Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Wakuu.. nimekutana na changamoto moja,
Mi ni electrical engineer sina mda mwingi mtaani... na ndoto zangu ni kujiajiri kwenye fani yangu.... lakin kabla hata sijaanza hizo harakati... ametokea mjomba... anataka kunipeleka jeshin... ndugu, marafiki woote wananisukuma niingie huko.... lakin mi roho inaniuma, maana sijajaribu ndoto yangu.
Nikijaribu kuwashirikisha ninachotaka kukifanya, kila mtu ananiambia nikijiajiri ntashindwa maisha.... jesh ndo nafas pekee ya kufanya maisha... nikishapata nyota zangu ntalipwa ela ndefu..
Kimsingi sielewi nifanye nin kwenye kona hii...
Mume wangu ana nyota zake za kutosha ila hana pesa kubwa kama mnavyoaminishana mtaani...Jiajiri mkuu...
Kuhusu jeshi wafate wenye nyota kuanzia kapten wakueleze hali halisi
 
Mkuu kwanza hongera kwa dhamira yako uliyonayo.

Kwa maoni yangu naona, ili mtu akushauri vizuri, kwamba uendelee kufanya kazi jeshini ama laa inabidi ajue mambo mengi kuhusu wewe mfano kwa jinsi familia yako ilivyo, yaani kama una pa kuanzia? Kwa maana ya mtaji ulionao. Tumeshafahamu maarifa ya huo ujuzi unayo.

Let's say una mtaji wa kuanzia, au yupo mtu wa kukupa mtaji wa kuanzia..... Utakuwa na haja gani ya kwenda huko kwenye amri ambapo haparuhusu mdogo ku reason na mkubwa, hata kama mkubwa anaenda chaka. So kama una pa kuanzia financially go direct for your dream Broo, ingawa inabidi utafiti hiyo industry ya electrical engineering kama ina lipa ama laa.

Option ya pili ni kuingia jeshini, hii njia nakushauri Ifuate kama tu huna pa kuanzia, hapa namaanisha mtaji. Kwani wewe hautakuwa boss of yourself wa kwanza kuanza kwa kuajiriwa na kisha kutoka na Kujiajiri mwenyewe. Hapa pia sijajua kwa jeshini ipoje, kama once you are in..... there is no way you get out and become a a normal civilian au inaruhusiwa kuacha kazi ya jeshi kama zilivyo kazi nyingine.

Kama jeshini inarusiwakuacha kazi jipe miaka 5, kusanya mtaji, kisha rudi uraiani kupiga mishe. Ila be careful, usinogewe na ka mshahara ka vimilioni na ration ya laki nne ukasahau ndoto yako. BEST LUCK FRIEND.
umemshauri vyema,
 
mi ni mmoja kati ya watu wenye plan ya kujilipua....

nachukia saaana kumuachia MTU muda wangu mwingi ili atengeneze faida zake.

soon nitatumia muda wangu kwa faida yangu.....

but before ya yoote... hizi ndizo nguzo muhimu.

1. miliki Nyumba 4. mbili kati ya izo ziwe maeneo mazuri kibiashara.

2. miliki mashamba si chini ya heka 50. 20 kati ya izo.... ziwe na mazao endelevu. eg. korosho... minazi... miti.. kahawa n.k

3. kuwa na mifugo... kuku..ngombe... mbuzi...nguruwe...

4. tenga mtaji wa m20 tu.....
acha kazi

hauwez juta kamwe.
 
Kwa mfanyakazi ategemeaye mshahara tu ni ndoto kufanikisha haya; Hususani wanaoishi mjini.

Ikiwa mtumishi ategemeaye mshahara ni changamoto kujenga nyumba moja tu, je ndio atakuwa na uwezo wakujenga nyumba 4 kupitia mshahara wa mwajiri wake??

Kimsingi kupata mafanikio nje ya ajira hakutegemei haya yote bali ni akiri yako tu na jinsi unavyojishughulisha.

Sababu MAISHA YAKO YANATOKANA NA UNAVYOWAZA NDANI YAKO
 
haujaelewa..... namaanishi kwa kutumia akili ukipata haya hapo ndipo kuacha kazi hakotokufanya uwe na mawazo.
 
mi ni mmoja kati ya watu wenye plan ya kujilipua....

nachukia saaana kumuachia MTU muda wangu mwingi ili atengeneze faida zake.

soon nitatumia muda wangu kwa faida yangu.....

but before ya yoote... hizi ndizo nguzo muhimu.

1. miliki Nyumba 4. mbili kati ya izo ziwe maeneo mazuri kibiashara.

2. miliki mashamba si chini ya heka 50. 20 kati ya izo.... ziwe na mazao endelevu. eg. korosho... minazi... miti.. kahawa n.k

3. kuwa na mifugo... kuku..ngombe... mbuzi...nguruwe...

4. tenga mtaji wa m20 tu.....
acha kazi

hauwez juta kamwe.
Haya ni mawazo mazuri lakini kumbuka mafanikio haya uliyoyasema ni ya mfanyakazi ambae ndo anastaafu.mpaka ukapate hivyo vyote si leo wala kesho na unaweza ukavikosa kabisa ukiwa kazini labda tu kuna watu kwenye mashirika ya kigeni NGO wenye nafasi nzuri na mishahara ya milion 7 mpka 8 huko ndo wanaweza kujiandaa kwa hivi ulivyosema wewe! Mimi nimeacha kazi nikiwa na nyumba moja tu na duka moja la mtaji wa milion 9 na gari moja rav4 kwisha.
 
Mi nafikiri kupata experience ya biashara kwanza ndo jambo la muhimu
Kwa nini?
Kwa sababu kabla hujaacha kazi plan lazma ijitosheleze
Kivipi?
Bajeti ya biashara iwe tofauti na ya kufanyia mambo mengine
Kwa sababu kuna watu wanaacha/wanatarajia kuacha kazi wakitaka kujiajiri labda unakuta amekusanya million 1 kwa ajil ya biashara
Shda inakuja pale mtu anapochanganya iyo million na kulipa kodi, ada n.k
Kwa mtindo huo lazma ufel
It's happened to me
kweli mkuu ilike your comment hapo ndo watu wengi hufeli unakuta mtu kalipia chumba na na kuweka frem katika mandhari nzuri ili iendane na mazingira anayotaka kununua miundo mbinu mingine kama meza shelves mtaji unakata
 
Kutoka kwenye ajira inahitaji maamuzi magumu,kabla hujaacha kazi anzisha biashara au mradi ambao utausimamia na ukaona faida yake inakuwaje na kama umepata hasara urekebishe wapi.Kwa sababu Mara nyingi biashara haikuwi Mara moja,ni kusimama na kuanguka.Tafakari kabla.
good comment
sasa watu wanaacha kwa kukurupuka tu baadae hata ela ya kula anakosa
 
Vitabu vingine vizuri ni E-Myth kinaongelea kuhusu kuanzisha MFUMO WA BIASHARA ambao ndio kiini cha mafanikio kwenye biashara. Kingine ni 21 Secrets of Self Made Millionaires, kuna Richest Man in Babylon, pia kipo The millionaire Next Door, Get Rich Your Own Way n.k

Ukivisoma hivyo huwezi kubaki kama ulivyokuwa mwanzo
Unavyo hivyo vitabu...naomba uweke attachment. Nataka nivisome
 
Kujiajiri inategemea inspiration yako, and ni vigumu kumanage business kama unafanya hivyo kwa kuiga mtu,.....
Waliofanikiwa kuacha kazi wakaingia kwny business na wakafanikiwa ni wao walikuw na mawazo hayo ya kujiajiri toka kipind wakiwa wadogo/shuleni, hawa kwao inakuwa rahisi maana anaingia kazini kwa lengo la kutafuta capital tu, mtu wa namna hii hata kwa mtaji wa mil8 tu anaweza kuwa Billionea ndan ya muda mfupi tu, hawa huwa rough sana kimwonekano hawana show off za ovyo ovyo, wanakuwa tayar kuish maisha ya kula wali maharage (buk ) wakat kaz aloacha staff tea tu buk5 , anakuwa tayar kulala chini(Hana kitanda) wakat hela ya kitanda anayo but analinda mtaji, anauwezo wa kulinda mtaji wake katika hali ngum coz anajua akiharibu itachukua muda kufika anapoenda,... kujiajiri inataka moyo but kiukwel kama una strategies unatafanikiwa, binafs niliacha chuo kabsa ili nipige biashara, mtaji unakuwa kwa kasi mpk najilaum sijui kwa nin skuishia tu f6 maana kama kiingereza kimeshakaa hesabu za hela zpo, ....ukitaka kukuza mtaji shart moja kama umeanza na mil1 ukafika mil5, usitumie faida Bali fanya hiyo mil5 yote mtaji hapo utafika mil20 then wekeza hata mil15 tena, taratibu utasogea mil50, endelea kukuza mtaji nakwambia within ten yrs mil 100 utaona pesa ya kawaida sana, kingine wakat unafanya biashara hii,unakuwa unafanya research kitu gan kingne ubaweza kufanya upanue wigo wako,..vijana wengi wanashindwa coz they know nothing about capital management in business issues, unakuta anamtaj wa mil10 AKIPATA faida yan tayar ashawaza kununua S8 edge, sijui gar, au akapange nyumba kali, ndan ya muda mfupi tu, hawajui lolote kuhusu DEAD TIME in business, hiki ni kipind ambacho hakuna faida unayoitumia zaid unakuza mtaji, haya Mambo hayahitaji shule ni natural kabsa, maana waliosomea biashara wameajiriwa kama manager, sjui account nk
 
Mkuu nimekuelewa sana. Ila naamini sio lazima uwe na mawazo hayo tangu ukiwa mdogo. Hata mimi haya mawazo ya Kuacha kazi nimepata may be 2 years ago, japo nikiri nina uwezo wa ku save fedha.

Ila mengine yote nimekubali mkuu. Cha msingi ni kutoridhika. Ukiwa na milioni 10, go for 20,ukiwa na 20 go for 50 hivyo hivyo mpaka ufike malengo yako. Mtu hutakiwi kuridhika haraka. Hata ukifikisha 100 million ishi kama ulivyokuwa unaishi ukiwa na 10 milioni
 
Wakuu mwenye vitabu vifuatavyo au ajuaye jins na wapi kwa kuvipakua atusaidie

Business school for people who likes helping people by Kiyosaki
2. What works on a wall street by James P. O. O’shaughness
 
Kujiajir kuna changamoto ILa ni kupambana nazo tu ...Mimi nmeacha kazi ya ualimu nloanza 2015 nna miaka 24 ....nimejiajir nasafirisha kuni toka pwan kuwaletea wauzaji wa rejareja na naangalia nifungue nam kijiwe changu ...

Japo bsness haijawa nzur kiivo na nna miez minne ila naamin ntafka mbali .

Na ukiwa uko job maybe hujui ukitoka ufanye nn ...zpo fursa nyingi sana ukiwa na hta one million tu ....unaweza end mtwara kununua korosho na ukauza kwa vyama vya ushirika inalipa sana

Let's do it kuajiriwa n utumwa sana ....Allah atufanyie wepes

Mkuu tutafutane mim nina kibali cha maliasili cha uvunaj wa miti
 
Kuacha kazi ni moja ya maamuzi màgumu ambayo yanahitaji ujasiri ña mentally preparation. Huhitaji kuwa na kiasi fulani cha pesa ili uache kazi ila unahitaji malengo,kwanini naacha kazi?unataka kufika wapi baada ya muda fulani?unataka uwe una earn kiasi gani cha pesa per month?Hàyo ni baadhi ya maswali yanayoweza kukuongoza kuchora ideas.Mwanafalsa John luis Bragos anasema"if you want to think more creative,you must challenge the boundary".Ukiwa unajiandaa kuacha kazi lazima ubadili mfumo mzima wa maisha wakati mwingine hata marafiki(mates)wako ili kuweza kufikiri out side of the room.A real estate investor Sir Donald Trump said"You have to think anyway,so why don't think big"Lazima uwe na malengo yako ya muda mrefu na uchore mpango kazi namna ya kuyatimiza hayo malengo.
Ukiongozwa na msukumo wa ndani na ukajifunza kwa waliofanya wakafanikiwa(mentor) naamini itakupa mwanga mkubwa sana katika safari Yoko.Note usiombe ushauri kwa wafanyakazi wenzako watakukatisha tamaa na kukutia woga.

Binafsi ni mwajiriwa but nimeweka malengo kuwa ikifika 2025 nataka kuacha kazi kwani nimeajiriwa 2015.Kwa kuwa safari yeyote inahitaji maandalizi nilishaanza kujiandaa since day one naingia kazini.Nasoma vitabu kwa wingi kuongeza maarifa lakini natafuta taarifa kwa hali na mali lakini pia nimeanzisha project ambazo zinanisaidia kuniongezea uzoefu katika kujiajiri.
My take.Failure is party of process of success
Nimekusoma!!!
 
Haya ni mawazo mazuri lakini kumbuka mafanikio haya uliyoyasema ni ya mfanyakazi ambae ndo anastaafu.mpaka ukapate hivyo vyote si leo wala kesho na unaweza ukavikosa kabisa ukiwa kazini labda tu kuna watu kwenye mashirika ya kigeni NGO wenye nafasi nzuri na mishahara ya milion 7 mpka 8 huko ndo wanaweza kujiandaa kwa hivi ulivyosema wewe! Mimi nimeacha kazi nikiwa na nyumba moja tu na duka moja la mtaji wa milion 9 na gari moja rav4 kwisha.
km ulifanya kazi kwa miaka 20 kwa mshahara wa laki 5 kwa mwez.... na ukashndwa kupata ivyo vitu had unastaafu....

ni uzembe pia.
 
km ulifanya kazi kwa miaka 20 kwa mshahara wa laki 5 kwa mwez.... na ukashndwa kupata ivyo vitu had unastaafu....

ni uzembe pia.
Miaka 20 kazini huwezi kua kwenye kundi la wanaotakiwa kuacha kazi na kwenda kujitegemea sasa,miaka yote hiyo upo kwenye kazi za watu si afadhali uendelee tu mpaka uzeeni.kaa kazini miaka mitano tu au 8 then nenda kajitegemee
 
Back
Top Bottom