Vijana, Kama Uwezo Upo Jengeni Nyumba za Kupangisha

Nina Room 11 daresalade ziko eneo zuri sana bandika bandua.

Pembeni Kuna nyumba inaiuzwa mzigo wa chap Sina kuivuta nishaurinini napate fund ziivute hii nyumba 35+m zinahitajika
 
Epuka assumptions. Hatujuani hapa.
 
Nina Room 11 daresalade ziko eneo zuri sana bandika bandua.

Pembeni Kuna nyumba inaiuzwa mzigo wa chap Sina kuivuta nishaurinini napate fund ziivute hii nyumba 35+m zinahitajika

Nyumba ya vyumba 11 ulijenga kwa bei gani mkuu?
Vipi kodi ni bei gani kwa mwezi kwa kila chumba kwa sehemu ilipo?

Hiyo inayouzwa kwa milioni 35 ina vyumba vingapi?
 
Ni wazo zuri kwamba una assets za kudumu lakini business return (ROI) yake inachukua miaka mingi sana...

Namna pekee ya kupata faida kutoka kwenye real estate ni kuhakikisha unapata faida per square meter...

Mtu anayepangisha jengo kibiashara kama fremu/kizimba ndio wanaongoza kupata faida zaidi, mathalani anaweza akawa anaingiza shilingi laki 3 kwa square meter 12, ilihali ukiwa na nyumba eneo hilo hilo unaingiza laki 3 kwa square meter 100 plus.

Hivyo watu wenye fremu, nyumba za kulala, watu wenye malls, wenye maeneo ya kupangisha ofisi n.k wana uwezo wa kupata faida maradufu kuliko wenye nyumba za makazi...
 
Huu ni ushauri kwa vijana wanaopata hela nyingi.

Sasa mtu anayepata hela nyingi sio level wa nyumba za kupangishs bro acha ushamba. Maana yake ana michongo mikubwa
 
Hapo kwenye fremu si kweli, labda kama ipo katikati ya mji,,,aisee frem anafaidika mpangaji,,
 
Hapo kwenye fremu si kweli, labda kama ipo katikati ya mji,,,aisee frem anafaidika mpangaji,,

Mawardat warda itakuwa sio kweli endapo kabla ya kujenga labda ulifuata mkumbo, biashara yeyote lazima izingatie kanuni ya demand and supply...

Mathalani maeneo yenye wanafunzi wengi, wazo la kujenga hosteli lina mashiko zaidi...maeneo prime kama Masaki n.k wazo la kuwa na nyumba ya makazi linalipa zaidi (square meter zile zile za mraba Masaki zinapangishwa kwa bei kubwa kuliko Mbagala kizuiani)...maeneo yenye wingi wa watu na mzunguko wa biashara, wazo la fremu ni zuri zaidi.

Hivyo lazima utafakari faida iletwayo na biashara ya ujenzi na wapi biashara hiyo imewekwa...
 
Changamoto nyumba inakula pesa nyingi hadi inakamilika na urudishaji wa GHARAMA ni WA taratibu. Mfano unajenga nyumba ya kupangisha Kwa GHARAMA ya milioni25 au zaidi halafu uipangishe Kwa laki mbili Kwa mwezi?itakuchukua miaka kumi kurudisha GHARAMA ndiyo uanze kupata faida.Kama unamtaji mkubwa kama milioni 150 na kuendelea Jenga lakini kama mtaji ni mdogo wekeza biashara zingine ambazo zinazalisha faida Kwa haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…