Vijana wa Kiume badilikeni

hata michongo yenyewe watakupa Kwanza mpaka wakudiscuss Kwanza Kama ni nimchongo watakupa kwa kuona kuwa unadhiki.
 
Kuna hili kundi ambalo pia linaonekana ni super women! Kumbe bure tu wanakaa kwenye vifremu wanapiga mizinga wabustiwe kodi na mtaji deile! Danga akiamsha unashangaa tu mtu biashara imemshinda😂
 
Mkuu tatizo lipo inawezekana uwasilishaji wake ukawa namapungufu lakini wadogo zetu wamekwama
 

Hili unalolisema lina ukweli mkubwa tu. Tatizo sisi tuna tabia ya kudharau aina fulani fulani za kazi na kuziona kama ni kazi za watu fulani mf wasiosoma.

Mfano kwa nchi zilizoendelea, ni kawaida kabisa kukuta kijana lets say hawa wanaosoma vyuoni, kipindi cha likizo anaweza kuomba kazi kwenye mgahawa, bar, supermarket nk na anakua anafanya kwa masaa fulani anaingiza kipato. Hii inamjenga hata siku akimaliza chuo hakosi cha kufanya na kila mtu anaheshimu kazi ya mwenzake.

Sasa njoo hapa kwetu. Kijana wa chuo au aliemaliza chuo hata bar ya baba yake hawezi kukaa kaunta auze, anaona kama ni kujidhalilisha! Graduate hawezi kuendesha hata daladala au bajaji ya nyumbani kwao anaona anajidhalilisha, matokeo yake ndio tunakua na vijana wanakaa tu kutwa nzima hamna wanachofanya.
 
Kwani asiposifiwa shida iko wapi?

Ukiendesha bodaboda watu wakakusema kwani unakufa?

Ndio maana tunasema vijana wenyewe hawajitambui. Kama mtu unamaliza chuo alafu unaogopa kufanya kazi flani kwamba watu watanionaje huku unapigika kwa njaa maana ake hujitambui.
 
Aisee, hongera sana
 
Wewe ndio umenena. Wazazi wanowaruhusu wapo. Shida ndio ipo kwenye jamii wanakuonea huruma sijui kama wao ndio wanafanya.
Kabisa mkuu.. jamii yetu inatakiwa kubadilika ili vijana waone ni kawaida kupambana nje ya box sababu wakichanganya na elimu yao speed ya kufanikiwa inaweza kuwa kubwa kuliko ambao hawakupata nafasi ya elimu ya juu..
 
Hongera mkuu umeliona
 
Safi sana..
 
Exactly ndo manake
 
Ipo haja ya kuanza semina kuwafungua akili vijana wa kiume coz kiukweli hata Kwenye mahusiano mengi siku hz kumekuwa na mashindano kat ya mwanaume na mwanamke kwakua ...tayar mwanamke ashaanza kupata coverage Kwenye uchumi ..na wanaume n kama wamelala hv
 
Hata mimi nimemshangaa sana pengine ni huyo ndugu yake tu na alipaswa kumsaidia sio kumsema vile. Hajui watoto wa kiume wanavyopambana kwa machungu na hasira.
 
Kama kibarua kipi kwa mfano unachokijua wewe?
Kuna kazi za ulinzi hapa Dar ukienda siku hiyo hiyo unapata kazi hata kama ni LASABA.

Mshahara mpaka Tsh 160,000.

Tena uzuri wa hizi kazi ni kukaa na kutembea tembea tu kidogo.

Kuna watu Dar hii wanabebeshwa viroba vya unga usiku mzima kwenye maviwanda na hawapati hiyo. Asubuhi kunakucha wako hoiiiii
 
Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…