Video ya Mzungu huyu TZ Ina views wengi ndani ya siku moja kuliko royal tour

Video ya Mzungu huyu TZ Ina views wengi ndani ya siku moja kuliko royal tour

Hizo pesa baadhi zilizotumika huku tungempa huko kama zawadi kwa kututangaza...

Ila all I can say is Thanks Mzungu kwa kazi nzuri
 
Video zake zipo clear na safi si Kama zile za bilioni saba
 
Kuna huyu Mzungu yupo huko you tube huwa anafanya documentary kuhusu misosi na utamaduni ndani ya nchi mbalimbali duniani na channel yake Ina nguvu sana. Inaitwa best ever food review show, Sasa huyu mtu ana subscription za you tube mil8.4 zaidi ya diamond platnumz, huyu mtu ameitangaza nchi ya Tanzania kiutalii Duniani zaidi ya filamu aliyoicheza chief H.

Katika documentary yake inayohusu mambo mbalimbali ya utamaduni wa Tanzania, ameweza kupata views milioni moja ndani ya siku moja huku akiipiku Filamu ya royal tour iliyochezwa na Chief ambayo hata view laki mbili haijafikisha. Huku gharama zikivuka bilioni 11 za Kitanzania.

Sasa Hoja ni kwamba, Kwanini serikali hii ya CCM , isitumie watu Kama Hawa wanaweza kufika pahala pengi duniani kuliko kutumia watu wenye connection chache Kama peter.

Huyu Mzungu documentary yake ametengeneza kwa pesa yake mwenyewe , hajachangiwa na Tanzania foundation sijui Nininini Sasa watanzania mtafakari, naweka link ya documentary aliyoitengeneza na kupata views mil 1 ndani ya siku 1 inahusu tanzania.



Wachaga na nyie Mzungu kawatengenezea royal tour yenu.

Kweli wewe ni mjanja. Nilitizama nikaona ni watanzania wachache Sana wameona video ya huyu bwana. We ni mjanja, I salute you.
 
Nimeiangalia iko vizuri sana,japo yeye kadili na kabila moja tu wazigua,hasa kwenye tamaduni yao ya kucheza na nyoka na chakula kwa ujumla.
Kafanya na wamasai, wachaga, na dar alienda feri, alienda cocobeach, alienda Kwa chef mwabuki, na Kwa mama ntilie
 
hivi, kwanini tusikamate watu 50 wenye viewers kama huyu huko ulaya tuwape pesa kidogo wawe wanatutangaza, kuliko kwenda kuweka matour na kwenye matv n.k. though sibezi royal tour, ila naona kama hawa watakuwa cheaper. hatujachelewa, tunaweza kujipanga upya tukafanya kitu.
 
Back
Top Bottom