imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Acha uongo, ni Binadamu gani ambae hachoki au kupumzika?Mh Rais anaendelea kufanya kazi bila kuchoka Wala kupumzika
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha uongo, ni Binadamu gani ambae hachoki au kupumzika?Mh Rais anaendelea kufanya kazi bila kuchoka Wala kupumzika
Ndugu zangu kwa miaka mingi na kwa kipindi kirefu na kwa chaguzi nyingi vijana wa kitanzania wamekuwa wakijitokeza kwa kiasi kidogo Sana kupiga kura na kushiriki katika uchaguzi, Japo wakati mwingine wamekuwa wahudhuriaji Wazuri wa mikutano ya vyama vya siasa lakini wamekuwa wa mwisho linapokuja suala la kujitokeza siku ya kupiga kura.
Hii Ni kutokana na kukatishwa Tamaa na baadhi ya watu au viongozi waliokuwa wanawaamini Mara wanapokuwa wamepata nafasi za uongozi, vijana wamekuwa wakiona Ni Kama wanatumiwa tu pasipo kupata faida yoyote, vijana wamekuwa wanaona ni Kama hawapewi kipaombele hasa suala la ajira na mikopo, vijana wamekuwa wakiona ni Kama hata wakijaribu nafasi za uongozi hawachaguliwi kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kifedha ambazo baadhi ya wajumbe Ni Kama wamekuwa wakiangalia kina Cha mfuko wa pesa kumpa mtu Kura
Jambo hili limekuwa likiwakatisha Tamaa vijana, kuwavunja moyo,kuwa fanya waichukie siasa, kuwachukia baadhi ya wanasiasa wanaokuwa wakitoa lugha zinazo chukuliwa Kama dharau kwa vijana hasa wanapoona mtoaji wa kauli katika maisha yake yote hajawahi kujiajiri Wala kuwa machinga Wala kuwa muuza karanga Wala kushika jembe Wala kuendesha bodaboda Wala kulima matikiti maji Wala kuwa na biashara ya aina yoyote Ile zaidi ya kuhudumiwa kwa Kodi za Watanzania wavuja jasho ambao hawana uhakika wa kupata hata Milo mitatu kwa siku Wala kuelewa Ni vipi watalipa Kodi ya nyumba.
Lakini Tangia Rais Samia aapishwe na kuwa Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ni Kama vijana wamechanua kimatumaini, wamepata Imani ya kuwa Sasa ndoto zao zitaweza kutimia, Sasa vijana wanajionaa wanaweza kugombea na kuwa viongozi hata Kama hawana fedha ilimradi tu wawe na sifa na vigezo vya kiuongozi na kukubalika na kuaminika na wapiga kura, Sasa vijana Wana Ari mpya na nguvu mpya ya kuijenga nchi yao, Sasa vijana na kila kijana anaona kuwa inawezekana kuinuka kiuchumi bila tatizo lolote,
Sasa vijana wanaona ukiwa hata na kiasi kidogo Cha mtaji unaweza ukafungua biashara na ikakua na kustawi na kuchangia katika ujenzi wa nchi yao, Sasa vijana wanaona kuwa keki ya Taifa inawafikia walipo, Sasa vijana wanaona kuwa serikali Ni yao, inawatumikia wao na inawapa kipaombele.
wanaona serikali yao inavyopambana kuweka mazingira wezeshi kwao, wanaona namna serikali yao inavyotaka kuhakikisha kuwa halmashauri zinatoa mikopo kwao pale wanapokuwa wamefuata taratibu na kukidhi vigezo, wanaona namna ambavyo hakuna ubaguzi katika kupata ajira au fursa ya aina yoyote Ile ya kiuchumi, wanaona namna serikali yao inavyojitahidi kutengeneza fursa za ajira kila Siku kupitia miradi mbalimbali Inayochipua kila siku
Rais Samia kawasha Taa ya matumaini katika mioyo ya Vijana wa kitanzania, Kaonyesha njia ya kufika katika mafanikio, kaonyesha upendo kwa vijana wake ambao hupenda kuwaita WANANGU kwa namna anavyo wapenda na kuwajari vijana wa kitanzania,
Hii imepelekea vijana kujiandaa kwa Hamu kubwa Sana kuja kumpigia kura nyingi Sana za ndio Rais Samia ili aendelee kuwatumikia vijana, ili aendelee kuwapa neema na fursa za kiuchumi maana vijana wameona kuwa Rais Samia Ni kiongozi aliyeonyesha dhamira ya dhati katika kuwabeba vijana na kuwakuza na kuwastawisha kiuchumi, Rais Samia ameonyesha Dhamira yake ya kuona fursa yoyote inayopatikana inakwenda kuwagusa kwanza vijana na kuwanufaisha
Rais Samia anahitaji kuona vijana wanajitegemea kiuchumi na kuwa na uwezo wa kujihudumia na kuwasaidia wazee wao wanaohitaji msaada wa kusaidiwa na kulelewa, Rais Samia Ni kipenzi Cha vijana ambaye amepelekea uchaguzi ujao kuwa mwepesi Sana kwake na kwa CCM kwa kuwa vijana wameamua kumpigia kura na kumuunga mkono
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Suala la umeme tunaona namna serikali yetu inavyo jitahidi kusambaza Hadi vijijini ili kufungua fursa za ajira kwa vijana, hat hivyo Mimi niliko huku umeme ulishafika na upo muda wote kasoro siku chache chache wanapokuwa wanafanyaa matengenezo yao ambapo huwa wananchi tunapewa taaarifaHao vijana wana matumaini gani ilhali nyenzo muhimu kama umeme hakuna?
Galileo alipingwa na kila mtu mpaka kifo chake alibaki anasimamia ukweli aliouamini na baadaye ikaja kugundulika na kubainika wazi kuwa alikuwa sahihi juu ya mawazo yake, hivyo Hilo lisikupe shida, maana ukweli hauangalii wangapi wanapinga au kuunga mkono, ukweli Ni ukweli tu hata ukipigwa mawe unabaki kuwa ukweliView attachment 2397436
masaa mawili like moja?? inafikirisha😀😀😀 we pokea ela yako ya uchawa
Wewe waona Ni uongo kwa kuwa unafanya kazi zako na kuishia unapoona panafaa kwa siku husika, lakini watanzania tunaona namna mh Rais akiwa kazini kuwatumikia watanzania hata Kama ametoka safarini na kufika Leo unakuta kesho yake yupo ziarani kusikiliza na kutatua kero za wananchiAcha uongo, ni Binadamu gani ambae hachoki au kupumzika?
Jiji lipiKero ya Jiji Braza Luka
Kwahiyo anapumzika, wewe umejikita kwenye Propaganda kuliko uhalisia,hakuna Binadamu ambaye hapumziki.Kama ametoka safarini na kufika Leo unakuta kesho yake yupo ziarani
Huku kwetu ni mgao na hakuna cha marekebisho yoyote yanayoendelea. Shughuli zote zinazohitaji umeme zimesimama, na hao vijana unaosema watampigia kura labda wawe wanatoka huko kwenu.Suala la umeme tunaona namna serikali yetu inavyo jitahidi kusambaza Hadi vijijini ili kufungua fursa za ajira kwa vijana, hat hivyo Mimi niliko huku umeme ulishafika na upo muda wote kasoro siku chache chache wanapokuwa wanafanyaa matengenezo yao ambapo huwa wananchi tunapewa taaarifa
Bila shaka kutakuwa na matengenezo yanayofanyika japo hamjapewa TaarifaHuku kwetu ni mgao na hakuna cha marekebisho yoyote yanayoendelea. Shughuli zote zinazohitaji umeme zimesimama, na hao vijana unaosema watampigia kura labda wawe wanatoka huko kwenu.
Hamna kijana wa kupigia kura chama cha wazee na majizi, labda wapewe hela, na bado kura ni kwa CDM.Utabaki mwenyewe tu hapo ufipa lakini vijana wanajiandaa kumpigia kura mh Rais wetu mpendwa mama Samia kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kuwatumikia watanzania
Huku kwetu ni mgao na hakuna cha marekebisho yoyote yanayoendelea. Shughuli zote zinazohitaji umeme zimesimama, na hao vijana unaosema watampigia kura labda wawe wanatoka huko kwenu.
Bila shaka kutakuwa na matengenezo yanayofanyika japo hamjapewa Taarifa
Vijana tujikite kujenga Taifa letu maana Taifa letu litajengwa na sisi vijana kupitia mikono yetu, Tumuunge mkono mh Rais ambaye ameonyesha dhamira njema kwetu vijana Katika kuhakikisha tunakua kiuchumiAnatafuta teuzi kwa nguvu zote.Pia ongeza namba yako ya simu .
Mimi naamini hakuna mgao ili linakuwa Kuna matengenezo madogo madogo, Niliko umeme upo muda mwingi Sana japo ni mkoaniMgao sasa hivi ni kawaida, acha kutetea serekali ya majizi wakati uwezo wao ni mdogo.
Nyanda za juu kusini huku vijana wote wanasema Ni Samia mpaka 2030[emoji23][emoji23] wawe wanatoka kwao