Vijana wengi wa kikristo huchelewa kuoa ama hawaoi ni ushahidi tosha kwamba ndoa za kikristo ni gereza

Mimi ni kijana. Nina ndoa sasa mwaka na miezi. Lazima ufahamu kuna ndoa na utandawazi. Ndoa ni makubaliano Kati ya pande mbili Bwana na Bibi. Alafu kuna cheti cha ndoa. Hii ni karatasi itokayo Serikalini ikiwa na maana ya kushughulikia mambo ya mirathi na ushahidi wa Bwana na Bibi kisheria. Unaposema kuhusu mafarakano na kuvunjika hapo tunaongelea utandawazi. Unaposema kuhusu kuzaa kabla ya ndoa pia ni utandawazi. Usichanganye ndoa na utandawazi haswa kwa hii nchi ya kitandawazi.
 
Baadhi ya point ni matakwa ya kinadamu sio dini.. Hata wanaofungisha izo ndoa ni watu kama wewe wanaangalia maslahi yao.Dini haihusiki.
 
Wanawake wa kikristo nanyi mnashindwaje kuvumilia kuwasubiria wanaume wakipewa vifungo vya miaka 30 jela ?

Mna visingizio vya ajabu sana kuolewa upya, unashindwa vipi kumsubiri mme wako amalize kifungo cha miaka 30 ndio mje mpate mtoto ?
Fallacy. Umeconduct utafiti kwa wangapi mpenzi?? Very simple achana na Ukristo babaa. Unapoona bidhaa dukani haikufai si unaenda tafuta inayokufaa ama!!

Maongezi ya kidini na faults za kidini ni very cheap. Unataka mabadiliko... stand out. Be the change.
 
Kufungua thread zaidi ya nne ndani ya miezi 2 kuongelea tu ndoa za kikristu inafikirisha brother
 
Lakini kuongeza mke sio kosa mbuna mfalme Sleiman alioa 600 na michepuko 300
 
Watu hukimbilia mahakamani kwasababu sheria za ndoa za kikristo haziwei kuyatatua matatizo yao.


-Mtu unaishi na mwanamke ana kiburi kupindukia, uchumbani alifeki ana tabia nzuri ili aolewe, unaenda kanisani eti mnaambiwa mvumiliane, haiingii akilini, solution ni kwenda mahakamani

-Mwanamke amegeuzwa kama ngoma anapigwa kila siku, huko kanisani mnaambiwa mvumiliane mpaka kifo, ni ujinga wa wapi huu, solution ni kwenda mahakamani.

-Mwanamke kamgomea mumewe kuongeza mtoto, yeye anataka mtoto moja tu, ni upuuzi huu! Sheria za kikristo zinambana kuvunja ndoa na kuoa upya, inabidi aende mahakamani

-Mwanamke anamnyima mme wake unyumba takribani miezi 6 sasa, iweje mwnaume asipewe haki yake ya kindoa na kanisa liendelee kukazia hauwezi kupata mbadala, ndio hapa solution huwa ni kwenda mahakamani.

-Mwanaume kaenda jela kifungo cha miaka 30 kamwacha mke wake na huko jela hawaruhusu mme hata kumtunga mimba mke wake, mke inabidi aende mahakamani kuomba ndoa ivunjwe aolewe na mwengine azae watoto awe na familia. kanisani hawawezi kuvunja ndoa na kumruhusu aolewe upya labda nao watoke nje ya sheria zao
 
Aiseee..Ila nadhani Biblia inatafsiriwa vibaya na viongozi wa dini. Maandiko yanasema isipokuwa kwa kosa la uzinzi, mwanaume mvumilie mke wako na usiwe na uchungu naye.

Hivyo talaka kwenye maandiko ipo sema viongozi wa dini hawaitaki maana kama leo hii itaruhusiwa, hiiiiiii tutashuhudia mambo mengi sana kwenye haya makanisa.

Sasa, kukwepa hii kadhia Mtume Paulo alishauri kabisa watu wasioe au kuolewa, wajikite kwenye kumtumikia Mungu. Akimaanisha kwamba duniani kuna mambo muhimu zaidi ya ndoa.

Siyo lazima kuoa au kuolewa....
 
Hata kuwa na mke mmoja sio sawa kabisa
Kuoa mke moja hakujawahi kukatazwa kwenye biblia maana hata kina Musa waliotuletea amri kumi walikuwa na mke zaidi ya moja kwa baraka zote za Mungu.

Yesu alielezea tu kumpa talaka mwanamke na wala hakugusia kuweka katazo la kuoa mke zaidi ya moja.

Hizi sheria za ndoa za sasa zilitafsiriwa kuendana na tamaduni za nchi kama Romania ambako dini ya kwanza ya kikristo ilizaliwa na hata hapo baadae dini nyingine zilipojiengua kitoka uroma, sheria za ndoa zilifanana na dini ya kwanza ya kikristo
 
Na ndio maana nimeamua nioe kitamaduni tu 😂😂😂
 
Kama Yesu hakuwa na mke kwanini wewe unaowa?? Alijua kuwa na mke sawa na kuwa na jini nyumbani🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…