Hapa umeongea ukweli kabisa, hawa mawakala mambo mengi hawajui, sisi user inawezekana tunajua mengi kuwashinda..
BTW line yangu ya kwanza ilizinguaga, ilikufa kabisa, nikamuita wakala aloniuzia, akaja.
Njia alizokuwa anatumia niliona ananipotezea muda tuu maana mambo yote alikuwa anategemea kuelekezwa na aliyekuwa anamuita "Leader" wake. Fanya hivi, fanya vilee lkn wapii line iligoma, kimsingi chip ilikuwa imekufa kabisa
Wakaniambia nika-swap, nikawauliza niki-swap itaendelea kubaki vilevile? Kifurushi changu nitakikuta au itabidi nianze upya kwa kulipia kingine. Hakuna aliyekuwa na jibu.
Mwisho wa siku niliswap ile chip ila ilibaki vilevile na kifurushi hivyo nikaendelea nilipoishia..