Watoto wa shule za kata ni wasumbufu sana. Walimu wanatakiwa kuishi na hao watoto kwa tahadhari kubwa. Na wakati huo huo mashinikizo ya kulazimisha wafaulu, hata kama hawataki shule, wana uwezo mdogo wa kuyamudu masomo! hutamalaki kila upande.
Mzazi kama una uwezo, na mtoto wako anajitambua; ni bora umpeleke tu shule za private. Binafsi sijutii kuwasomesha watoto wangu shule za private. Shule za kata zimejaa watoto wengi wasumbufu, watukutu, wasiojitambua, nk. huku wale wastaarabu na wanaojielewa wakibakia kuwa wachache.