Vijana 125 watelekezwa Singida baada ya kuahidiwa kazi za Q NET licha ya kutozwa kiasi cha fedha

Good morning billionaire hata kama ni usiku hata kama ni mchana wao ni good morning

..ukileta watu watatu nao kila Mmoja wao akaleta watu watatu na wao wakawaleta watu watatu watuatu..unapanda unaendelea kupanda mpaka unajikuta ...una mahela MENGI baada ya muda MFUPI.
 
Serikali wilayani Singida imewataka vijana wanaojihusisha na biashara ya Q-NET kuacha shughuli hiyo na kurejea makwao, kufuatia tuhuma za kulaghaiwa kwa ahadi za kupata malipo makubwa yasiyoendana na uhalisia.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, baada ya vijana takribani 125 kutoka mikoa 11 nchini kutiwa mbaroni kwa tuhuma zinazohusiana na shughuli hizo.

Gondwe amesema vijana hao wanaishi kwa makundi ya watu 30 hadi 50 katika nyumba moja ya kupanga.

Amewataka kurejea makwao ndani ya saa 24, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kuwashikilia viongozi wa shughuli hizo na kuwachukulia hatua stahiki ili kuzuia vijana wengine kushawishiwa kujiunga.

Kwa upande wao, baadhi ya vijana hao wamesema walijiunga na shughuli hizo baada ya kushawishiwa na marafiki zao.

Wamesema baada ya kufika Singida, wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya biashara ya mitishamba bila kupata malipo, huku wakitakiwa kuomba fedha kwa wazazi wao ili kuendelea na mafunzo hayo kwa ahadi ya kulipwa baadaye.

View: https://www.facebook.com/share/v/19xtjV692F/

Hawa jamaa ni wajanja wanatafuta mtu unaemuamini au ndugu yako anakushawishi na lazima uamini kwanaana mtu anakuambia ni mtu wako wakaribu lazima uingie kwenye mfumo tu(kwenye 18)
 
Serikali wilayani Singida imewataka vijana wanaojihusisha na biashara ya Q-NET kuacha shughuli hiyo na kurejea makwao, kufuatia tuhuma za kulaghaiwa kwa ahadi za kupata malipo makubwa yasiyoendana na uhalisia.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, baada ya vijana takribani 125 kutoka mikoa 11 nchini kutiwa mbaroni kwa tuhuma zinazohusiana na shughuli hizo.

Gondwe amesema vijana hao wanaishi kwa makundi ya watu 30 hadi 50 katika nyumba moja ya kupanga.

Amewataka kurejea makwao ndani ya saa 24, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kuwashikilia viongozi wa shughuli hizo na kuwachukulia hatua stahiki ili kuzuia vijana wengine kushawishiwa kujiunga.

Kwa upande wao, baadhi ya vijana hao wamesema walijiunga na shughuli hizo baada ya kushawishiwa na marafiki zao.

Wamesema baada ya kufika Singida, wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya biashara ya mitishamba bila kupata malipo, huku wakitakiwa kuomba fedha kwa wazazi wao ili kuendelea na mafunzo hayo kwa ahadi ya kulipwa baadaye.

View: https://www.facebook.com/share/v/19xtjV692F/

Ukitaka kugombana na hao wajinga jaribu kuwasanua kuwa hapo mnatapeliwa, yaani hawakuelewi kabisa.

Sijui kwanini mtu anayetapeliwa anakuwa mgumu sana kusanuka. Halafu hapo utakuta ni wanaelimu nzuri tu. Acha watapeliwe
 
Back
Top Bottom