Uchaguzi 2020 VIDEO: Wachambuzi wa siasa Kenya washangazwa na muundo wa uchaguzi wa Tanzania, wasema walitoka huko kitambo sana

Siasa za Kenya ni za ubaguzi wa kikabila.

Kenya wapambane kwanza waondoe hili kabla ya wao kukosoa wengine.
KWahiyo ukiwa dhaifu ukaambiwa udhaifu wako, badala ya kurekebisha udhaifu wako una deal na aliyekuonesha udhaifu wako? Nadhani tungejadiri alicho kisema kama ni cha kweli au laa then tukirekebishe, huo ndio uungwana.
 
Pale Kenya sasa hivi ni kama hamna mkubwa! Kila mtu ni kambare! Wamejaa ukabila, hayo ndio waliyoendelea hakuna kingine.

Fikiria uchaguzi bado miaka 2 lakini ofisi ya rais Kenyata ina mgogoro wa kugombea madaraka ya 2022

Hoja yake ina mashiko au hapana?
 
Tume sio tatizomtambuka linaweza kutatuliwa na mambo yakawa poa.
Siasa za ukabila wa Kenya unaumalizaje bwashee?
Unafikiri tatizo kubwa kwenye tume yetu ya uchaguzi ni lipi hasa hadi uone kweli kuna haja ya kuifanyia marekebisho??
 
KWahiyo ukiwa dhaifu ukaambiwa udhaifu wako, badala ya kurekebisha udhaifu wako una deal na aliyekuonesha udhaifu wako? Nadhani tungejadiri alicho kisema kama ni cha kweli au laa then tukirekebishe, huo ndio uungwana.
Sawa lakini mimi pia nimeonyesha nawao pia wanachangamoto.
Tume huru itakuja tu kwa hapa Tanzania ni swala la muda tu.
ila kwa Kenya siasa za ukabila wanalo na linawatafuna sana.
 
W
Hawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.

Wakenya wasubili cha moto wao wenyewe makamu raisi na raisi hawaelewani sasa badala ya kuchambua ya kwao wao wanataka ya tanzani,
Hivi sasa wengine wameanza kampeni wakati uchaguzi ni 22 na wasipoangalia watauna tena kama kuku.
 
Hata hapa ukabila tayari umejengwa na awamu ya tano.

Reli mbili zinaenda sehemu moja, je tunamahitaji hayo?
Huo siyo ukabila?
Makabila mengine tunafikiriaje?
Kuwa na fikra pana bwaashee.
Hizo reli zimepaa mpaka Mwanza ama Chato ama zinapita kwenye mikoa tofauti?
 
Kawaulize wakenya wanachokipata saa hii kutokana na hiyo katiba nzuri
Katiba ya Kenya ninayo hapa! Na ninayo ya Tz na pia ya Zanzibar. Katiba ya Kenya ni nzuri sana ila inaongoza Wanadamu wenye roho mbaya kama ilivyo ya Tz. Nipatapo muda nitaandika uzi wa kuzilinganisha hasa katika masuala ya sheria na uchaguzi. Matatizo ya Kenya yaliyopo sasa yanatokana na uchu wa madaraka na wala Sio katiba japo wapo katika harakati za kuboresha katiba yao baada ya kuwa nayo kwa miaka 10. Mfano mdogo ni kuwa kulingana na Katiba ya Kenya, hakuna kosa lisilodhaminika. Kosa la mauaji linadhaminika. Iwe uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha au lingine lolote yote unapewa dhamana. Hii imesababisha Polisi kuwabambikia watu kesi
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kwa hiyo hayo ndio ganafanya hiyo katiba iwe nzuri?
 
Kwa hiyo yetu tusiifanyie marekebisho hata baada ya kujua mapungufu yaliyopo kwa sababu wao hawajafaidika na yao? Mkuu, hii tume haifai. Nina uhakika hata wewe unakubaliana na hili.


Hakuna nchi Dunia hii ambayo ina mfumo wa uchaguzi uliokamilika yaani usio na malalamiko kutoka upande mmoja ambao unaona mfumo uliopo hauwanufaishi, cha muhimu ni kutafuta balance na kupima gharama ya mabadilio kama ni kubwa au ndogo, na jibu la hilo swali huja tu wala halihitaji kulazimishwa, hivyo watanzania kwa wingi wao wakiona mfumo uliopo hawafai wataukataa, na itaonekana tu, ...
 
Kwa Africa hata kwenye nchi zenye tume huru bado malalamiko huwa ayakosekanagi.
 
Yaani wao wana mambo chungu nzima, yamewashinda ya kwao wanatafuta ya jirani !!!! Hawa inabidi tuwavalishe kanga moko
 
Ukitaka ujue akili za wachangia pata muda upitie comments zilizopo toka mwanzo, watu hawachangii khs mada wanatetea jambo lingine.
 
Wakenya wana matatizo mengi na Magufuli kawanyoosha ni vema wakachambua uchaguzi wa marekani maana wao ndio vibaraka wao afrika ya Tanzania hayawahusu
 
Bwana jela,

Umesoma katiba ya Kenya? Huwezi kuilinganisha na ya Tz. Ni nzuri mno!
uzuri wa katiba ni kutekeleza yaliyomo, lakini kenya haiko hivyo ndo maana kila baada ya uchaguzi ni vurugu na mtu analia kaibiwa kura mpaka anajiapisha mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…