Vijana 125 watelekezwa Singida baada ya kuahidiwa kazi za Q NET licha ya kutozwa kiasi cha fedha

Vijana 125 watelekezwa Singida baada ya kuahidiwa kazi za Q NET licha ya kutozwa kiasi cha fedha

Nchi ya ****** sana hii..hao qnet kila mara wameshasemwa ni matapeli ila naamin ni mradi wa mtu mkubwa serikalini ndio mana BAADA ya skendo za utapeli hua wanarudi tena kutapeli watu...na sijui kwanini watu wananchi hawaelewi au wamelogwa ..qnet ni mikundu na matapeli tu kama matapeli wengine ..
 
Kama hawawasikilizi wazazi wao na kuchukua ushauri kwanini wasizulumiwe miaka kama mitano imepita vijana waliachwa katika jumba Arusha huko wengine Dodoma lakini bado hawakomi acha wapate akili
 
Serikali wilayani Singida imewataka vijana wanaojihusisha na biashara ya Q-NET kuacha shughuli hiyo na kurejea makwao, kufuatia tuhuma za kulaghaiwa kwa ahadi za kupata malipo makubwa yasiyoendana na uhalisia.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, baada ya vijana takribani 125 kutoka mikoa 11 nchini kutiwa mbaroni kwa tuhuma zinazohusiana na shughuli hizo.

Gondwe amesema vijana hao wanaishi kwa makundi ya watu 30 hadi 50 katika nyumba moja ya kupanga.

Amewataka kurejea makwao ndani ya saa 24, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kuwashikilia viongozi wa shughuli hizo na kuwachukulia hatua stahiki ili kuzuia vijana wengine kushawishiwa kujiunga.

Kwa upande wao, baadhi ya vijana hao wamesema walijiunga na shughuli hizo baada ya kushawishiwa na marafiki zao.

Wamesema baada ya kufika Singida, wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya biashara ya mitishamba bila kupata malipo, huku wakitakiwa kuomba fedha kwa wazazi wao ili kuendelea na mafunzo hayo kwa ahadi ya kulipwa baadaye.

View: https://www.facebook.com/share/v/19xtjV692F/

wakulaumia ni CCM
 
Nchi ya kijinga sana hii
Nchi sio ya kijinga Bali watu wake ndio wajinga.

Hii issue ilishawahi tokea siku za nyuma Kwa mtindo huu huu wa kukusanya watu kwann viongozi wa Hilo eneo wanaruhusu? Au ndio mradi wa CCM?
 
Goodmorning....

Hapo mchana kweupe jua linachoma kama pasi, matapeli yanakusalimia kama mwanzo wa kukuingiza chaka...
 
Ukizaa mtoto omba apate akili yake binafsi tuu ya utambuzi wa maisha ya kila siku achana na nasaha zako na maonyo yako pekee...apate tuu akili za kujiongeza...
 
Inasikitisha sana aisee. Idadi ya wajinga nchini ni kubwa sana.
Halafu gentleman,
huenda kwasasa,
kufuata mkumbo ikawa ndio janga kubwa zaidi nchini, coz haiwezekani jambo la kitapeli kama hilo linazungumzwa mitandaoni daily but mtu kwa kujua kabisa anakwenda kutapeliwa na hashituki mpaka apigwe pesa kwanza.
Hii ni maajabu aise,

Ama kwa hakika,
mtu akikaribia kutapeliwa anakua mbishi mbaya sana aise gentleman 🐒
 
Serikali wilayani Singida imewataka vijana wanaojihusisha na biashara ya Q-NET kuacha shughuli hiyo na kurejea makwao, kufuatia tuhuma za kulaghaiwa kwa ahadi za kupata malipo makubwa yasiyoendana na uhalisia.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, baada ya vijana takribani 125 kutoka mikoa 11 nchini kutiwa mbaroni kwa tuhuma zinazohusiana na shughuli hizo.

Gondwe amesema vijana hao wanaishi kwa makundi ya watu 30 hadi 50 katika nyumba moja ya kupanga.

Amewataka kurejea makwao ndani ya saa 24, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kuwashikilia viongozi wa shughuli hizo na kuwachukulia hatua stahiki ili kuzuia vijana wengine kushawishiwa kujiunga.

Kwa upande wao, baadhi ya vijana hao wamesema walijiunga na shughuli hizo baada ya kushawishiwa na marafiki zao.

Wamesema baada ya kufika Singida, wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya biashara ya mitishamba bila kupata malipo, huku wakitakiwa kuomba fedha kwa wazazi wao ili kuendelea na mafunzo hayo kwa ahadi ya kulipwa baadaye.

View: https://www.facebook.com/share/v/19xtjV692F/

IMG_5110.jpeg

Utapeli ni ule ule. Jina tu ndo limebadilika .Hizi kampuni zinapata vipi usajili ?

Hao vijana 500 wangekua wamekusanywa kufanya project ya kilimo. Serikali ifanye tathmini namna ya kutumia nguvu kazi ya vijana.

Ikiendelea kuwaacha hivi matapeli wanawatumia.

Au basii.. serikali yenyewe haijali.
 
Maradhi, Ujinga, Umasikini.

Ujinga ni janga la taifa. Hii issue ni serious iangaliwe kwa jicho la tatu.. ujinga ujinga ujinga
 
Elimu kwa umma itolewe ili Gen Z waache kutapeliwa. Hawa Gen Z wakina Mwashambwa wanajifanya wajuaji wanaishia kutapeliwa. Waelezwe hakuna shortcut kwenye maisha na ukiitiwa fursa ujue wewe ndio fursa.
 
Yaani uweke laki moja na themanini urudishiwe dola laki sita,si wavumilie tu hiyo dola laki sita irudi,ni mapema mno nyie vijana kuweni wavumilivu.
 
Dah 😅😅😅 Hawa nao 2026 bado wanapigwa.
Kuna watu wapo juu wana ushawishi mkubwa sana.
Mdada Hanzuruni alikuwa meneja wa Nmb Mbeya akatumbuliwa na Magu,yupo pale anajisifia aliacha umeneja wa benki akajiunga na qnet kwasababu inalipa sana,watu wanamuamini kwa ushawishi huo
 
Dah 😅 Mbingu ngumu sana.
 
Back
Top Bottom