Video: Wachina wana mpango gani na nchi yetu? Kuna hii store Mikocheni wanauza kila kitu 3,000. What's going on?

Video: Wachina wana mpango gani na nchi yetu? Kuna hii store Mikocheni wanauza kila kitu 3,000. What's going on?

Acha ujinga dogo.

Yaani unadhani Wachina wako hapa kuja kukurahisishia wewe maisha?

Kwanini hawataki kuanzisha VIWANDA kama wanawapendeni kweli.

Watu weusi ndo maana mlitawaliwa. Mnapenda mambo laini laini sana!

Eti ni "wakombozi"

Hahahaha!
Mchina sio mkombozi mkuu. Mkombozi winga.
 
Kawaida sana...
Japan ni nchi iliyoendelea lakini maduka ya namna hii yapo Kila mtaa...

Cc: Mahondaw

My point exactly. Japan ISHAENDELEA meaning tayari wananchi wake wana mitaji.

Sisi wafanyabiashara wetu mitaji hawana. Ukiruhusu WAGENI wafanye biashara kama hizi maana yake unaua wafanyabiashara wako wa ndani.

Hayo mastore yakiwa Marekani sijui Dubai ni sawa ila sio Tanzania.

Siku Wachina wakimiliki supermarkets na maduka yote nchi hii mtanielewa.

Kwani ukoloni ulianzaje?
 
Ni hivi: Wachina watakuja kufanya nchi isitawalike. Unajua ni wengi hawaoni hili lakini madhara yatakuja kuwapata raia wote, wenye fedha, viongozi na mafukara. Hili jeshi la vijana wasio na kazi ambalo CCM inalijenga litakuja kuisambaratisha nchi.
Katika ujumbe mzuri niliouona na kusoma leo ni huu. Hongera kwa kuwa na vision.
 
Kwamba kuuza mitumba ni huduma ambazo serikali na taasisi zimeshindwa kutoa?

Kabla ya hao Wachina kuja Watanzania tulikuwa tunatembea bila nguo na wanawake walikuwa hawavai urembo?

Ni huduma zipi kati ya ZINAZOLALAMIKIWA ambazo wachina wanatoa sisi tunashindwa kuzitoa?

Unaweka mamifano ya Whatsap sijui telecommunications mifano tofauti kabisa.

Wachina wanamiliki Startimes, Tekno, Infinix etc lini umesikia wabongo wanalalamika? Kinacholalamikiwa hapa ni Wachina kufanya kazi za Uchuuzi.
Hivi hata kuna uhusiano / communication kati ya fikra zako na unachoandika ? Mimi nimekwambia laumu sheria inapovunjwa na sio watu kuuza vitu kwa bei nafuu; Hakuna kosa la mtu kuuza vitu kwa bei ndogo au hata kutoa nyongeza hilo sio kosa na kama unataka kujua wanapataje faida ndio nimekwambia niulize nikupe business models za watu....

Na kukupa connection ni kweli serikali imeshindwa kuhakikishwa wananchi wake wana ujira wa kutosha kusustain needs zao na bila mchina kama manufacturer of the world na kwa maisha ya sasa wengi wangekosa luxuriously products, unaongelea mitumba ??? Uliza kabla ya ujio wa mitumba na viwanda vyetu ambavyo ni non existent kama watu walikuwa hawatembei na midabwada....

Serikali na nchi hii yenye mito na mabonde mengi yenye rutuba ingekuwa na watu wenye akili tungefurahia hao watu kutoka huko kwenye less resources waje huku watulimie kama enzi zile warundi walivyokuwa wanakuja kulimia watu mashamba (ila now its vice versa tunasema uchuuzi ndio kazi zetu zile creme de la creme hatuwezi tunawaachia wengine) na hatulalamiki sheria zinapovunjwa bali eti wanauza bei ndogo sisi walanguzi tunakosa kuuza....
 
Dollar store. Wenzetu wanayo ya aina hii kitambo sana. Kila kitu dollar moja.
 
Nani kakwambia wanauza vibanio vya nywele tu humo ndani. Wanauza vitu vingi sana humo ambavyo value yake sio 3000

But still, haimake sense kuanzisha hiyo store Mikocheni.
Sina baya na Wachina mimi kabisa mimi nina baya na Wabongo wanaotuibia yaan wanaotupiga mbongo unajua sio kabisa just imagine kapata chimbo km hilo la 3000 anachukua kidude cha 3000 huko anaenda kumkanda mbongo mwenzie 30,000 kitu kimoja cha 3000 tu anapata faida 27,000 na hapo mbongo anajiona amewin balaa yaan anapiga hesabu akipata watu km huyo 1000 mpaka 10,000 au 100,000 ndani ya mwaka kashaporomosha mjengo Goba, sasa hawa mimi ndio nawaona wabaya sio Wachina Wachina wana nia njema na sisi ila sisi kwa sisi ndio tuna nia mbaya ya kuumizana wenyewe kwa wenyewe sio kusaidiana na mbaya zaidi wengi hua wanayaficha maeneo km haya ila huyo mchina wa Mikocheni kashtukia Chezo kaamua atangaze wazee wa Machimbo hii wamechukia kweli kweli kwanini huyu Mchina kalitangaza hili chimbo wale Wachina wenye machimbo yao mengine ya kila takataka unazotaka wakitangaza tu machimbo yao ya bei rahisi tena yapo kibaaaaao hapa bongo namaanisha kibaaao bei rahisi ila wabongo wameyaficha wanafanya kupata faida sasa Wachina wenyewe wakiamua kuyatangaza utasikia milio ya Wabongo Wabongo watalia sana sababu ya roho mbaya kupiga wenzao tu

Kadet mchina anaiuza 5,000 mbongo Kadet ile ile quality's ile ile material yale yele kakaza sura anakuuzia 50,000 wewe hapo kati ya mbongo na Mchina unaenda kwa nani? Usishangae ndivyo tulivyo wabongo wizi wizi mwingi kila sehemu sio Serikalini tu hata huku Wabongo tunaibiana tu, sasa wanapokuja hawa wazee wa kunyoosha rula watu wanachukia wewe unachukua kitu 3000 unaenda kumuuzia mtu 30,000 kitu cha 3000?

Jingine linaenda kutungua Raba za Wachina kwenye Mabelo Ilala Boma Karume na machimbo mengine ya bei rahisi yapo kibao 3000 mpaka 5000 anakuja kukazia watu sura raba hio hio ya 3000/5000 anataka 30,000 mpaka 35,000 tena ukiingia kichwa kichawa anaanzia 50,000, kisa nini? eti ameipiga brush na kuipaka rangi na kiwi, hivi huyu mbongo ana akili kweli? Si umpeleke tu mwenzio umwambie raba zile pale 5000 nenda pale kachukue na wewe shida ipo wapi ni 5000 yako tu? Wabongo kuumizana tu na kutaka utajiri wa haraka
 
Wakuu,

Kuna hili duka la Wachina hapo Mikocheni pembeni ya Clouds linaitwa Citistore.

Hili duka ni la ajabu sana. Yaani kila kitu humo ndani kinauzwa 3000.

Yaani chochote, kuanzia accesories za wanawake, make ups na masuala ya urembo, stationeries na kila kitu humo ni 3000 tu. Ukipita hapo muda wote wanawake wanapanga foleni kwenda kununua bidhaa humo

Nimejiuliza sana. Wote tunajua kupata frame au eneo la biashara Mikocheni ni expensive sana. Wafanyabiashara wetu wengi wa kibongo wanapaepuka Mikocheni kwa sababu ni ghali sana kupata frame huko. Frame zetu nyingi Bongo ziko Mwenge na maeneo wanaoishi watu yaani residential areas kama huko Sinza, Ubungo na maeneo mengine

Inawezekanaje hawa Wachina, wachukue sio frame tu bali ni upande mmoja floor nzima in the heart of Mikocheni alafu wauze kila kitu 3,000. Wanapataje faida?

Hapo nimeongelea gharama za kodi ya eneo la biashara , sijazungumzia kulipa watu mishahara, kodi ya serikali, umeme na maintenance ya biashara. Wachina wanawezaje?

Wanapewa misaada ya kodi ya bandarini? Wanachukua vitu bure huko viwandani au ni mbinu gani inatumika mpaka wanaaanzisha store kubwa kama hii alafu wanauza chochote 3,000?

Mna uhakika hawa hawana plan ya ku-take over supply chain yetu yote? Huu sio mpango mkakati wa serikali ya China?

View attachment 3303936

ni fursa ya biashara hiyo, Acha mawazo ya kimasikini.. au unaendaga China nini?😅😅😅​
 
Isijekuwa wanauza bwimbwi
 
Halafu vyote ama vingi ni plastic
Hapa kuna mazaga kibao 3000 kila zaga unalogusa mpaka mswaki ukigusa 3000 dawa ya meno 3000 sabuni 3000 taulo 3000 perfume 3000 chochote unachokigusa ni 3000 hata iwe pin ndogo ukigusa tu bei ni 3000 usiseme fyoko ni 3000 rula imenyooka na vipino vimezingatiwa hutaki nenda kajionee au basi nenda kajinyee
 
Wabongo tuna matatizo siungani na anachofanya mchina ila
Kinachotokea leo kwa mchina ni maumivu ya kibiashara yaliyosababishwa na wafanyabiashara wa kibongo

Mbongo kitu cha tshs 10000 atakuuzia sh 50000 nitanunua leo kwako kwa hiyo 50000 ila siku nikijua ukweli hutoniona dukani kwako. Wabongo tubadilike inauma sana umepata pesa kwa shida halafu mbongo mwenzako anakuuzia bidhaa ya sh 10000 kwa sh 50000

Mfano
Mjmi nauza gari langu sh milion 5 nimemwambia dalali nitafutie mteja
Ajabu ni pale unasikia gari unalouza sh milion tano dalali analiuza milioji kumi na mbili na wateja wanaolitaka kwa milioi 5 au 6 anawakataa.

Nyakati zinabadilika tubadilike na turidhike na hicho kidogo tunachokipata
 
Ukienda kwa wageni ni wakweli, mfano bidhaa ile ile na inafafanana kwa kila kitu atakuambia bidhaa hii ni original inauzwa sh 200,000 na hii ni fekiinauzwa 80,000 ili wewe uchague..
Nenda kwa mbongo sasa bidhaa zote anakuambia bei sawa tena wakati mwingine atakuchoreshea ile feki so sad
 
Wabongo Wezi kinomanoma utapelitapeli kutaka kutajirika kwa njia za mkato
 
Jambo jingine watanzania sijui ni uoga au mentality zetu haziko sawa
Leo unaona mwenzako anateseka ww unafurahia kwasababu mateso hayo hayako kwako siku yamekufika ndo unaanza lalamika,

Unawapiga pesa ndefu watanzania wenzako unaona maisha umeyapatia leo unapigwa wewe unalalamika
 
Ukienda kwa wageni ni wakweli, mfano bidhaa ile ile na inafafanana kwa kila kitu atakuambia bidhaa hii ni original inauzwa sh 200,000 na hii ni fekiinauzwa 80,000 ili wewe uchague..
Nenda kwa mbongo sasa bidhaa zote anakuambia bei sawa tena wakati mwingine atakuchoreshea ile feki so sad
Mbongo anataka akuumize ili urudi akuumize tena ukienda tena urudi akuumize tena sasa siku ukigundua unaibiwa ndio hapo akili inapokurudi kwamba route zote nilikua najipeleka kwa kibaka?
 
Back
Top Bottom