Vijana watajitokeza kwa wingi sana kumpigia kura Rais Samia uchaguzi Ujao, Ni uchaguzi utakaoweka Historia ya vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura

Kweli umesahau kuweka namba ya simu ili uteuzi unaousaka uupate kwa urahisi!
 
vijana watakao piga kura wanamattz ya akili kdg
Umeme n janga
Maji usiseme
Mabando mungu wangu
Tozo
Hayo mamb hayahusian kbsa na vita vya ukraine
analeta porojo hana jipya pamoja na waliomtuma.
 
Labda kama waliofukuzwa na kuvunjiwa vibanda vyao wakijitafutia ridhiki mitaani siyo vijana.

Labda wanaomaliza vyuo na kukosa ajira siyo vijana.

Labda kama wanaopata adha ya ku katika kwa umeme kila siku na kushindwa kufanya kazi yoyote ya kujipatia kipato hata kama ni kuuza barafu siyo vijana.

Labda kama wanaokutana na utitiri wa kodi pale wanapotaka kusajuli biashara hata kama ni ya kuuza pipi siyo vijana.

Labda kama wanaokwazika na uzorotaji wa maadili katika utumishi wa umma siyo vijana.

Labda kama wanaokwazika na rushwa, uzembe makazini na ubadhirifu wa Mali ya umma siyo vijana.

Labda kama matozo na makodi yasiyokuwa na msingi hajawagusi vijana.

Labda kama na vijana wote nchini nao wanapata wanapata pa kulamba asali.

Hivi unawachukuliaje vijana jomba? au unaona watu ni wajinga saaana? Watanzania wapo kimya tu ila wanaona kila kinachofanyika so let's wait and see
 
labda kijiji cha ng'ombe waliokatwa mikia ndio wanaosema hayo.
Ni vijana wa kitanzania walioridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia, mfano vijana wanaojishughulisha na kilimo wanamuunga mkono Rais baada ya kutoa Ruzuku ya mabillioni ya pesa za kitanzania na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni , vijana wa sekondari na vyuo vikuu na vya Kati ambao wameona namna mh Samia alivyotoa nuru kwao ya kupata Elimu bila kikwazo hasa baada ya kufuta Ada Hadi kidato Cha sita na kuongeza mikopo kwa Elimu ya juu
 
unau hakika unaelewa ulichoandika???
Hapa hatuongelei iman tunaongelea vijana
wala hatuongelei mapenzi binafsi tunaongelea Umma!!…

…….
#KalagaBaho
 
unau hakika unaelewa ulichoandika???
Hapa hatuongelei iman tunaongelea vijana
wala hatuongelei mapenzi binafsi tunaongelea Umma!!…

…….
#KalagaBaho
Hata Mimi nimeongelea habari za vijana kuwa na Imani na matumaini makubwa Sana na uongozi wa mh Rais Samia, kutokana na namna alivyo fanya kazi kubwa ambayo imetoa fursa za ajira kwa vijana
 
Unawaza kupiga kura, hauwazi matatizo yaliyopo kila siku bila kutatuliwa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unawaza kupiga kura, hauwazi matatizo yaliyopo kila siku bila kutatuliwa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Matatizo yanaendelea kutatuliwa na serikali ya mama Samia kila Siku, Tumeona katika mbolea namna Bei ya Bei juu ilivyotatuliwa na serikali, Tumeona namna suala la Bei ya nishati ya mafuta ambavyo lilitatuliwa, Tuliona namna suala la uhaba wa madwati na vyumba vya madarasa ambavyo yalitatuliwa. Kwa ufupi Ni kuwa hii Ni serikali ambayo IPO kazini muda na Wakati wote
 
Huyu mpuuzi APUUZWE, asijibiwe, ataacha upuuzi wake.
Unaweza ukachangia bila hata kutumia lugha za ukakasi, Taifa letu litaendelea na kusonga mbelee kimaendeleo kutokana na fikira zetu chanya, siyo muda wote umejengeka katika kukosoa na kupinga pinga tu bila hoja za kueleweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…