Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

View attachment 2097715
Router ni hio mkuu si kama vile vi mifi.

View attachment 2097718
Ina ports za kawaida za Ethernet kama unataka kutumia waya badala ya wifi
View attachment 2097719
Hicho ndo kibox kinacho convert.
Kwenye michoro ya hapo juu, box 1 linaitwa ADSL filter, na box 2 linaitwa router, sometimes modem inaweza kuchukua nafasi ya router

ADSL filters (a).png
 
Kwenye huo mchoro, box 1 linaitwa ADSL filter, na box 2 linaitwa router, sometimes modem inaweza kuchukua nafasi yake baadala ya router

View attachment 2097739
Mkuu adsl zime evolve ni kweli zamani walikuwa wanatumia simu ila Adsl 2+ router zake hazitumii.

Pia hizi router zina built in modem hivyo wamerahisisha unapata modem na wifi papo hapo.
 
Mkuu adsl zime evolve ni kweli zamani walikuwa wanatumia simu ila Adsl 2+ router zake hazitumii.

Pia hizi router zina built in modem hivyo wamerahisisha unapata modem na wifi papo hapo.
Nimekupata. Kwahiyo ADSL internet za siku hizi hapa TZ ni ADSL+?, na ISP wa siku hizi wakikufungia ADSL hawakupi simu ya mezani?
 
Adsl pia ni ya kizamani mkuu ila ina unafuu compare na Satelite.

Unakumbuka zamani enzi za modem za 3.2mbps? Kipindi cha 3g unasubiria movie nusu saa idownload. Expect speed kama hii kwa adsl.

Yenyewe inatumia zile waya za shaba ambazo zamani tulitumia kwenye simu za mezani. Na ukiunga adsl unapewa na namba yako kabisa inayoanziwa na 0222 kama ya simu za mezani.

Fiber ni mziki mwengine ipo fast sana hasa ping, ni 1ms ama 2ms, sometime wakati unabrowse ni kama hutumii internet ukigusa tu inafunguka. Sema coverage yake kwa sasa ni ndogo sana ipo tu mjini katikati.

Hivyo mkuu nenda tawi la TTCL karibu na Nyumbani ulizia, kama Fiber ipo kwako unga hio 20mbps kwa 55,000 ni bei nzuri sana.

Kama haipo covered adsl ndio option iliobakia. Adsl naona kifurushi cha 25000 na 50000 vina value zaidi 4mbps na 8mbps. Mimi siamini kama adsl ya TTCL inaweza gonga 8mbps hivyo nimechukua cha 4mbps, unaweza jaribu cha 50000 ukaleta feedback.
Juzi nilipita duka la ttcl mcity wakaniambia fibre ipo maeneo ya sinza.

Huko kwingine kuna copper.
 
Hivi mkuu, internet huwa haikatiki/haipotei hewani na inarudi baadae?

Niliwahi sikia hili tatizo.
Kwa Zuku haikatiki, hii Adsl ya TTCL ilikuwa inazingua siku ya kwanza baadae sijui wakaniambia hawajapunch ila now siku kama ya 3 naona ipo vizuri.

Kwa uzoefu fiber ipo poa sababu ni miundombinu mipya, kifupi ina capacity kubwa na haijajaa, hivyo early adopters wanafaidi kwa sasa, sijajua kwa baadae tukiwa wengi.
 
Ukishaona internet unapimiwa kwa speed ujue ni unlimited. Ingekuwa limited kwa GB kadhaa wangekupa full speed ili GB ziishe haraka.

Zote satelite ya Konnect, Adsl ya TTCL na hizi Fiber ni unlimited tena bila vikwazo, Zuku nadownload games kubwa kubwa Over GB 100, Inastream youtube na Netflix almost 24 hours per day tena Nyumba zaidi ya moja na sijaona hata siku moja wakileta Longolongo.

Too bad haipo hvyo kwa Konnect [mention]Chief-Mkwawa [/mention]
 
Ndio mkuu ni filter, na router tu na hizo waya basi.
Najiuliza tu, huwezi kuichukua hii Home unlimited internet kutoka ndani ya nyumba ukaitumie nje mbali ya nyumba?, yaani kwa kuichukua kwa kutumia vifaa kama Mi-Fi au pocket Wi-Fi. Au kuna vifaa maalum vya kuichukua kwenda kuitumia mbali?
 
unaweza kama kuna line of sight, utumie zile transmitter
non-line-of-sight-wireless-bridge-system.jpg

otherwise huwezi tumia kama line sababu inakuja na waya.
 
unaweza kama kuna line of sight, utumie zile transmitter
non-line-of-sight-wireless-bridge-system.jpg

otherwise huwezi tumia kama line sababu inakuja na waya.
Juzi kati nilikaa na jamaa zangu wa kitaa, nao wanalalamika bei mbaya ya vifurushi vya intaneti, nikawapa hii altenative ya ADSL na fiber. Kama unavyowajua Wabongo, kuridhika na kitu mpaka waulize maswali mengi. Wamekubali ila wameniuliza maswali ambayo mimi mwenyewe nimetaka kujua majibu yake. Wanataka kujua kama kuna alternatives za kupunguza gharama za kujiunga na hizi huduma za wired internet. Nina imani hakuna kisicho na alternative:

1: Kama unatumia ADSL, ukinunua router ya fiber bila kumtaarifu ISP, kuna uwezekano wa kukubaliwa kununua vifurushi vya fiber?

2: Kwa ISP wanaotilia mkazo kukufungia kwa gharama, ukinunua mweyewe vifaa na kufunga mwenyewe, halafu kazi yao iliyobaki ni kukufungia waya kutoka kwenye nguzo na kukuuzia vifurushi, inakubalika?

3: Vifaa vyako vyote vikiwa universal (visivyo tumia ISP mmoja tu), kuna uwezekano wa kununua vifurushi kutoka mtandao wowote?, mfano mwezi huu unanunua Voda, mwezi ujao unanunua TTCL.

4: Ipi njia nzuri ya kutumia kiasi kidogo cha pesa kufungiwa fiber kati ya hizi, kufungiwa fiber direct?, au kufungiwa ADSL kwanza halafu baadaye ununue router ya fiber?
 
Mimi nina katatizo kidogo naomba nisaidiwe. Nina router ya Tigo 4G ila nikiitumia bando ninalokuwa nimejiunga linaisha haraka. Nimefanya uchunguzi nimegundua hata pale ninapokuwa si browse lakini bando linakuwa linaendelea kuliwa. Kama kuna namna ya kurekebisha au kutatua hili tatizo naomba nisaidiwe. CHIEF MKWAWA
 
Juzi kati nilikaa na jamaa zangu wa kitaa, nao wanalalamika bei mbaya ya vifurushi vya intaneti, nikawapa hii altenative ya ADSL na fiber. Kama unavyowajua Wabongo, kuridhika na kitu mpaka waulize maswali mengi. Wamekubali ila wameniuliza maswali ambayo mimi mwenyewe nimetaka kujua majibu yake. Wanataka kujua kama kuna alternatives za kupunguza gharama za kujiunga na hizi huduma za wired internet. Nina imani hakuna kisicho na alternative:

1: Kama unatumia ADSL, ukinunua router ya fiber bila kumtaarifu ISP, kuna uwezekano wa kukubaliwa kununua vifurushi vya fiber?
Tofauti na mitandao ya simu, Fiber na Adsl ni miundombinu miwili tofauti. Wanakuletea waya nyumbani toka nguzo zao, ukiletewa waya wa adsl hauwezi pitisha bandwidth ya Fiber. Mfano adsl max ni 24mbps wakati fiber ni zaidi ya mara 1000 speed yake.hivyo ukiunga adsl ni adsl ukiunga fiber ni fiber.
2: Kwa ISP wanaotilia mkazo kukufungia kwa gharama, ukinunua mweyewe vifaa na kufunga mwenyewe, halafu kazi yao iliyobaki ni kukufungia waya kutoka kwenye nguzo na kukuuzia vifurushi, inakubalika?
Atleast TTCL wanaruhusu ila kampuni nyingi installation ni bure.
3: Vifaa vyako vyote vikiwa universal (visivyo tumia ISP mmoja tu), kuna uwezekano wa kununua vifurushi kutoka mtandao wowote?, mfano mwezi huu unanunua Voda, mwezi ujao unanunua TTCL.
Hii inawezekana kwa mitandao ya simu tu, Fiber ili ubadili provider inabidi wa kwanza atoe Nyaya zake mwengine aje kuweka zake.
4: Ipi njia nzuri ya kutumia kiasi kidogo cha pesa kufungiwa fiber kati ya hizi, kufungiwa fiber direct?, au kufungiwa ADSL kwanza halafu baadaye ununue router ya fiber?
Kama kwako kuna access ya Fiber vyema uende fiber moja kwa moja ina speed kubwa zaidi hata kama mnashare wengi speed haitapungua sana.
 
Back
Top Bottom