Video: Wachina wana mpango gani na nchi yetu? Kuna hii store Mikocheni wanauza kila kitu 3,000. What's going on?

Video: Wachina wana mpango gani na nchi yetu? Kuna hii store Mikocheni wanauza kila kitu 3,000. What's going on?

Mnaona fursa mnaanza kulalama
Mkiletewa kitu kipya ndio mda wa kuiga

Malalamiko ya umasikini shida sana
Kama ni mpya huko si ufungue na wewe ya hivyo?
Mtaanza ooh mtaji baba uko wapi?
Changamkeni
Huku maduka ya hivyo walifungua wazungu, ila sasa hivi Wadosi wamefungua kila sehemu Ulaya
 
Ni hivi: Wachina watakuja kufanya nchi isitawalike. Unajua ni wengi hawaoni hili lakini madhara yatakuja kuwapata raia wote, wenye fedha, viongozi na mafukara. Hili jeshi la vijana wasio na kazi ambalo CCM inalijenga litakuja kuisambaratisha nchi.
Japo wanasaidia kushusha gharama za maisha.....hawa wa kwetu mtu anataka faida hata mara 50 ya bei aliyonunulia huko+kodi
 
Wakuu,

Kuna hili duka la Wachina hapo Mikocheni pembeni ya Clouds linaitwa Citistore.

Hili duka ni la ajabu sana. Yaani kila kitu humo ndani kinauzwa 3000.

Yaani chochote, kuanzia accesories za wanawake, make ups na masuala ya urembo, stationeries na kila kitu humo ni 3000 tu. Ukipita hapo muda wote wanawake wanapanga foleni kwenda kununua bidhaa humo

Nimejiuliza sana. Wote tunajua kupata frame au eneo la biashara Mikocheni ni expensive sana. Wafanyabiashara wetu wengi wa kibongo wanapaepuka Mikocheni kwa sababu ni ghali sana kupata frame huko. Frame zetu nyingi Bongo ziko Mwenge na maeneo wanaoishi watu yaani residential areas kama huko Sinza, Ubungo na maeneo mengine

Inawezekanaje hawa Wachina, wachukue sio frame tu bali ni upande mmoja floor nzima in the heart of Mikocheni alafu wauze kila kitu 3,000. Wanapataje faida?

Hapo nimeongelea gharama za kodi ya eneo la biashara , sijazungumzia kulipa watu mishahara, kodi ya serikali, umeme na maintenance ya biashara. Wachina wanawezaje?

Wanapewa misaada ya kodi ya bandarini? Wanachukua vitu bure huko viwandani au ni mbinu gani inatumika mpaka wanaaanzisha store kubwa kama hii alafu wanauza chochote 3,000?

Mna uhakika hawa hawana plan ya ku-take over supply chain yetu yote? Huu sio mpango mkakati wa serikali ya China?


Waungwe mkono hao wachina wanatu faa mbona kuna waarabu waislamu wameingizwa muhimbili watu mlikuwa mna sifia sasa hao wachina wanao jitafutia kwa kutufanyia wepesi wa maisha wamekuwa nongwa ambao wameleta mitaji wao wenyewe..? Mbona waarabu wamepewa bandari yetu tuliyo igharimia wenyewe kwa mabilioni ya shilingi bure tena milele daima ..je wale wasudani pale muhimbili nani anaye wagharimia kama siyo serikali ya samia na ccm
 
Mimi Naona kwa jicho la Fursa nzuri kwa Wazawa sijui wenzangu
 
Sasa siku ile soko ya Ubungo ikianza operations, servers za JF zitapona?!

Maybe tujaribu ku tune mindset zetu na kuona fursa kwenye hili, tupambane kuanzisha viwanda vyetu tuweze ku dominate soko letu la ndani vinginevyo, Tanzania sio kisiwa…
 
Nadhani Watu tuna miss point ya msingi hapa.Na wengine wanamlaumu Mleta uzi kwamba ana wivu.Kikubwa ni kwamba hilo duka ni la kurahisisha uuzaji wa bidhaa zao wanazozalisha China.Huwezi kukuta kuna bidhaa ya kwetu au kwingine.Ndio kusema hata kama hump kipo cha elfu kumi kitafidiwa na bidhaa nyingine iliyopaswa kuuzwa mia tano au elfu moja, kikubwa kwao ni mauzo yawe mengi.Tatizo hapa ni kuwa bidhaa za aina hiyo hamtokaa mzitengeneze wenyewe kwani wataleta wao maelfu ya makontena.Kama tuna akili timamu hayo si ya kushabikia.Kama wanatupenda basi wangeleta hiyo teknolojia tuzalishe wenyewe . Sisi kujazana hump dukani ni kukuza shira China na kwenu kubaki kuwa Waendesha Bodaboda.
Wakizalisha hapa bei si itakwenda juu mkuu kutokana na gharama za umeme, maji, vibali nk vinavyotozwa na serikali. Gharama ya uzalishaji ikiwa juu si watatuuzia bidhaa kwa bei ghali sana.

Sasa bora tunufaishe wanunuzi ambao ni wengi au tuwaumize wananchi wengi na kufurahia ajira 5 zitazotolewa kwa wazawa?
 
Kitu ningewashauri wafanyabiashara wangekomaa kupambana wapunguzwe makodi yasiyo na msingi, ukichunguza wanapigwa makodi ya ajabu ajabu sana, badala wakomae na hilo ambao linaweza wapa hata wao uhuru wakuweka bei shindani wanakomaa na wachina.

Wachina wapo sana, na sio wachina tu ukicheki wamilikiwa properties nyingi kule Fumba Town Zanzibar ni foreigners (wa mataifa mbalimbali), nao miaka 5, 10 mbele wanaweza kuzama kwenye biashara yeyote hapa nchini.

Mimi kwangu kitu kikubwa nilichokiana ni kodi za kijinga, hao wachina hawana shida na wamepewa vibari na viongozi wenu, nyie mnawalalamikia bure sana. Hakuna kiongozi wenu ambaye hajui kuhusu uwepo wao mjini.
 
Au unaonaje tungewashukia na WhatsApp kutoka huduma ya calls na mengineyo bure hivyo kuwanyima faranga kina TTCL...
Hivi Skype walilalamika kuhusu WhatsApp kuwa na feature ya call?? Juzi nimeshangaa kuona Viber app bado ipo aisee, hawa walikua na feature ya call free kitambo sana
 
Hizo bidhaa ni recyclable? Au wamegeuza Tz dumpo? Au baada ya mwezi bidhaa haifai tena kwa matuzi? ni yenye ubora duni sana.
 
Hawa wana uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu wanaleta kwa wingi na kule kwao wananunua viwandani au wengine ndiyo wenye viwanda. Mtanzania hawezi kushindana nao na baada ya miaka kadhaa wauza nguo na bidhaa kutoka China wengi watafunga maduka yao na kubaki maduka makubwa kama hayo. Usisahau pia wachina ni very corrupt hivyo sehemu kama bandarini ni lazima watakuwa wanahonga na kodi kuwa chini. Na kingine: bidhaa wanazouza ni za quality za chini na nyingine zina chemical zinazodhuru. Kwa mfano Ulaya kuna hizi zinazoitwa ''ultra fast fashion'' , nguo zinazotoka China na kuuzwa online kwa bei chini sana, wameanza kuzipiga marufuku au kuziwekea sheria kali.
Uko sahihi. Bongo kama hakuna serikali. Unakuta mijitu imekaa ofisini haitaki kuajiri vijana. Vijana wanajiajiri halafu wanawaleta wachina wachuuze bidhaa ambazo zingeweza kuchuuzwa na vijana wa nchini. Wapumbavu wanaamini ccm inawasaidia kumbe inawakandamiza waendelee kuwa maskini ili wawatawale vizuri.

Adui wa kwanza wa taifa ni ccm, wa pili ni cccm, watatu ni ccm, wa nne ndio ujinga kisha unafuata umaskini.
 
Nadhani Watu tuna miss point ya msingi hapa.
Nadhani point ya msingi kaipoteza kwenye kulalamikia bei ndogo (kama vile kuna mashindano ya kumkomoa mlaji wa mwisho ) tunasahau kwamba sababu ya huyu mchina kuuza blender au tuseme kibanio kwa elfu tatu mtu huyu anabakia na elfu mbili za kwenda kununua nyanya...
Na wengine wanamlaumu Mleta uzi kwamba ana wivu.Kikubwa ni kwamba hilo duka ni la kurahisisha uuzaji wa bidhaa zao wanazozalisha China.
China ni mzalishaji wa dunia sio sisi tu bali sehemu zote sababu wamejiposition kuweza kutengeneza bidhaa kwa gharama nafuu kuliko wengine, na hapa kama muuzaji una choice ukiona kuuza maplastiki ya urembo ya kichina hayafai tengeneza mikufu ya shanga ya kimasai na uuze ; Badala ya kungagania kutengeneza vitu ambavyo hatuna comparative advantage labda ifike wakati tujiulize tunaweza kuzalisha nini kwa ubora na sio kuuza ndani tu bali mpaka nje
Huwezi kukuta kuna bidhaa ya kwetu au kwingine.Ndio kusema hata kama hump kipo cha elfu kumi kitafidiwa na bidhaa nyingine iliyopaswa kuuzwa mia tano au elfu moja, kikubwa kwao ni mauzo yawe mengi.Tatizo hapa ni kuwa bidhaa za aina hiyo hamtokaa mzitengeneze wenyewe kwani wataleta wao maelfu ya makontena.
Je tunaweza kutengeneza cheaper kuliko kununua ? Kumbuka kwamba hapa unaongelea mwananchi asiye na disposable income ni kwamba hizo ukizifanya buku kumi huenda asinunue, sasa ifike wakati tuwaze jinsi ya kumuongezea kipato huyu mwananchi sababu as things stands amepigika, na mchina ni chembe ya matatizo na hata akiondoka tutaendelea kubaki na masikini wasio na vibanio na urembo wa elfu tatu tatu..., Cha kufanya ni complete overhaul ya mfumo mzima; na mpaka dakika hii huyu mchina ni mkombozi wa huyu mbangaizaji

Kama tuna akili timamu hayo si ya kushabikia.Kama wanatupenda basi wangeleta hiyo teknolojia tuzalishe wenyewe . Sisi kujazana hump dukani ni kukuza shira
Kwanini wakupende ? Trade ni Quid Pro Quo, kwahio wataendelea kupata wateja kama tu wanunuzi wanaona value na pili unaweza kusema hivyo vitu vingine kuna watu huko wanatengeneza wakiwa kwenye madorminotry na kulipwa peanuts, it just happen wao ni wachapakazi na wanazinfaya kwa bidii bila kulaumu issue sio teknolojia issue ni vigumu kutengeneza hizo bidhaa as cheap kama wao (sababu wana comperative advatange na economy of scale) that's a fact and wont change anytime soon
China na kwenu kubaki kuwa Waendesha Bodaboda.
Hata hizo boda shukuru wahindi na wachina ama sivyo hao boda tungekuwa tunakabana kitaa, hali ni mbaya na kesho yetu ni balaa sababu leo hatujajipanga, tena leo hawa wana nguvu zao vipi kesho wakiwa wazee na hata pensheni hawana

 
Sasa hivi mabonanza ya wachina yapo hadi vijijini ndani ndani kabisa, kwenye kutafuta hela mchina hacheki na mtu
 
Wakuu,

Kuna hili duka la Wachina hapo Mikocheni pembeni ya Clouds linaitwa Citistore.

Hili duka ni la ajabu sana. Yaani kila kitu humo ndani kinauzwa 3000.

Yaani chochote, kuanzia accesories za wanawake, make ups na masuala ya urembo, stationeries na kila kitu humo ni 3000 tu. Ukipita hapo muda wote wanawake wanapanga foleni kwenda kununua bidhaa humo

Nimejiuliza sana. Wote tunajua kupata frame au eneo la biashara Mikocheni ni expensive sana. Wafanyabiashara wetu wengi wa kibongo wanapaepuka Mikocheni kwa sababu ni ghali sana kupata frame huko. Frame zetu nyingi Bongo ziko Mwenge na maeneo wanaoishi watu yaani residential areas kama huko Sinza, Ubungo na maeneo mengine

Inawezekanaje hawa Wachina, wachukue sio frame tu bali ni upande mmoja floor nzima in the heart of Mikocheni alafu wauze kila kitu 3,000. Wanapataje faida?

Hapo nimeongelea gharama za kodi ya eneo la biashara , sijazungumzia kulipa watu mishahara, kodi ya serikali, umeme na maintenance ya biashara. Wachina wanawezaje?

Wanapewa misaada ya kodi ya bandarini? Wanachukua vitu bure huko viwandani au ni mbinu gani inatumika mpaka wanaaanzisha store kubwa kama hii alafu wanauza chochote 3,000?

Mna uhakika hawa hawana plan ya ku-take over supply chain yetu yote? Huu sio mpango mkakati wa serikali ya China?


Pokea hiyoo

Ova
 

Attachments

  • Screenshot_20250518_093902_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20250518_093902_WhatsApp.jpg
    266.7 KB · Views: 21
Niliona dubai maduka ya riyal 20 (tzs 12,000 ) kila nguo, mitas ya deira pale ( ndo kariakoo yao)

tofauti ya Dubai na huku, kule utakuta walalaho wawili watu ndio wanayzongea hayo maduka, Huku nchi nzima utaikuta hapo. Kule hayawezi kuwa na athari bali huku yataleta ahari tena kubwa.
 
Back
Top Bottom