Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Nimejifunza kitu ila sina nafasi tena mimi umri ushapita but naitamani sana ya 3 mimi nilipata ya 6 mkuu but still nawaza kwann sikumake wonders?
Hakuna asiyetamani one ya tatu sema tu ndio vile uwezo unatofoutiana kati yetu.....

So bwana CCNP ni ruksa kufurahia misonge yake Mkuu nashangaa watu kwanini wanamkosoa ingawa najua fika kila mtu moyoni alikuwa anatamani kupata one ya saba o level.... one ya tatu advance na chuo kutoka na GPA ya nguvu.....

Kufaulu kwa maksi kubwa kuna raha yake asikwambie mtu....
 
Raia ambazo hazikuwa na akili za darasani zimepovuka sana kwenye huu uzi.

Sasa sijui watoto wao hawajawapeleka shule au hawatarajii wafaulu sana elimu ya darasani ili wawafundishe elimu ya kitaa watusue maisha.
 
Jamaa ana point kweli ila ana majivuno mengi.

Sijawahi kuona mwanaume msomi anajisifia hata siku, labda Jerry Muro.
 
Kuna jamaa namjua alimaliza na 1st class with distinction BSc; ila jamaa poa sana yupo mechanical eng pale mlimani ni DR.

Tulianza kumwita engineer tukiwa form II pale Moshi Tech baada ya kufumua mtihani wa form II averange ya 86 masomo yote 11 mabanda tupu . Form four akapiga 7 mabanda 9 yote hadi bible knowledge. Akaenda Dar Tech record zake hakuna aliyevuja; akaenda mlimani ikawa balaa tupu.
.

Jamaa yupo poa sana hana mineno mingiii... naanza kupata wasiwasi na huyu msomi wetu.
 
Mtamfanya ahamie Kenya Talk kwa maswali haya maana ni magumu kweli kweli .Ila akikujibu jibu sahihi usikose kunikumbuka nikuje kusoma.
 
Wabongo bwn japa wako bize wanakandia mtu aliefauluu wkt kila mtu anapeleka mtoto shule

Elimu ndo urithi mengine ataamua akiwa mkubwa

Hongera mkuu...technique zako shuleni kama zangu kwa kiasi kikubwa
Sijawahi soma tuition,wala usiku wa manane...

Ugonjwa wa taifa hesabu ni somo la kusolve maswali kila siku utapata A bila ubishi
Mzazi chukua hilo litamsaidia mwanao

Himizeni watoto kupenda shule na other life skills at par..
 
Mkuu watoto wako usiwapeleke shule. Waishie darasa la 7 then uwape Elimu na Skills za mtaa
 
Sorry ,amegundua nini mpka sasa?
 
Hiyo ndio shida ya wengi wao. Kuna mmoja type kama yake nilikutana naye Mkoa mkoja (jina kapuni) katika kambi ya jeshi ni mlevi balaa basi story zake bar akiwa kalewa ni hizi hizi zinafanana na za huyu jamaa.

,..Mara alikuwa TO, mara alipata highest GPA ever kutokea Tz ktk kozi ya sayansi aliiyokuwa anasomea, mara the youngest Senior lecturer kuajiriwa ktk chuo kikuu kimoja nchini ( jina kapuni), mara nina nyota 3 jeshini, na bla bla nyingine nyingi tu… ila sasa ukimuangalia utamhurumia jinsi alivyochakaa kwa sababu ya ulevi. Na sio huyo tu, nina mifano mingi ya kweli ya watu type hii, ila kwa leo huu mmoja unatosha.

In short ni kwamba, type ya watu kama hawa ambao tunasema wana uwezo mkubwa kupita average people ni kuwa wana tabia ya ku over-think on problems (kutumia akili kubwa sana kufikiria changamoto zinazowakumba katika maisha yao), kitu ambacho kina cause their own anxieties to raise above normal ( kuwafanya wapaniki kupita kiasi) ambapo mwisho wa siku hupelekea kuwa depressed (kupata msongo wa mawazo) ,especially pale waanaposhindwa kusolve the real problems they face in life.

Kama mtaalam wa mambo ya afya, siwezi kushangaa kusikia majivuno ya mleta mada kwani naelewa yupo kwenye stage gani na endapo asipobadili mtazamo wake basi hapana shaka hali inaweza kuwa worst zaidi hata ya huyo mjeda.
 
We acha mkuu hao wanaoponda ni vilaza tupu
 
Usisite kunitafuta mapema kabla hizo symptoms n signs zako za clinical depression hazijawa worst tukakupoteza mkuu. Wala sikutishi mkuu, ila Trust me, i know nachokisema.
 
huyo jamaa anaitwa nani boss ...usikute ndo mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…