Katiba ya Kenya ninayo hapa! Na ninayo ya Tz na pia ya Zanzibar. Katiba ya Kenya ni nzuri sana ila inaongoza Wanadamu wenye roho mbaya kama ilivyo ya Tz. Nipatapo muda nitaandika uzi wa kuzilinganisha hasa katika masuala ya sheria na uchaguzi. Matatizo ya Kenya yaliyopo sasa yanatokana na uchu wa madaraka na wala Sio katiba japo wapo katika harakati za kuboresha katiba yao baada ya kuwa nayo kwa miaka 10. Mfano mdogo ni kuwa kulingana na Katiba ya Kenya, hakuna kosa lisilodhaminika. Kosa la mauaji linadhaminika. Iwe uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha au lingine lolote yote unapewa dhamana. Hii imesababisha Polisi kuwabambikia watu kesi