Vigogo na Watoto wa Vigogo wana mitaji lakini mbona hawajiajiri?

Wanaambiwa na wazazi wao kuna pesa za bure za umma ukimaliza uje uibe
 
Mkuu Masomo siyo real life? Real life ni life la namna gani mkuu?
 
Kujiajiri kunahitaji akili na sio kubebwa.Mtaji bila akili ni kazi sifuri
 
Kwenye kujiajiri kunatumika akili sana na stress ni nyingi sana na pia kwenye kujiajiri Uwezekano wa kupata hasara ni mkubwa sana !!
Na ni lazima ujibane sana kufanya matanuzi !!
Unaonaje hapo ?! Utachagua pande gani uende ??! 😅🙏🙏
 
Wewe unausema ukweli ambao watu wengi hawausemi au hawaujui
 
Wanapambana wapate ajira seriaklini, wajenge connections, wapate experiences, ndio waje wajiajiri,
Yupo mtoto wa rais mstaafu, ni mbunge na waziri, na Ana kiwanda kikubwa cha vifaa vya ujenzi, Nondo, tiles nk,


Kujiajili sio swala rahisi kama kwenda kununua chips kuku, au kwenda kariakoo kununua simu ya tekno,
Na hapa nazungumzia biashara ya huduma na bidhaa, sio uchuuzi wa kufata mzigo china na kuja kuuza bongo, that is simple, kuna jamaa zangu tulifanya kazi, wote kipindi hicho,2002, Leo wengine wanakampuni za mambo ya engineering, solar, umeme, generators, car tracking,

Imewachukua miaka 10+kuweza kufikia hatua ya kufungua kampuni, kupata mtaji pesa,ujuzi na kazi za kufanya.
 
Kama kusingekuwa na selfishness watanzania wengi wangeweza kufanya hayo Kwa msaada wa serikali na kutoa ajira Kwa watu wengi, tatizo ni hawa hawa na vizazi vyao wanaogopa competition wanataka wao pekee waishi kifalme wengine wote wawe watwana...Ila nature ilivyo hii ni short lived, lazima kutatokea revolution
 
DC nae ni Tajiri??
Au Mwenyekiti wa Ccm Lindi nae tumuite Tajiri?..

Sometimes umasikini wetu hufanya yeyote Yule mwenye nafuu tumuombe Tajiri na kigogo...kumbe wao tofauti na wewe wala sio kubwa ..
Hakuna DC's wanaaopiga dili za magendo kama wa mipakani.Mimi nimewahi kuishi Tarime njia ya Sirari,wakubwa wanakula maisha Mkuu,rushwa nje nje.
Muulize RC Hapi kama ni rafiki yako atakuambia.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Mengine nimeambiwa na mengine nimeshuhudia......wako vizuri kwenye hustling za mafanikio.
Wachache sana,ata kwenye Elimu majority ni wazembe.Mimi nimesoma nao wengi English medium kama Watoto wa IGP Mahita walikuwa bure kabisa.
Ila wapo wanaojitambua wanapiga fresh tu!


Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kuna vitu viwili unachanganya, kuna watoto wa vigogo serikalini na viongozi na watoto wa matajiri, watoto wa matajiri ni watoto wa wafanyabiashara, Bakhresa, Mengi, Rostam, Subash Patel, Dewji.

DC, Katibu Mkuu wa Chama tawala, watumishi wa Umma wenye vyeo, watofautishe na wafanyabiashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…