Vijana kufanya maandamano kumuunga mkono Rais Samia kuelekea 2025

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Vijana wanne kwa kila wilaya wameandaliwa kufanya maandamano Mkoani Dodoma baada ya mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM.

Maandamano hayo yatakuwa ya kuonyesha vijana wanamuunga mkono Mama Samia awe mgombea pekee wa CCM Mwaka 2025.

Pia vijana hao watatoa tamko kali sana kwa wanaompinga Mama Samia kama kina Dr. Bashiru n.k.

Hivyo nimewapa taarifa mapema mnunue popcorn kusubiri hiyo movie hapo tarehe 28 November 2022.

Kazi Iendelee.

Pi
 
Hahahahaha?najuta kuzaliwa inch hii
 
Haya maigizo yamefikia mwisho wake,wayaandae maandamano ,waandae na medias,mapicha kibao,headelines kwenye magazeti yote lakini cha mtema kuni wanacho
 
Haya mambo yanafaa sana kwa nchi za kikomunist..nashauri katiba mpya itambua nchi yetu kuwa niya kikomunist na chama kiwe kimoja tu.

Tofauti na hapo yanayoendelea hapa nchini ni ujinga na upuuzi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mama ajiepushe na njia hizi za uchawa watu hawazipendi asiposikiliza sauti hizi atanyolewa na wembe uleule uliomnyoa hayati ; ccm siku zote ni genge la wanafiki na uislamu wa mama hautaki hizo mambo!
 
Nawaunga mkono, ila Dr. Bashiru hajampinga Mama, bali amekosoa mambo ya uchawa wa kuupiga mwingi.

Kuhusu 2025 wengi tunaunga mkono Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Ila pia angalizo kama hili, Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! lisipuuzwe!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…