Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Nashindwa kuwaambia jinsi nilivyojikatia tamaa kiasi cha kuwa kichaa.

Ila ninachoweza kuwaambia tu vijana wenzangu tuacheni kubeti kwa malengo kwamba tunapata pesa huko haraka haraka.

Fikiria nimefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 8, nikafukuzwa kazi nikaenda NSSF nikachukua milion 7.5 niliyokuwa nakatwa alafu yote nimeimaliza kwenye kindege cha aviator ndani ya siku 5 tu.

Nahisi kuna roho flani iliniongoza kwa sababu kwa akili ya kawaida najiona siyo mimi.

Lengo ilikuwa kubetia elfu 50 kama mtaji wa kubetia lakini kilichofata ni kupoteza milion 7.5 zote bila kubaki hata mia ndani ya siku 5 tu.

Hapa nilipo I wish hata nijitoe roho tu maana sijui ni wapi naanzia maisha tena pesa yote nishaipoteza kwenye uraibu wa kamari.

Kila nikiwaza nna miaka 30, sijaoa, sina biashara yoyote niliyoisimamisha kunilinda, sina maisha, kwa kifupi hiyo milion 7.5 nilitegemea ndiyo niingie nayo mtaani inilinde.

Lakini shetani kanikamata na kunikanda kisawa sawa.

Najiona mjinga wa kiwango cha Phd ndiyo maana nimejiita Zero Brainer, sina wa kumlaumu ila tujiepushe sana na uraibu hasa wa kubeti.

Mimi naweza nikafa leo ila sitaki vijana wenzangu yaje yawakute yaliyonikuta mimi sasahivi.

Mimi hali nnayopitia sasa kwa sababu ya kubeti nakosa maneno ya kuwaelezea ila siku nikifa mjua KINDEGE cha AVIATOR kwenye kampuni ya kubeti ya SPORTYBET kimesababisha kifo changu .
Acha uongo
 
Tupige forex
Kuna jamaa yangu kwa sasa hana maisha sababu ya forex..hadi familia imesambaratika. Alijifunza forex mda mrefu na akaijua, kazini walipomzingua akawapiga chini akalamba na nssf yake kwa kuhonga..akapeleka kwenye forex akapambana kama 3 years. Saizi ndio kaanza kurudi kawaida japo hana kitu anapiga mizinga tu..na baada ya jaribio la kutaka kujiua
 
Ndo maana ukaitwa zero brain sheikh

Mi majuzi niligombana na wife, nikachepuka kwa kitoto kina neema za allah kama zote, baada ya kuzoeana nikakapangia mahali ukiweka Kodi na vitu vyake vya ndani na ukijumlisha kaduka nilichomfungulia pale pale maana Kuna frame kwa nje haizidi 5M, yaani ni kama nimeoa mke wa pili kwa 5M na Kila siku napata Huduma ndo niende home.... Au naweza kuweka kambi hapo hata wiki kwa safari za kufata mizigo ya biashara za uongo

Nikiskia vijana mnapoteza 5M nahuzunika sana, kama unabeti beti hata buku tu aisee, m5 ukienda dar uswahilini huko unavuta wake watatu utakatikiwa mpaka ukimbie Jiji
...Kwa hiyo na Wewe Mkuu umebetia Milioni 5 Yako kwenye Mchepuko ? Mchepuko ambao Ukienda Home kulala na Mkeo na Mchepuko wako nao Unalalana Mchepuko wake ? Unalijua hili ??..
 
Muda muda muda muda.

Napata tumaini kupitia wewe kwa sababu umeamua kuishi kwenye hisia za maumivu yangu.

Ila Baba muda plus rasilimali ndiyo changamoto.

Imagine mwanaume 30 years single, economically kwa sasa niko zero, job opportunity zero, rasilimali ya kuanza nayo ili niinuke upya nijitetee ni zero.

Nilipata opporrunity ya kutokea (hiyo 7 milion) lakini nika lose the chance.

Ama kweli hakuna rangi nitaacha kuona kama wadau wanavyosema.

Kila nikiwaza nilicho kipoteza nahisi moto unaniunguza tumboni.

I feel more than hell.

Bora basi ningepoteza 7 milion lakini nna kazi ya kuingiza chochote kwa mwezi, nako hamna.

Ningepoteza basi seven milion lakini nna rasilimali ya kuuza nianze upya, nako hamna zaidi ya hii samsung galaxy A 14.

Yaana mimi najiona kabisa ni marehemu anaesogeza siku tu hapa
...Mkuu, Milioni 7 kununua Hata Kaboda boda ka kukuingizia japo Laki Moja Kila Wiki ?...
 
Kuna jamaa yangu kwa sasa hana maisha sababu ya forex..hadi familia imesambaratika. Alijifunza forex mda mrefu na akaijua, kazini walipomzingua akawapiga chini akalamba na nssf yake kwa kuhonga..akapeleka kwenye forex akapambana kama 3 years. Saizi ndio kaanza kurudi kawaida japo hana kitu anapiga mizinga tu..na baada ya jaribio la kutaka kujiua
Wazee wa forex nao wanapigwaga sana.

Nadhani kwemye forex nayo tuanze kuiangalia kama ni kamari pia..
 
Nashindwa kuwaambia jinsi nilivyojikatia tamaa kiasi cha kuwa kichaa.

Ila ninachoweza kuwaambia tu vijana wenzangu tuacheni kubeti kwa malengo kwamba tunapata pesa huko haraka haraka.

Fikiria nimefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 8, nikafukuzwa kazi nikaenda NSSF nikachukua milion 7.5 niliyokuwa nakatwa alafu yote nimeimaliza kwenye kindege cha aviator ndani ya siku 5 tu.

Nahisi kuna roho flani iliniongoza kwa sababu kwa akili ya kawaida najiona siyo mimi.

Lengo ilikuwa kubetia elfu 50 kama mtaji wa kubetia lakini kilichofata ni kupoteza milion 7.5 zote bila kubaki hata mia ndani ya siku 5 tu.

Hapa nilipo I wish hata nijitoe roho tu maana sijui ni wapi naanzia maisha tena pesa yote nishaipoteza kwenye uraibu wa kamari.

Kila nikiwaza nna miaka 30, sijaoa, sina biashara yoyote niliyoisimamisha kunilinda, sina maisha, kwa kifupi hiyo milion 7.5 nilitegemea ndiyo niingie nayo mtaani inilinde.

Lakini shetani kanikamata na kunikanda kisawa sawa.

Najiona mjinga wa kiwango cha Phd ndiyo maana nimejiita Zero Brainer, sina wa kumlaumu ila tujiepushe sana na uraibu hasa wa kubeti.

Mimi naweza nikafa leo ila sitaki vijana wenzangu yaje yawakute yaliyonikuta mimi sasahivi.

Mimi hali nnayopitia sasa kwa sababu ya kubeti nakosa maneno ya kuwaelezea ila siku nikifa mjua KINDEGE cha AVIATOR kwenye kampuni ya kubeti ya SPORTYBET kimesababisha kifo changu .
Na licence ya urubani hujapata 😂😂
 
Fanya mpango tuipate hii nakupa laki tano

Screenshot_2024-12-10-20-51-19-236_nssf.nssftaarifa-edit.jpg
 
Back
Top Bottom