6OK kipande, kuna wamba wana unlock hiyo device gharama ya juu maximum ni 10$ sawa na 28,000 tu.
View attachment 3097704
Nilichokuja kugundua hata watanzania wengi wanaotangaza ku unlock hizi device sio kama hiyo kazi wanafanya wao.
Kuna mmoja nilimcheki baada ya kuona tangazo lake akanitajia bei 35K nikatulia.
Nikaingia YouTube kwenye channel ya muarabu mmoja nikamcheki WhatsApp akaniambia anafanya unlock kwa 8$ hapo ni baada ya kufanya utanzania yani kumshusha kwenye bei yake ya asili ambayo ni 10$
View attachment 3097705
Sasa huyu jamaa nikamuomba anioneshe uthibitisho wowote kufanya nimuamini kwasababu ya scam zimekuwa nyingi hususan ni huduma inafanywa baada ya malipo.
Jamaa alinitumia screenshot za chats za wateja zake kutoka taifa langu yani wabongo wenye code za +255
Akazi crop zile screenshot chats kwa kutoonesha full namba lakini moja ya chat katika zile screenshot ilikuwa ina dp ya yule jamaa aliyeniambia ana unlock kwa 35K.
Kwa hiyo nikagundua kuwa hawa wabongo waliowengi wanaosema wana unlock hizi device ni kama madalali tu ambao hawafanyi wao hizo kazi bali kuna mtu ndio wanayemtumia.