Vijana mkipata nafasi ya kuji attach kwenye royal family, Usirudi nyuma

Mpaka kujiattach lazima nawewe uwe na kitu kinachoweza kukuweka hapo, kuna sehemu ukiji-position atajishtukia mwenyewe kama huna kitu cha ku contribute. Inasemekana mwamba katoa 143.9B kama mahari, sasa kama huna kitu huwezi fika high table.

We know, "fake it till you make it really" kuna vitu vinatokea accidentally tu, na mara nyingi demu/huyo mwanamke awe attracted nawewe. And not otherwise
 
Umeongea ukweli. Daima yaangalie mahusiano katika jicho la kibiashara. Hili suala wanawake wameli-master. Wanaume ndio tunajifanya tuna unconditional love.

Umemsahau jux pia. Jamaa kumuoa Priscilla bila shaka alilenga kuingia kwenye soko la Nigeria.
 
Maada ya mleta maada ni nzuri ila Kuna vitu havijui

Kijana aliyeoa kwa mwinyi hakubalisha dini Bali walifunga ndoa kanisani tena st Joseph na yule binti wa mwinyi hakuwa mwisilam Bali alikuwa mkristo kwa dini ya mama yake
 
"...Oa binti anayetoka kwenye famila ambayo iko chini ukilinganisha na familia yenu...", by Eli Cohen.
🔥🔥🔥

HAKUNA UBISHI HAPA .

UNAPOOA DEMU ALIE CHINI KIMAISHA YAKO NA FAMILIA YAKO ANAKUWA SUBMISSIVE KWAKO NA ILI NDOA IWE ITULIE LAZIMA MMOJA AWE MASTER

SAASA NGOJA UJICHANGANYE UOE DEMU KWAO WANA HARRIER ALAFU ANA MAKEBO MAKUBWA NDIO UTAJUA HAUJUI😁😁
 
Unamaanisha wanaume wanatakiwa kudanga/kuishi na mentality ya kudanga ?

Mara nyingi wavulana wanokimbilia kitonga cha maisha kwa wanawake waliotoka familia zenye uwezo wanaishia kuangukia pua (kukosa Uhuru WA Uanaume)

Mwanaume anatakiwa kuwa huru kabla ya kuingia kwenye mahusiano, wakati na baada.

Usione vinaelea vimeundwa.

ndo hii unakuta mtu anakosa Uhuru kwenye mahusiano yake na kuishia kuishi kwenye mfumo wa utaki utataka. Kwa ufupi wapo wavulana hawana Uhuru kwenye mahusiano yao Kwa sababu ya kutanguliza mihemko ya njaa. unakuta mvulana anapangiwa akae wapi, aishi wapi, aonge nini, ale nini, anywe nini sometime hata maamuzi yale ya kawaida kabisa anapangiwa na familia ya mke wake. It's crazy.

Simpangii mtu, lakini Uhuru wa mwanaume ni kitu no.1 kwenye mahusiano yoyote. Mwanaume ndo anatakiwa kua na kauli ya mwisho kwenye mahusiano yake.
 
Acha hizo mambo...
Ndoa ni kitu ingine.

Kuna jamaa yangu wameoa huko ila wanaishi kama kondoo...

Wanaume tunapenda uhuru...

Uhuru wako ni bora kuliko mafanikio lukuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…