Hawa mashabiki wa CHADEMA wana ufahamu mdogo sana! Wameshindwa mbinu zao sasa wanaomba hata kifo kije CCM tu wao wabaki, jambo ambalo haliwezekani. Yaani haka ka-uchaguzi wanategemea kalete vurugu za kuwafikisha The Hague CCM? Eti Lissu anatafuta kuungwa mkono Ulaya na US, kwa lipi? Nani aliona wazungu kumuunga mkono mtu asiye na maslahi kwao? Demokrasia ipi wakati kuna marais afrika hii wanaishi Ufaransa kwa amani bila hata kupigiwa kelele?
Kuna mambo ya msingi ambayo kwa miaka yote wabunge wa upinzani walistahili kuyapigia kelele, wao wakishaingia Bungeni tu, mambo yote ni dili za pesa, ufuska na ulevi wa Dodoma. Uchaguzi ukiwa mwaka huu ndo wanakumbuka tume huru. Huko mikoani wako chini ya mkuu wa mkoa/wilaya ambaye pia ni mkuu wa usalama mkoani/wilayani ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa (CCM) ya mkoa/wilaya! Hilo wanaliangalia tu na wanaona haliwaongezei posho, hawalalamiki. Bure kabisa!