Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Home shopping center wamesilimu sasa wanajiita ocean nini sijui na chawa wao Mwijaku.Ndiyo maana nimempatia series moja inaitwa the Gentlemen. Inaonyesha jinsi matajiri wanavyoishi na kuendesha biashara zao nje na vile jamii inavyojua.
Pia inaonyesha namna gani ukileta magumashi wanavyokupoteza bila kusita.
Kwenye biashara watu wanalinda jina/uamnifu na Kingdom yake. Huwezi ukaleta ujuaji kwenye kimojawapo halafu wakakuacha.
Mfano mzuri kipindi cha JK: Kampuni moja ya clearing and forwarding kwa ghafla tu ilikuwa juu kuliko kampuni nyengine. Walianzisha na ofisi yao China hivyo ikawa inawadaka wafanyabiashara wa Tanzania hukohuko na huku wana kampuni yao.
Matokeo kampuni nyengine zikawa zinakosa kazi na zinakufa. Kilochotokea Mkurugenzi mtendaji wa hiyo kampuni siku yupo Kariakoo kwa ghalfa mtu kamgusa nyuma kwenye bega. Ile kugeuka tu kamwagiwa tindikali usoni. Za chini chini zikawa zinasemwa kwamba wafanyabiashara wenzake waliona watakufa njaa haiwezekani mtu mmoja atawale biashara nzima wao watakula wapi!
Hivyo biashara zina umafia sana chini ya kapeti. Watu wapo serious na kazi zao. Watu wanachukua mikopo na wakati mwengine pesa wanazipata kwa njia zisizo halali halafu uzingue! Wanakupoteza.