Uchaguzi 2020 VIDEO: Wachambuzi wa siasa Kenya washangazwa na muundo wa uchaguzi wa Tanzania, wasema walitoka huko kitambo sana

Kenya siyo nchi ya kupigia mfano!
Nikiona chadema wanavyojidharau kwa kujilinganisha na Kenya, naonaga kabisa hawa jamaa wakipewa nchi, hao Wakenya wanaweza kuteuliwa hadi wakuu wa mikoa wakiongoza kutoka Nairobi.

Hivi Kenya wana nini cha kujilinganisha nao?
 
Kenya hawana la kuifundisha Tanzania. Waendelee tu na mambo yao kila uchaguzi vifo, fujo, na kunyakua madalaka.

Uchaguzi uliopita ni fundisho tosha kwama sio uchaguzi ulibakwa tu.
 
INAWEZEKANA katiba yetu ikawa na mapungufu kama ilivyo yakwao pia

SWALI LA MSINGI

"'kwa nini uchungulie chumbani kwa jirani yako na huku ukijua muda huo wanaweza kuwa faragha?''

Huo ndio unafiki uliopo kwa hao jamaa,

Umewahi ona vyombo vya Tanzania (wanahabari) au viongozi wakichambua katiba ya Kenya wakati wa uchaguzi? au wakati wowote ule?
 
Unaweza kutaja hayo uliyosema kwa mifano?
Ndio
Ameua Akina saa nane
Amefilisi wafanyabiashara
Amekula hela ya rambirambi za wahanga wa tetemeko kule bukoba
Kila mkoa kuna waislamu ambao hata bunduki hawajui wapo jela kwa tuhuma za ugaidi ni watuhumiwa wengi kuliko Afghanistan
Mkaguzi mkuu wa mahesabu alisema kuna zaidi ya dollars billion moja imepotelea ikulu
Huyu mtu katili Sana Ndio maana ulinzi wake ni mkubwa kuliko rais yeyote
 
Uko sawa kabisa, Kenya tatizo lao kubwa linajulikana ni ukabila. Vipi sasa kwenye hili tatizo waliloongelea linalotukabili sisi "TUME YA UCHAGUZI" hapo unasemaje?
Tume sio tatizomtambuka linaweza kutatuliwa na mambo yakawa poa.
Siasa za ukabila wa Kenya unaumalizaje bwashee?
 
Nilifikiri una la maana kumbe ujinga tu!

Ndio nyie mnasema hakuna uhuru wa kutoa maoni lakini mnakuja kuhara humu na kusababisha Melo anapata kazi ya kuwatetea.
 
Bado hapa kuna mtu atakuja na hoja mfu kukupinga haya. Hili ndilo tatizo la watanzania walio wengi, wameyabeba yale wanayoambiwa na wanaokula keki badala ya kufikiri wao wenyewe na kujua ukweli kama huu.
 
Pale Kenya sasa hivi ni kama hamna mkubwa! Kila mtu ni kambare! Wamejaa ukabila, hayo ndio waliyoendelea hakuna kingine.

Fikiria uchaguzi bado miaka 2 lakini ofisi ya rais Kenyata ina mgogoro wa kugombea madaraka ya 2022
Demokrasia hiyo
 
Ingekuwa hapa kwetu watu wangesha potezwa
 
Siasa za Kenya ni za ubaguzi wa kikabila.

Kenya wapambane kwanza waondoe hili kabla ya wao kukosoa wengine.
Hata hapa ukabila tayari umejengwa na awamu ya tano.

Reli mbili zinaenda sehemu moja, je tunamahitaji hayo?
Huo siyo ukabila?
Makabila mengine tunafikiriaje?
 
Kwa hiyo yetu tusiifanyie marekebisho hata baada ya kujua mapungufu yaliyopo kwa sababu wao hawajafaidika na yao? Mkuu, hii tume haifai. Nina uhakika hata wewe unakubaliana na hili.
 
Siasa za Kenya kila uchaguzi wanaunda vyama vipya kinachoshinda kinachukua tenda zote na kujimilikisha nchi hadi uchaguzi mwingine. Sasa hivi Mt Kenya group kwa wakikuyu hawataki kusikia rais wa 2022 anatoka kabila lingine isipokuwa mkikuyu hakuna Ruto wala Raila wala Mudavadi wala Kalonzo pengine wakampa Martha Karua au Peter
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…