Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Kariakoo 90 % biashara inatembea Kwa uaminifu , ili uuze mzigo kariakoo lazima uhusishe watu wengi sana na sharing ni kubwa , mawinga ndo catalyst ya biashara kariakoo Ila nguzo Yao kuu ni uaminifu , sasa njoo na tamaa zako uone , unakamuliwa kinyesi live live
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kariakoo 90 % biashara inatembea Kwa uaminifu , ili uuze mzigo kariakoo lazima uhusishe watu wengi sana na sharing ni kubwa , mawinga ndo catalyst ya biashara kariakoo Ila nguzo Yao kuu ni uaminifu , sasa njoo na tamaa zako uone , unakamuliwa kinyesi live live
Wenye tamaa huwa wanapakwa Kimbo 😂😂😂
 
Wengi wanaochangia wamemung'unya sana maneno kiasi asiyejua kinachoendelea hapati clue ya yanayotokea,vijana wanaopotea Kariakoo ni upande wa vitu kama simu laptop na tv na vitu mfanano wa hivyo pamoja na spare za magari.

Mimi nafanya biashara ya spare za magari,nyuma miaka saba nikiuza used kwanza Kariakoo kisha Ilala kule Lindi St so nikizungumza kwa upande huo nawajua vijana pamoja na watu wazima 11 wamepotea toka 2022 hadi leo hawajulikani walipo wa mwisho kwa upande huu walipotea wawili kwa pamoja mwaka jana mwezi wa tano na wote miaka ya nyuma wakati nafanya used walikuwa wanajihusisha sana na kununua vitu vilovyokuwa vikiibiwa kwenye magari ya watu wenyewe wakiita ”full",yaani gari inavunjwa kioo wanatoa lock wanachukua kuanzia dashboard show p/window switch radio side mirrors headrest nje wanang’oa taa zote bumpers nyuma na mbele kama mmiliki alisahau chochote cha thamani wanabeba so hawa jamaa walikuwa wanakaa pale mnada wa spare ulioungua moto nyuma ya Big Born p/station.

Jamaa walikuwa wanakula na askari wa Msimbazi na Central wakati fulani Mambosasa akiwa mkuu wa police Dar akalivalia njuga kwa kuwapa kitu kama offer (maana walikuwa wanajulikana kote police Msimbazi Stakishari Central Mabatini kwamba ndiyo wanaodhamini biashara hiyo hata picha zao zilibandikwa kutani) kwamba kuanzia pale hawana kesi ila wakiri kuacha mara moja mchezo huo kwani option iliyokuwa ifanyike baada ya kudhihirika wanaendelea na kazi hiyo ni kupotezwa moja kwa moja na kwamba jeshi la polisi halitakuwa na muda wa kwenda kutoa maelezo mahakamani,kilichoendelea wanakijua wenyewe baadae walipovunja hicho kiapo ndiyo wakapotea.

Baada ya hii ambush ndiyo matokeo tunayoyaona sasa wizi ule umepungua kama siyo kuisha kabisa nadhani hata Agrey baada ya wale watano kupotezwa kuna mabadiliko.
Hapa ndo nimeelewa sasa, Lol
 
Na ndiyo maana hata maduka ya spare used pale Kariakoo yamehamia Ilala wengine tumebadilika kuingia kwenye spea mpya kwa sababu wakati huo ilikuwa mtu akishaibiwa anaambiwa nenda Kariakoo ndiko wanakouza spare za wizi (wakimaanisha hapo kwenye mnada wa spare) na siyo kila mtu alikuwa anapajua so anajikuta ameingia Kariakoo lakini hajui aanzie wapi.

Sisi wenye maduka tulikuwa tukimkamata tunampina temper yake tukimuona mwepesi tunamuunganisha na wanaonunua vitu vya wizi vyake vikiwepo anafungiwa sisi tunakula comission na ndiyo kisa cha kufahamiana na hao niliosema wamepotezwa,alipoingia Magufuli ndiyo aliwa-push watu kufanya kazi na matokeo ndiyo hayo na leo Kariakoo maduka yote ya used yamefungwa na majuzi ule mnada ulipoungua nao ilibidi uhame lakini wanachama wake wakakomaa.
Mkuu story yako ni very interesting yaan umefunguka vizuri sana kuna mengine wengi tulikua hatuyajui kwa hio Jamaa wote waliokua wanaiba spea za Magari sasa hivi hawapo tena wamepotezwa wote?
 
Back
Top Bottom