Nakumbuka zamani ile naenda kujiunga na gym (ya mtaa) ila iko smart sana, mara ya kwanza kuingia ndani tu nilishtuka asee kuna madogo na mafather wamekata yani ndani unakuta watu kazi watu chuma tuu.
story mkiwa ndani sasa utasikia, fulani umu ndani ndo king alipiga askari watano kwa pamoja usimchezee na story nizakweli. Kuna jamaa mmoja alikua anapenda kutembea usiku sana akikutana na kibaka anampasua uso anamtoa jino anakuja nalo gym kutuonesha.
Kwaiyo ilikua kama challenge ivi, huwezi kua member verified bila kua na tukio la kishujaa na huwez kua top member bila matukio endelevu.
Kufikia tu mwezi nkajikuta nisha adapt kuvaa mashati makubwa, kunyoa upara, kuvaa viatu vya seft tu kama timberland and etc. Mtaani nikawa mkombozi watu wakidhulumiwa naitwa nikasuruhishe.
Sasa sikuizi izi gym ziko mixed na wanawake dah naona ni kama kuhamasishana uzinzi tuu. Tulikua tunafanya mazoez ya pumzi sana ila pale hakuna ambae alishawahi kufanya ayo mazoez ya squats kubinua tako ivo hell no.