Mtoto wa Malecela wa kiume aliyekuwa anajulikana Oysterbay ni marehemu Ipi Malecela.
Ipi alikuwa anaendesha Benz anapenda kupiga nyimbo za Notorious BIG Oysterbay Beach.
Ipi alikuwa akirudi kutoka Uingereza lazima Bonny Love amtangaze club, "Ipi Malecela straight from London".
Alikuwa anawaletea watu wa Clouds records (LP), tena akiwaletea records anawanunulia mbilimbili, moja anampa DJ Bonny Love, nyingine anampa Kusaga.
Sasa watu walikuwa wanashangaa inakuwaje Bonny Love anamfagilia sana Ipi Malecela? Kumbe Ipi alikuwa anawanunulia sana LPs Clouds.
Mzee Malecela alikuwa anamuandaa Ipi kwenye chama, akawa kiongozi jumuiya ya vijana, akafariki katika mazingira ya utatanishi naye.
Mzee Malecela akaulizwa kama anataka mwili wa Ipi ufanyiwe autopsy madaktari wajue vizuri kilichomuua, lakini Mzee Malecela alikataa, akisema yote ni mapenzi ya Mungu tu.
Marehemu William "LeMutuz" alikuwa mkubwa sana kwetu nafikiri alishaingia kwenye ubaharia miaka hiyo, hivyo watu wengi wa rika letu hatukupata kumuona tulivyokuwa Oystebay.
Mimi William nimekuja kukutana naye baadaye kabisa New York.