JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tuweke mzigo mezani
Ndugu zangu kuna hii taarifa, yupo yeyote ambaye anajua ukweli wake, maana mtu ambaye yupo ndani mgodini amenitumia ujumbe huu ambao nimeambatanisha na picha alizotuma:
BARRICK NORTH MARA YAFUNGULIA MAJI YA SUMU NA KUTEKETEZA SAMAKI MTO MARA
Jitihada zimefanyika ili kujua ukweli wa hii habari. Ametafutwa mmoja wa ‘supervisor’ katika Mgodi wa Barrick North Mara, Elly Shimbi na kuulizwa kuhusu ukweli wa taarifa hiyo alisema:
“Mimi siwezi kulizungumzia hilo suala, mtafute msimamizi mkuu wa mradi ndiye atakwambia, kama una taarifa hizo mimi siwezi kukwambia chochote.”
Elly Shimbi hakutoa ushirikiano wa mawasiliano ya mkuu wake wa kazi ambaye alitaka atafutwe yeye kuhusu suala hilo.
Licha ya kutotoa ushirikiano huo, Ofisi ya Barrick iliyopo Dar es Salaam ilithibitisha kuwa Shimbi ni mmoja wa ‘supervisor’ ambaye bado yupo kwenye majukumu yake Barrick North Mara.
Tayari bosi ambaye ndiye msimamizi wa mgodi huo ametumiwa taarifa hii kwa njia ya e-mail baada ya namba yake kutopatikana lakini haijajibiwa.
======
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Eng. Samuel Gwamaka Mafwenga, ameiambia JamiiForums leo tarehe 10/03/2022 kwamba, kutokana na taharuki iliyotokea baada ya Picha za Samaki waliokufa kusambaa Mitandaoni wanaodaiwa ni kwenye Mto Mara, tayari timu ya Dharura imeundwa kuchunguza swala hilo.
Mafwenga amesema timu hiyo inahusisha Watu kutoka NEMC, Bonde la maji la Ziwa Victoria, Mkemia Mkuu wa Serikali na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara.
"Hivi sasa tunapozungumza, tayari Kamati ipo Sehemu ya tukio Wakichunguza ili tujue chanzo ni nini na kimetoka wapi. Sisi tunaangalia afya na Uhai wa Binadamu na Wanyama." amesema Mafwenga.
Pia soma ;
1). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
2). Eti, "Kinyesi cha mifugo chatajwa kuwa chanzo cha kufa samaki mto Mara"
3). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko