Baada ya dakika 20 naye akajibu meseji
View attachment 2754571
Nikamjibu
View attachment 2754575
Nikamfahamisha kuwa kesho ambayo ndio leo nitafika ofisini kwao ili nipate uhakika zaidi
View attachment 2754576
Leo sasa kabla sijaondoka kwenda ofisini kwao nikapiga simu tena kwa surveyor ikaita lakini haikupokelewa.
Nimefika ofisini kwao nikamkuta mwenzake ambaye alikuja naye siku ya survey.
Nikamuuliza vipi mchakato umefikia wapi. Huyu akaniambia eneo langu connection ya B.O.Q imejaa hivyo wataalamu wapo katika mchakato wa kufunga zingine, zikikamilika watanijuza.
Nikamuuliza kuhusu uhakika wa siku ambayo hiyo process ya kufunga hiyo connection itakamilika.
Akaniambia yeye hawezi kujua kwasababu hilo jambo lipo nje ya uwezo wake.