Vigogo na Watoto wa Vigogo wana mitaji lakini mbona hawajiajiri?

Na huyo :Richa" ni mtoto wa "kigogo" pia?

Itakuwa hujawaona watoto wa Kinondoni, umezowea kuwaona wa kigogo wenzako tu.

Vipi wewe, wanakupiga hao watoto wa kigogo?
Yaani Faiza, sisi wengine tumezaliwa kaskazini huko hatuwezi kutofautisha R na L sometimes.
 
Mkuu hawa wana jiajiri na bado wako kwenye hizo nafasi nyeti..

Kwa ufupi wanapiga zote zote kujiajir na kuajiriwa
 
Kwa uzoefu wangu hawa jamaa wana miradi mingi kuliko makabwela.

Angalia wamiliki wa sheli, mabasi ya mikoani, hisa kwenye makampuni makubwa, viwanda vya kati, wachimbaji/wafanyabiashara wa madini, wamiliki wa maroli, shule na vyuo binafsi,mashamba makubwa na makampuni ya ujenzi bila kusahau real estate business.

Hizo business zote wamejaa wanasiasa, viongozi wakubwa wa umma na mabalozi wetu. Lakini pamoja na kumiliki vyote hivyo hawaachi ajira zao. Kwa nini?

Simply kwa sababu zina maslahi makubwa na zina mianya ya kuiba pesa za umma au kufuja kwa kutumia madaraka yao ( kuchota ). Wanaishi bila wasiwasi na biashara zao nyingi zinaenda vema kwa kukwepa kodi na magumashi nyingi.

Wanaposema watoto wa masikini wajiajiri bila kuwa na mitaji ina maana hizi biashara za uchuuzi, kuwa machinga, au duka la mangi. Kama ni kilimo basi ni kile cha bustani.

Hata hivyo hakuna haja ya kulalamika maana bado jamii ya wajinga ni wengi Tanzania ambao hawaoni umuhimu wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Maana katiba iliyopo inaendelea kuwapa wenye nchi fursa nzuri na watoto wa masikini wataendelea kuisoma namba.
 
Nafasi wanazopiganiwa na baba zao serikalini ni zile za mishahara minono na ya upigaji pesa. Hizo kazi mtu kuongiza milion 10 kwa mwezi ni kawaida (salary plus wizi).

Sio hizo za halmashauri. Ndo tofauti iliopo
 
Nafasi wanazopiganiwa na baba zao serikalini ni zile za mishahara minono na ya upigaji pesa. Hizo kazi mtu kuongiza milion 10 kwa mwezi ni kawaida (salary plus wizi).

Sio hizo za halmashauri. Ndo tofauti iliopo
Aisee kumbe wanajua
 
Hili nalo neno Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…