Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Wakuu habari?
Hivi vifurushi vya halotel m2m mnavielewa siku hizi. Juzi tu Alhamisi saa 8 za mchana nilijiunga bando la wiki zile gb 4 katika matumizi yangu nimetumia kama zimefika ni gb 2 tu jana asubuhi eti bando limeisha na hii haikuishia hapo tu hata huko nyuma nilijiunga bando la gb 18 kama mara 3 hivi linakata kimazingaombwe na kibaya zaidi nikijaribu kuuliza salio sms haitumwi nikajua zimebaki na gb ngapi kwa bando langu?? HIVI WADAU HII IMEKAAJE NI KWANGU MIMI TU NAPITIA CHANGAMOTO HII AU NA WENZANGU MPO?

Halotel wanakupa bando (Nusu) ila sms ya salio utajua utakapoipata
 
Hii ndio solution pia nataka kuweka Savana .Kwanza bei yao ni 49k na sijasikia malalamiko kwa mtu hata mmoja so far.

Ttcl walitutumia msg kuomba radhi kuhusu speed ila hamna kilichobadilika. Uzuri sehemu ina kila Fiber unayotaka, kulalamika ni kujitakia tu.

Kuna wengine wanaitwa Neso nimeona wamebandika matangazo yao kwenye nguzo.
Hivi hiyo savana hicho cha 49k kina uwezo wa kuunganisha vifaa vingapi?
 
Hivi hiyo savana hicho cha 49k kina uwezo wa kuunganisha vifaa vingapi?
Idadi ya vifaa ni router yako na sio speed ya internet, 40mbps inaweza hudumia hata watu 50 assume wanatumia Tu matumizi ya kawaida streaming, kuchat, kuperuzi etc. Ila router atakayokuletea ISP itakua ya bei rahisi maana anakupa bure, at most watu 30 itaunganisha na speed pia haitakua kubwa Sana maana zinatumia WiFi za zamani WiFi 4 na 5.

Kama unataka kuunga watu wengi unanunua router ya maana WiFi 6/7 ambazo zina bandwidth za kutosha kuhudumia watu wengi.
 
Idadi ya vifaa ni router yako na sio speed ya internet, 40mbps inaweza hudumia hata watu 50 assume wanatumia Tu matumizi ya kawaida streaming, kuchat, kuperuzi etc. Ila router atakayokuletea ISP itakua ya bei rahisi maana anakupa bure, at most watu 30 itaunganisha na speed pia haitakua kubwa Sana maana zinatumia WiFi za zamani WiFi 4 na 5.

Kama unataka kuunga watu wengi unanunua router ya maana WiFi 6/7 ambazo zina bandwidth za kutosha kuhudumia watu
ISPs wanakubali ku-replace Router yao na ile aitakayo mteja?.
 
Wakuu, habari.
Nahitaji kutoa lock kwenye router ya Airtel (toleo la kwanza). Kama kuna mwenye ufahamu wa jinsi ya kufanya hivyo, au anayemfahamu mtu anayeweza kunisaidia, naomba tuwasiliane kupitia PM.
Asanteni.
 
Hii ndio solution pia nataka kuweka Savana .Kwanza bei yao ni 49k na sijasikia malalamiko kwa mtu hata mmoja so far.

Ttcl walitutumia msg kuomba radhi kuhusu speed ila hamna kilichobadilika. Uzuri sehemu ina kila Fiber unayotaka, kulalamika ni kujitakia tu.

Kuna wengine wanaitwa Neso nimeona wamebandika matangazo yao kwenye nguzo.
Nawatumia kitambo ni wanaitwa netsolution wapo mkabala na chuo Cha cbe dar...hawana longolongo kabisa...mwanzo walikuwa wanaringa sahizi safii baada ya savvana kumwingilia kwenye makazi yake
 
Sio lazima ureplace, unatumia waya wa Ethernet kuunganisha router mbili, sababu Ethernet ina Nguvu kuliko WiFi haziwi bottlenecked so router ulionunua ya pili ndio unafanya configuration zako, kama unauza ama ni office etc.
Hapo kwenye ku configure router ya pili asisahau kuzima option ya DHCP SERVER yake ili kuepusha IP Configuration Failure kwenye vifaa vitakavyo unganishwa nayo... Ile Router ya ISP ndiyo iwe ubongo wa kugawa IP na second iwe AP tu ya kuchukua internet na kusambaza au kama akipata Router yenye Port ya SFP ni advantage zaidi anaweza itoa kabisa hiyo ya ISP kama hawaja block internet yao kua inatumika na router zao tu..
 
Wakuu imekua proved kuhusu FUP ya TTCL kuna rafiki angu anawatumia sana miaka kaniambia jana insider mmoja kamwambia wana FUP hiko kifurushi cha 100k ambacho speed 150Mbps alkua anapenda kuunga kina 2TB limit..

Fikiria cha 100k FUP ipo 2TB je cha 55k vipi? 😂😂🫵

Chief-Mkwawa

WA_1785658734536.jpeg
 
Wakuu imekua proved kuhusu FUP ya TTCL kuna rafiki angu anawatumia sana miaka kaniambia jana insider mmoja kamwambia wana FUP hiko kifurushi cha 100k ambacho speed 150Mbps alkua anapenda kuunga kina 2TB limit..

Fikira cha 100k FUP ipo 2TB je cha 55k vipi? 😂😂🫵

Chief-Mkwawa

View attachment 3641775
Bora wangebaki na Ile Ile Tu 20mbps, kuongeza speed halafu kulimit watu data kwenye fiber hakumake sense yoyote, kutaongeza Tu kelele.

Jambo zuri ni kwamba wengine nao wanasambaa Sana nje ya katikati ya jiji, soon watakimbiwa TTCL, advantage Yao Vs wengine imeondoka.
 
Mpaka nashangaa lengo lao lilikua nini sasa kuongeza speed na promo ya marking kuuubwa afu wana capp bandwidth dronedrake Hii imekuaje mpaka ndugu zako TTCL wameamua kukengeuka 😁
 
Mpaka nashangaa lengo lao lilikua nini sasa kuongeza speed na promo ya marking kuuubwa afu wana capp bandwidth dronedrake Hii imekuaje mpaka ndugu zako TTCL wameamua kukengeuka 😁
hawa wanapambana na wale unlicensed internet resellers
kitendo cha kuja na routers ambazo kubadili ssid/password mpaka uwaone wao nikajua kumekucha tayari
ujinga wa kuzuia ethernet ports zisifanye kazi ni adhabu inayojumuisha waliokuwemo na wasiokuwemo
wakapata fununu kwamba, kuna wanaounga mikrotik kwa router zao kwa njia ya "wifi repeating mode" naona ndiyo wakaongeza makali kwa FUP
 
Back
Top Bottom