Tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa sugu sana. Ni vijana wengi tunaohitimu vyuo na sekta ya ajira ina nafasi ambabzo haziwezi kutosheleza makontena ya wahitimu yanayomwagwa mtaani kila mwaka.
Mimi ni mmoja wapo wa wahanga waliokosa ajira na kuihangaika sana kuzunguka na vyeti mtaani hadi nikakata tamaa tu baada ya mwaka mmoja nikaachana na kutafuta ajira mpaka Mungu aliponiona na kunipa plan B.
Kujiajiri mara nyingi kunahitaji mtaji hata kilimo pia kinahitaji mtaji kwahiyo wengi wanaosema mkajiajiri utakuta wao wameajiriwa.
Leo nita share nanyi njia ambayo mtu unaweza kujiajiri ukatengeneza pesa ambayo hata wale walioajiriwa wanaiota.
Kuna kitu kinaitwa freelancing. Nadhani wengi mmeshwahi kusikia kuna kazi unaweza kufanya mtandaoni na kulipwa. Na najua wengi mlishwahi kujaribu na mwisho unagundua hakuna ukweli na wala huambulii chochote na wengi mtu akiwambia kuna kazi unaweza fanya mtandaoni ukalipwa utaishia kusema ni utapeli.
Lakini ukweli ni kwamba ndiyo kuna kazi unaweza fanya mtandaoni na ukalipwa, tatizo ni kujua zipi fake na zipi za ukweli.
kuna kufanya surveys, hizi hazina malipo ya maana na mitandao mingi inatoa shopping vouvhers na siyo ela. Mfano wake ni opinion panel ambbayo inatoa kati ya 0.50 pound kwa kila survey utakyopewa na inaezekana upewe moja kila week sasa kwa mustakhabari huo huwezi tengeneza pesa ya maana zaidi ya kupoteza muda.
Kuna referals, Kuna mitandao inadai inatoa ela kwa kurefer watu wengine wajiunge. Nimejaribu kuipitia mitandao mingi ipo amayo kweli inatoa ela lakini ni kiasi kidogo hata kufikisha 10$ kwa miezi sita ni kazi. Na may zaidi mitandao mingi ya hiovyo ni ya uongo.
Ipi mitandao ya kweli na nitajuaje kama kama kazi zilizopo ni za kweli.
Kwanza kabisa zingatia hili, hakuna free money. Ukiona mtandao unakuahidi kukulipa pasipo kufanya kazi yoyote ya maana jua huo mtandao ni fake/scam. Inaidi ufanye kazi.
Pili ela unayoahidiwa kulipwa iendan na kazi, siyo unaambiwa utype page moja then ulipwee $200, katika akili ya kawaida utaona kabisa malipo hayaendani na kazi.
Tatu tumia mitandao ina yo review na kukwambbia kama mtandao flani ni Legit au scam.
Jinsi ya kutengeneza pesa.
Katika kufanya kazi mtandaoni kama freelancer nimeweza kuja na list ya mitandao ambayo ninaiamini.
1. Feverr: Huu ni wa uhakika kabisa kuna kazi nyingi sana humu. Ila inahitaji utengeneza profile na portfolio ya maana maana wanafanya screening ya nguvu kabbla ya kukuruhusu kuanza kugombea kazi zilizo postiwa.
Kuna kila aina ya kazi kuanzia kutype, graphics, we designing, content writting, music, animation, Legal Documents yani kazi zote uzijuazo wewe. Na jambbo la kushangaza ni kwamba kuna hadi wa tanzania wanapost humu wakitafuta freelancers wa kuwafanyia kazi zao.
Freelancer. Huu ni mtandao mwingine ninaouamini na nimefanya kazi nyingi hapa na babdo ninaendelea kufanya walau kila siku kazi 2 mpaka 5. Tatizo la huu mtandao kuna matapeli kutoka Asia ambao wanapenda kupost akzi za data entry zikiwa na malipo makubwa sana mfano type 30 pages for $250. Ukiona hivi machale inabidi ya kucheze. Pia malipo na kazi zote zinabidi zifanyie kwenye platform yenyewe maana mpaka mtu anakupa kazi wao freelancer wanakuwa washa hold ile ela mliyoelewana ili ukimaliza waiachie kwenye account yako sasa hawa matapeli wanakushauri mkaelewane kwenye email ukiona hivyo jua ni matapeli maana kwanza policy ya freelancer ni kuwork within the paltform ili msitapeliane. Uwa wanaondoa matangazo yao lakini incase ukikutana na scenario ya namna jua umekumbana na tapeli.
Kuna mtandao mwingine unaitwa Guru nao ni kama freelancer.
Kuna mmoja huu sasa si wa freelancer ila unaitwa Kentar Futures. Hawa watu wanalipa ela sana sana unaweza kuhisi ni matapeli ila ni kweli mtupu na nimefanya nao kazi kwa muda mrefu japo ni kwa msimu kazi zao zinaweza kuja mfululizo miezi sita halafu zikakata hata kwa miez sita mingine lakini zikianza kuja unakuta unapewa kazi kila week kazi moja na kila kazi ukimaliza unalipwa $450. Inategemea ni kazi gani ila sometimes uwa malipo anashuka kama ni kazi ndogo ya siku 4 unakuta wanalipa $115 na wanalipa direct via money wire.
Nitaendela kuwahabarisha mengine mkiwa interested.
View attachment 869024