Vijana wetu wa IT huko vyuoni wanafanya nini? Mbona kimya sana?

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Kibongo bongo kozi za kompyuta tushazoea kuziita kozi za IT ikiwemo computer science, computer engineering, IT, n.k.

Maisha ya sasa teknolojia ipo mbali sana na tunatembea, smartphones, internet, apps, n.k. zimekuwa sehemu ya maisha yetu.

Hapa bongo pametulia mno utadhani hatuna wanafunzi wa hizi kozi, hakuna pirika pirika.

Pirika pirika hizi ni mwanafunzi wa chuo fulani katengeneza app hasa inayoendana na mazingira yetu.

Mwanafunzi fulani kafikia hata robo fainali ya mashindano ya IT kimataifa.

Wanafunzi wa chuo fulani wanapiga pesa kwenye internet.

Migomo ya mtandaoni, mfano vifurushi vilipopanda bei tovuti mojawapo ingetunguliwa, ukiingia unakutana na bango likilaani vifurushi kupanda bei inaathiri kusomea mtandaoni.

Hatusikii hata wanafunzi watukutu wametungua system ya chuo wameiba mitihani ama kubadili marks.

Kimya sanaa, kumepoa mno.
 
Bado wanasoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna chuo kimoja juzi wanafunzi waliidukua na kulipa ada hewa..
Zaidi ya wanafunzi 200...hukusikia?
 
Wanangoja DP World waje waombe kazi.
 
Nenda DIT pale ,utajua mengi sana au tafuta scholars wa DIT wakuambie how good they are when it comes to coding
Wazee wa printf na studio.h watakuja hapa wakuelezee hapa

DIT Karibia kila MTU ni programmer pale (kidding)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…