Adsl pia ni ya kizamani mkuu ila ina unafuu compare na Satelite.
Unakumbuka zamani enzi za modem za 3.2mbps? Kipindi cha 3g unasubiria movie nusu saa idownload. Expect speed kama hii kwa adsl.
Yenyewe inatumia zile waya za shaba ambazo zamani tulitumia kwenye simu za mezani. Na ukiunga adsl unapewa na namba yako kabisa inayoanziwa na 0222 kama ya simu za mezani.
Fiber ni mziki mwengine ipo fast sana hasa ping, ni 1ms ama 2ms, sometime wakati unabrowse ni kama hutumii internet ukigusa tu inafunguka. Sema coverage yake kwa sasa ni ndogo sana ipo tu mjini katikati.
Hivyo mkuu nenda tawi la TTCL karibu na Nyumbani ulizia, kama Fiber ipo kwako unga hio 20mbps kwa 55,000 ni bei nzuri sana.
Kama haipo covered adsl ndio option iliobakia. Adsl naona kifurushi cha 25000 na 50000 vina value zaidi 4mbps na 8mbps. Mimi siamini kama adsl ya TTCL inaweza gonga 8mbps hivyo nimechukua cha 4mbps, unaweza jaribu cha 50000 ukaleta feedback.