Vijana waliofanikiwa maisha

Vijana waliofanikiwa maisha

Kwani ukisema maisha wameyapatia kwa juhudi zao dhambi?
Mungu alisema tusiibe wala tusidhulumu lakini vijana wanafanya yote ili waishi vizuri, hizo ni juhudi zao

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Pasipo Mungu wasingefika hata hapo walipofika,

Ukisoma kitabu cha Mwanzo

Mungu aliwaambia bustanini: '..siku mkila tunda la mti huu hakika mtakufa'

Shetani yeye naye akawaambia: '..mkila tunda la mti huu hakika hamtakufa..'

Shetani alichowaambia hapo ndicho unachoniambia kua Mungu hana issue kwako/kwao unaweza/wanaweza hata bila Mungu kwa juhudi zao binafsi usisahau kwamba kuna wadau wanapumulia mitungi ya oxygen mda huu tena kwa gharama kubwa, wewe hapo ulipo unavuta hewa safi bure, kwanini usimshukuru Mungu?

All in all kila mtu abaki na kile anachokiamini

Mimi ninaamini hata juhudi ulizo nazo wewe au nilizo nazo mimi kwenye kuyatafuta mafanikio nyuma yake kuna uwezo na nguvu kubwa za Mungu zinazotusukuma kuyafikia mafanikio, wewe pekee huwezi usijitukuze na ukajitakatifuza ukaona kana kwamba Mungu hana nafasi katika maisha yako kisa tu umepata mafanikio angalau

Fanya kazi kwa juhudi na bidii ila kwamwe usimsahau Mungu

Rejea: 2 Wathesalonike 3:10
 
Kuna vijana ambao wanaona maisha wameyapatia kama vijana wenye sifa hizi;-
1. Anakaa sinza
2. Anamiliki crown au Mark x
3. Anafanya kazi posta
na hii sio lazima sana anafanya kazi bank.

vijana hawa huwa wanaona maisha wameyapatia sana,
Kwani wewe unafanya kazi wapi?
 
Nilivyo na nilivyonavyo ni kwa ajili ya Mungu,

Wapo watu wanaoishi km kwamba wàmependelewa sana na Mungu

Tambua kwamba ni Mungu aliefanya wawe jinsi walivyo sio juhudi, jitihada, maarifa wala bidii zao binafsi na wala sio matokeo ya akili, maamuzi au matakwa yao binafsi

Yupo anaeshinda, anaelinda, anaetunza na anaekuza kwa ajili yako/yao

Ni yeye pekee alie ukamilifu na utoshelevu

Fanya kila kitu kwa ajili ya yeye pekee

Injili ya Luka 12:19-20

Kumbukumbu la Torati 8:12-14


Nawasilisha..
Asante mkuu
 
Yaani kwa mfano sinza nyumba analipia 300,000+ per month,mafuta ya gari 300,000 per month, matumizi yake 400,000 per month,huoni sio pesa ya kutisha sana,na unaweza kukuta haweki savings.Akipnga nyumba ya laki kuna ubaya gani? au akiendesha ist au vitz ili kusave hela nyingine akajenge
Crown ingekuwa inatumia wese la laki 3 kwa mwezi hata mimi ningelinunua, hayo mafuta ni ya gari kama IST na wenzie
 
Crown ingekuwa inatumia wese la laki 3 kwa mwezi hata mimi ningelinunua, hayo mafuta ni ya gari kama IST na wenzie
Mkuu acha uongo...Kwahiyo unataka kusema kwamba crown kwa safari za sinza to posta ni mafuta zaidi ya 300k+?
 
Mkuu unapotafuta pesa kumbuka kuishi pia, sio lazima ujibane kama wazee wa zamani.
 
Back
Top Bottom