Vijana Kuweni na Busara hata Kidogo

Vijana Kuweni na Busara hata Kidogo

Sifurahishwi na majibu yeyote yenye shabaha ya kutweza utu wa mtu bila kuangalia age ila najaribu tu kufikiria nje ya box katika mazingira ya huku mtaani.

Mtaani hususan huku uswahilini tuna wazee wengi wanaopenda usela, yani wazee vijana wenye habit zote za ujana na wanaopenda kujichanganya na vijana.

Wazee wa aina hiyo sio rahisi kuwaona waki react negative kwa kupewa aina hiyo ya maneno na kijana.

Na hata wao pia unakuta ni watumiaji wazuri wa aina hiyo ya maneno.

Mfano ukipita kwenye vilinge vya ma draft utakutana na wazee wengi hapo vijiweni ambao kwa mionekano yao na sura zao utawaona wana busara lakini wakianza kuongea wakiwa wamekubana kwenye mchezo wa draft ndio utajua kuwa wahuni nao wanazeeka.

Kwa hiyo unaweza ukam-judge jamaa kwa sauti yake na lugha aliyoitumia kwa Mzee lakini usijue ya upande wa pili kwasababu sauti yake hujaisikia ni aina ya kauli gani aliyoitoa huyo Mzee mpaka huyo kijana kufikia kusema hivyo.
 
Jana jioni nilikuwa nafanya mazoezi(jogging) nikapita barabara moja kuna ghorofa linajengwa.

Nikasikia kijana mmoja (27-30yr) anafoka na kutukana kwenye simu.
'WEWE MZEE SIKU YA PILI LEO NAFIKA HAPA UMEACHA LINDO. HUO UZEE WAKO MIAKA 70 ISIWE KIGEZO KUTUSUMBUA. KAMA ULITUMIA HELA ZAKO VIBAYA UJANANI USITULETEE... Duh nilishtuka sana nikaishia zangu.

Aisee inawezekana kweli mzee kakosea ila kuna njia nzuri ya kuongea na mtu mzima au mfanyakazi wako na sio lugha kama hizo. Kijana mdogo namna ile kumtukana mzee ambae anaweza kuwa baba au babu yake si sawa. Kuna laana nyingine za kujitakia. Vijana kuweni na busara.
Hatari, ila kijana yupo kazini na hataki mazoea na inaonesha ni wazi hakumuajiri kwa kumuonea huruma ila alimuajiri kwakua alimuamini anaweza kupiga kazi vizuri.
 
Leo kidogo nimetembezee mzee wa miaka 65 kipigo maana Sasa nimevumilia nimeshindwa .
Iko hivi aliniuzia tofali elfu nne ,wakati nazibeba akanimbembeleza kuwa aisee naomba kazi niwe fundi mkuu ,dah ngoja kwanza nipumzike nitamalizia nimejihisi hasira tena kaka
Mkuu achana nae kiustaarabu tu. Umri wa huyo mzee ukimgusa utajitafutia murder case uiache familia yako kwenye matatizo.
 
Mkuu achana nae kiustaarabu tu. Umri wa huyo mzee ukimgusa utajitafutia murder case uiache familia yako kwenye matatizo.
Ningekuwa na namba yako Kaka ningekutumia alichonifanyia site alafu namwambia anacheka eti anakumbushia kipindi anaanza ufundi Ila pia mafundi hawajawahi kula hata Mia anakula yeye mwenyewe .

Finally ananitishia maisha huyu mzee
 
Sifurahishwi na majibu yeyote yenye shabaha ya kutweza utu wa mtu bila kuangalia age ila najaribu tu kufikiria nje ya box katika mazingira ya huku mtaani.

Mtaani hususan huku uswahilini tuna wazee wengi wanaopenda usela, yani wazee vijana wenye habit zote za ujana na wanaopenda kujichanganya na vijana.

Wazee wa aina hiyo sio rahisi kuwaona waki react negative kwa kupewa aina hiyo ya maneno na kijana.

Na hata wao pia unakuta ni watumiaji wazuri wa aina hiyo ya maneno.

Mfano ukipita kwenye vilinge vya ma draft utakutana na wazee wengi hapo vijiweni ambao kwa mionekano yao na sura zao utawaona wana busara lakini wakianza kuongea wakiwa wamekubana kwenye mchezo wa draft ndio utajua kuwa wahuni nao wanazeeka.

Kwa hiyo unaweza ukam-judge jamaa kwa sauti yake na lugha aliyoitumia kwa Mzee lakini usijue ya upande wa pili kwasababu sauti yake hujaisikia ni aina ya kauli gani aliyoitoa huyo Mzee mpaka huyo kijana kufikia kusema hivyo.
Mkuu makuzi yangu nimefundishwa namna ya kuongea na wakubwa,hasa wazee, I'm not judging. Ila busara kidogo haiumizi.
 
Back
Top Bottom