Na chanzo kikuu ni kufuata sheria za watu viongozi wa makanisa wanaofanya ndoa ziwe ngumu badala ya kufata maandiko matakatifu yaliyorahisisha ndoa
1. KUVUNJA NDOA
Sheria ya ndoa za kikristo imekataza kuvunja ndoa kasoro tu ukiwa na ushahidi watu wajue "unachapiwa" na ndio maana huwa mafumanizi yanaandaliwa, cha ajabu watu wanakimbilia mahakamani kuvunja ndoa zao kwa sheria, sababu zao ni kwamba mwenzake ni mchawi, kwa miezi anamnyima unyumba, ni mlevi, anatukania wazazi wake, anatenga ndugu zake, n.k inashindikana vipi kuvumiliana kwenye shida kama mlivyokubali kiapo cha shida na raha ?
2. KUOA / KUOLEWA UPYA
Sheria ya kuoa upya ndoa za kikristo ni pale tu mwenza wako akifa ama uwe na ushahidi watu wajue unachapiwa, cha ajabu mtu akishindwana na mwenzake kwa sababu zilizo nje ya hizo mfano kunyimwa unyumba, mke anatenga ndugu zake, mme anampiga sana, n.k. anakimbilia mahakamani kuvunja ndoa na anaoa ama kuolewa upya,
3. KUONGEZA MKE / MME
Sheria za kuongeza mke hazipo kwenye ukristo lakini mambo ni tofauti, Michepuko imekuwa ni wimbo wa taifa kwa sasa hasa kwa wakristo maana hawarusiwi kuongeza mke, imekuwa kama fashion, mtu anavyoishi na mchepuko ni kama mke wake tu, ni kawaida hata kukuta mchepuko kajengewa nyumba, chanzo cha haya yote utasikia "mme kaenda jela kifungo cha maisha", "mke kaenda kusoma ulaya miaka mitatu", "nyumbani kuna vurugu hakuna amani hatuongei", n.k
4.MIMBA AMA KUZAA KABLA YA NDOA
Imekuwa kama fashion sikuhizi, mimba ama kuwa na watoto kwanza kabla ya ndoa, sababu ni kwamba ndoa ya kikristo ni mpaka kifo, wengi wanaogopa kuoa wanawake wenye matatizo ya uzazi waje kuishi bila watoto, wazazi wao wakose wajukuu....