Mussa Ramadhani Mussa
Member
- Jul 30, 2024
- 29
- 59
Habari zenu wakuu,
Nipo hapa kuelezea Kero inayotupata Wananchi kutoka kwa vijana wa KIMASAI jijini Arusha.
Vijana Hawa wamekuwa na Tabia ya kupiga, kudhalilisha, kunyanyasa na kutweza utu wa watu kila WAPITAPO kwa makundi barabarani.
Juzi walimpiga bodaboda maeneo ya ofisi za Halmashauri ya wilaya Arumeru (Sekei) mpaka wakamjeruhi. Na siku mbili nyuma walimpiga kinyozi mmoja kwa fimbo zao sehemu ya jicho mpaka jamaa alikaribia kupoteza jicho lake maana ameumizwa sana.
Nimeskia pia juzi Kati hapa walimpiga kijana mmoja maeneo ya Kijenge nusu wamuue.
Nimejaribu kufuatilia lengo la wao kupita barabarani kwa makundi (idadi ya vijana 200 au 300 hivi) nikaambiwa kuwa wanafanya mambo ya kimila (mfano wa jando na unyago wa KIMASAI) ila sasa naona jamaa wamevuka mipaka maana wamekuwa hatari na hata wakipita barabarani hawataki mtu Mwingine akatize vinginevyo wanamshambulia bila huruma Wala kujali usalama wake.
Nimeona nilete Kero hii maana naona inazidi kushamiri na kuonekana ya kawaida na mamlaka ziko kimya haziwachukulii hatua sasa nashindwa kuelewa iwapo Hawa vijana Wana mandate ya kupiga watu ovyo.
Nawasilisha!