mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Ndivyo wanavyoamini !Huenda ndio siri ya mafanikio Yao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndivyo wanavyoamini !Huenda ndio siri ya mafanikio Yao.
Econometrics 😆Yani ,unavyoandika utafikiri fundi, kumbe uli sup MTH 106 STATISTICS MPAKA THIRD ATTEMPT
Wachana na mawazo finyu ya wana ccm.Kwanza nikiri watoto wa vigogo wengi wamesoma sana na wana bidii sana kwenye masomo.
Zamani niliaminishwa vijijini kwamba watoto wa matajiri hawapendi shule na kwamba huwa wanafeli.
Baada ya kusogea mbele ki elimu nikahama mkoa niliokuwa naishi huko vijijini nilikutana na ulimwengu wa tofautu kabisa.
Watoto wa vigogo yaani RC, DC, DAS, Ma generali wa jeshi, Wakurugenzi wa Tasis za serikali kama BOT, NSSF, PSSF, TPDC, TANESCo, bila kusahau watoto wa wenyeviti na makatibu wa ccm ngazi mbali mbali Taifa, mkoa na wilaya niligundua wako serious sana na masomo na ni vichwa sana.
Wanajituma kusoma na wana sapoti nzuri kutoka kwa wazazi wao ikiwemo pesa na matumizi mengine ya kujikimu.
Ilikuwa ni jambo la kawaida mtoto wa kigogo kukuta ana akiba ya pesa kuanzia Laki moja kwenda mbele huku tukiwa Boarding school na kila kitu nakula hapo hapo.
Hali ile nilijua inawapa sana motisha watoto wao kusoma na kutokata tamaa. Na wengi waliongoza kwa ufaulu darasani. Ikitokea mtoto wa kabwela amefaulu kuwazidi basi inakuwa kwa uchache sana.
Richa ya hayo yoote bado linapokuja swala la ajira watoto wa vigogo wenye utajiri na mitaji hatuoni wakijiajiri badala yake Wazazi wao wanapigana vikumbo kuhakikisha watoto wao wanapata nafasi za ajira serikalini.
Majaji, wabunge na mawaziri ndio hivyo hivyo.
Huku wakiwambia watoto wa kabwela kuwa kuajiriwa ni umaskini na kujiajiri ndio mpango mzima.
Je tunapigwa?
Mkuu umeona wapi mtoto wa kigogo mwenye mtaji akijiajiri?Wachana na mawazo finyu ya wana ccm.
HahahsYani ,unavyoandika utafikiri fundi, kumbe uli sup MTH 106 STATISTICS MPAKA THIRD ATTEMPT
Wa vigogo kinachowatoa ni kusomea shule bora.Ila watoto hawa wengi wao SI vichwa.
Watoto vichwa(genius) ni wale wanaotokea familia za kawaida, tena kijijini.