Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Huu ndio ujumbe wangu wa Jumapili kwa vijana wa Tanzania waliopewa nafasi za kuwa viongozi, Tafadhalini sana, tafadhalini jamani, madaraka ni dhamana ya muda mfupi mno, jitahidini kutenda haki kwa mujibu wa Katiba ya nchi, mkifanya hivyo hata mwisho wa madaraka yenu hamtaishi kwa mashaka na wala visasi havitakuja upande wenu.
Maandiko matakatifu yanasema hivi, nanukuu "AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU, AMFANYAYE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE NA MOYONI MWAKE AMEMWACHA BWANA" YEREMIA 17:5.
Hapa Mwenyezi Mungu anatuasa kwamba tukitenda kiburi kwa vile wako wanadamu wenye madaraka zaidi wanatulinda tutakuwa tunakosea sana, maana siku za mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke hapa duniani si nyingi sana, siku watakapoondoka duniani baada ya kutwaliwa tutachanganyikiwa.
Nakutakieni Jumapili njema na Kwaresma yenye baraka