Wakipiga marufuku kupiga mashuleni,
Hata ukatili majumbani utapungua pia
Serikali ndio chanzo cha ukatili na wanashindwa kutoa maamuzi magumu
Huwezi kusema tu tutaliangalia
PM hana maamuzi peke yake ni lazima lijadiliwe kwa upana
Kila leo tunasikia ooh nchi ya Amani lakini kuna ukatili zaidi ya nchi zenye vita
Mara baba kamlawiti mwanae, wanawalawiti na watoto wanashindwa kusema kwa sababu na shule wakienda wakishindwa kujibu wanachapwa na hao wapumbavu badala ya kumuuliza mtoto nini kinachokusibu mpaka unakuwa mnyonge hivyo?
Mwalimu hana ukaribu na mwanafunzi anamuona kama adui yaani kama mfungwa na gereza au mgonjwa na nesi au doctor yaani wote wamoja
Hii ni kwa sababu hatuongei kwa kutaka kujua tatizo na kutatua bali ni matusi, kufoka, adhabu na fimbo na hata kuuwa kabisa
Poleni sana kama hamtabadilika mtaishi kama wanyama tu