 
Ni Chris Msando. Kamishna Chebukati yeye alitorokea Dubai alikokwenda kuchapa karatasi za kura akaenda US. Halafu kimtu kinakuja kusifu Kenya hapa TZ!
 
Umenikumbusha mkuu!

Kiufupi wajumbe wa tume ya uchaguzu ya Kenya ikifika kipindi cha uchaguzi maisha yao huwa yanafika mwisho, na pengine huwa wanaandika usia kabisa
 
Katiba inampa haki Rais kuteuwa tume.
Mwamko wa katiba mpya bado ni mdogo sana kwa hao viongozi wa vyama wa mpaka wananchi.acha kwanza miaka isogesogee.
Shida nyingine ni pale hata anayefanikiwa kushida, anakwambia KATIBA mpya siyo kipaumbele chake, kwa sababu tu anaona hii iliyopo inampa umungu mtu (inampa madaraka makubwa). Kiukweli JK alikua ameamua kutuachia KATIBA mpya, lakini watu wa chama chake walipoona maisha ya chama yapo hatarini, walichotufanyia unakijua. Tuombe aje atokee mwenye moyo wa kutupatia katiba mpya.
 
Bungeccm spikaccm hakuna haki kwa wabunge wa upinzani Bungeni
Porojo Kama hizi hazisaidii chochote,falsafa ya CHADEMA unaamini zaidi katika swala la kuongea kuliko kutenda,ndio maana wabunde wengi wa CDM husifiwa kwa kuongea jwao na sio kutenda.
 
Bungeccm spikaccm hakuna haki kwa wabunge wa upinzani Bungeni
Kama ni hivyo waachane na siasa kwani wao walizaliwa kuwa wanasiasa? Kazi isiyo na manufaa kwa nini wanaendelea tu hadi kufukuza wengine wanaowafuta CHADEMA! Mahindi yangu yalipokauka kwa jua, siku hizi nafuga kuku na silalamikii wabunge. Kwa nini wao wanatulalamikia utadhani waliumbwa kwa kazi hiyo? Ni uzembe!
 
Umenikumbusha mkuu!

Kiufupi wajumbe wa tume ya uchaguzu ya Kenya ikifika kipindi cha uchaguzi maisha yao huwa yanafika mwisho, na pengine huwa wanaandika usia kabisa
Mashekh wa Mombasa huwa wanakufa ovyo,afu bado Kuna mtu anakwambia Kenya Ni sehemu nzuri.
 
Hawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.

Vp nasikia washaanza kukinukisha huko, Kenyatta na William Rutto hawaelewani tena.
Bado 2 years kufikia uchaguzi mkuu huko Kenya, ila ogomvi ushaanza tayari.
Inabidi wajadili yakwao kwanza.
 
Kamilisha sentensi yako kwa kuongeza maneno haya kwanza ili tuelewane vizuri."Wapinzani waliopo kwaajili ya kupinga kila kitu,kupotosha,na kutoangalia masilahi mapana ya watz"
Kazi ya upinzani ni nini? Kazi yake siyo kuifagilia CCM wakifanya ufisadi mambo ya hovyo yasiyo na tija kwa Taifa, kazi ya upinzani ni kupinga mabaya yote ya CCM na katika hii miaka mitano hawajafanya la maana ndiyo maana wanapingwa kwa kila kitu bila kuchuja, wanajidai kuleta maendeleo kununua Ndege na miradi kibao kote kuna ufisadi 10% za wajanja wachache, kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani ndiko kutoangalia masilahi mapana ya watanzania?
 
CCM hawana cha kuigwa hata kimoja zaidi ya kuendelea kulalamikiwa zaidi juu ya mfumo wao mbovu wa uchaguzi
 
Utawala huu ni utawala penda kesi kesi ni utawala umetumia kesi kesi kama rungu la kuwakomoa watu waliojitolea kuwakosoa live, siku zote Serikali yenye uovu mwingi hutumia mahakama na Polisi kunyamazisha watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…