Mimi nilitoka advance nikiwa nina mhemko balaa kwamba siwezi kufundisha shule bila kulipwa Tsh 150,000 ( enzi hizo shule za kata zimeshamiri sana na hazina walimu ). Na shule nyingi zilikuwa zinalipa laki 1 mpaka 120.
Nilivyofika home nikamkuta mama anafanya kazi ya kulipwa 1,500 kwa siku yaani Tsh 45,000 kwa mwezi. Nilijiona mpumbavu sana, nakataaje Tsh 100,000 wakati mama analipwa elfu 45.
Nikaamua kwenda kufundisha, mshahara ni Tsh 100,000 ila take home ni 95,000 baada ya kukatwa elfu 5 ya chai.
Vile vile, baada ya kuhitimu chuo 2016 nilijua tu hapa nikijifanya msomi uchwara nitajuta. Nilienda oufanya kazi za ulinzi ( kampuni niliyoenda recruitment yake utafikiri unaomba kazi usalama wa taifa wakati mshahara ni 250,000 )
Yaani baada ya muda ( wakati wengine bado wanasubiri kazi za ndoto zao wakiwa wamekaa ) mimi nina mambo yangu mengine tu. Vile vile huko NSSF tayari nina kama 3M.
Dunia haijawahi kuwa na huruma na mtu yeyote.
Kaa Dar uzeeke, urudi kijijini kuongea kiingereza kwenye vijiwe vya gongo na kuwasilimulia uliomakiza nao lasaba habari za Dar. Time flies so fast.