Vijana, Kama Uwezo Upo Jengeni Nyumba za Kupangisha

Sio assumptions Ni miaka nenda rudi unatutangazia ujenzi naona ndo umekamalizia unatamba kwenda vacation na million 2 kasoro .
Ha ha ha. Sawa. Ndio ninekamilisha ujenzi mkuu. Kwahio kesho nikisema vijana nunueni magari ndio nitakuwa nimenunua gari ya kwanza sio? Bado ni assumptions hatujuani. Jadili mada.
 
Changamoto nyumba inakula pesa nyingi hadi inakamilika na urudishaji wa GHARAMA ni WA taratibu. Mfano unajenga nyumba ya kupangisha Kwa GHARAMA ya milioni25 au zaidi halafu uipangishe Kwa laki mbili Kwa mwezi?itakuchukua miaka kumi kurudisha GHARAMA ndiyo uanze kupata faida.Kama unamtaji mkubwa kama milioni 150 na kuendelea Jenga lakini kama mtaji ni mdogo wekeza biashara zingine ambazo zinazalisha faida Kwa haraka.

Kuwa na pesa nyingi bado inakataa kimahesabu, kama milioni 25 tu inachukua miaka 10 kuirudisha je hiyo million 150 si itachukua miaka takribani 60 ndio irudi?
 
Hivi mnaposema pesa irudi,irudi kutoka wapi? Unapojenga umeiweka hela yako katika hilo jengo. Chochote unachoingiza ni faida hela yako ipo pale pale kwenye jengo na inaendelea kupanda thamani. Labda kama umekopa. Na mkopo una mahesabu yake.
Sio kama biashara ya nyanya lazima uziuze upate faida la sivyo zitaoza na mtaji kupotea.
 
Kiasi ulichowekeza kurudi
 
Mawardat warda itakuwa sio kweli endapo kabla ya kujenga labda ulifuata mkumbo, biashara yeyote lazima izingatie kanuni ya demand and supply...

Mathalani maeneo yenye wanafunzi wengi, wazo la kujenga hosteli lina mashiko zaidi...maeneo prime kama Masaki n.k wazo la kuwa na nyumba ya makazi linalipa zaidi (square meter zile zile za mraba Masaki zinapangishwa kwa bei kubwa kuliko Mbagala kizuiani)...maeneo yenye wingi wa watu na mzunguko wa biashara, wazo la fremu ni zuri zaidi.

Hivyo lazima utafakari faida iletwayo na biashara ya ujenzi na wapi biashara hiyo imewekwa...
Eeeh fremu Jenga sehemu ambayo Kuna mzunguko,, maana pembeni ya mji mafremu yamefungwa,mtu anapanga iliisha Kodi anapita hivi,,,,,,Bora ujenge ya kupangisha kuishi.
 
Ha ha ha. Sawa. Ndio ninekamilisha ujenzi mkuu. Kwahio kesho nikisema vijana nunueni magari ndio nitakuwa nimenunua gari ya kwanza sio? Bado ni assumptions hatujuani. Jadili mada.
Psychology tu mkuu inaonesha wewe ni mara yako ya kwanza kumiliki nyumba.
Ndio maana unafurahi tu kuiangalia na kuiongelea Kila saa Kila saa hapo mtu hawezi kukushauri chochote ,ili mradi unaiona roho yako inaridhika, with time akili itakukaa sawa utaanza kuwaza namna nyingine.
 
Sawa.
 
Changamoto nyumba inakula pesa nyingi hadi inakamilika na urudishaji wa GHARAMA ni WA taratibu. Mfano unajenga nyumba ya kupangisha Kwa GHARAMA ya milioni25 au zaidi halafu uipangishe Kwa laki mbili Kwa mwezi?itakuchukua miaka kumi kurudisha GHARAMA ndiyo uanze kupata faida.Kama unamtaji mkubwa kama milioni 150 na kuendelea Jenga lakini kama mtaji ni mdogo wekeza biashara zingine ambazo zinazalisha faida Kwa haraka.
Kaka kwaiyo iyo biashara ya million 150 inarud Kwa mda gan? Hebu jaribu biashara ya lodge vyumba 10 tu uone maajabu yake hichi kipindi Cha mambo ya likizo kinaleta pesa mnoo kama umejenga lodge Kwa million 100 na Kila siku unalaza laki hapo nimesemea tu je pesa yako million100 inarud mda gan?
Hujengi nyumba za kupangisha kupata hela hapo Kwa hapo hiyo ni Mali yako miaka nenda Rudi wewe na kizazi chako kama huyoona faida basi watoto wako watakula faida yako ni kitu kisicho Isha wa kuharibika ovyo ovyo kipo na pesa inaingia Kila mwez au Kila siku Kwa lodge
 
Psychology tu mkuu inaonesha wewe ni mara yako ya kwanza kumiliki nyumba.
Ndio maana unafurahi tu kuiangalia na kuiongelea Kila saa Kila saa hapo mtu hawezi kukushauri chochote ,ili mradi unaiona roho yako inaridhika, with time akili itakukaa sawa utaanza kuwaza namna nyingine.
Mwanetu unakitu natamani kupata nondo kutoka kwako. Nyumba na nyumba ya kupangisha sio ya muhimu kivile ni vile tu psychological tunairate na vitu vya ovyo kama kununua magari na starehe. Kweli nyumba ukiilinganisha na ivyovitu aliejenga nyumba anaonekana anaakili kubwa.
 
Nyie kwanini msiende mkafunguq thread kujadili huvyo vitu vya maana na muhimu kuliko nyumba? Thread hii waachieni wanaoona nyumba ni kitu muhimu. Hapa nawashauri vijana siio nyinyi matajiri wa JF.
 
Acha hizo boss, Eti matajiri wa JF daah, Tunashauriana na kuboresha mawazo ili tujikwamue usitufukuze ukichalenjiwa kidogo.
 
Haya hongera sana mkuu sote tutajitahidi kujenga na kupangisha kama wewe lakini hatuwezi kukufikia mkuu yaani wewe ni mwamba kwelikweli hongera sana sana chief.
Acha utoto jikite kwenye mada.
 
Back
Top Bottom